Aziza Mbogolume (wa pili kulia) enzi za uhai wake wakati akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya Mwanamakuka 2013 kutoka kwa Mke wa Makamu wa Rais, Aisha Bilal. |
Baadhi ya viongozi waratibu wa shindano la Tuzo za Mwanakuka wakistaajabia kazi za mikono ya Aziza Mbogolume (wa pili toka kushoto) enzi za uhai wao katika maonyesho ya mwaka huu yaliyofanyika Escape 1 Mikocheni |
Kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO imepenyezewa na wasomaji wake na kuthibitishwa na Mshindi wa mwaka huu, aliyekuwa wa pili wakati marehemu Aziza akiibuka kidedea, Leila Mwambungu ni kwamba marehemu alikumbwa na mauti mchana wa saa 9 kutokana na tatizo la shinikizo la Moyo.
Inaelezwa kuwa kabla ya kukumbwa na mauti, Aziza aliyenyakua tuzo hiyo na kuzoa kitita cha Sh. Mil 6 toka kwa waandaji wa shindano hilo Marafiki Wanawake wa Tanzania UWF na kudhaminiwa na benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kwa kipaji chake cha kuchora picha mbalimbali za mapambo alikuwa akisumbuliwa na tatizo hilo.
"Ni kweli hata mwenzetu amefariki. Nilipigiwa simu na Mwenyekiti wa UWF, Mariam Shamo na kunijulisha na nimempigia mtoto wa marehemu naye amenithibitishia. Kwa kweli inasikitisha kwa sababu ni wiki iliyopita nimetoka kjuwasiliana naye na kuahidi kuja kuniona," alisema Leila kwa sauti na huzuni.
Leila alisema, yeye ametoka kujifungua na hivyo alimjulisha mshiriki mwenzake wa tuzo hizo na shoga wake juu ya kujifungua kwake salama na kumjulisha angeenda kumjulia hali na ghafla leo mchana napigiwa simu juu ya msiba wa Aziza.
Mipango ya mazishi ya marehemu Mwanamakuka huyo wa 2013 zinaendelea na MICHARAZO itawajulisha mara itakapopatra taarifa kamili.
Marehemu Aziza aliyezaliwa miaka zaidi ya 40 mjini Tabora na ameacha mtoto mmoja wa kike aliyekuwa akiishi naye Magomeni Mwembechai na kufanya shughuli zake za uchoraji na uuzaji wa bidhaa za mapambo eneo la Mwenge Vinyago. Mwenyezi Mungu Aiweke Roho ya marehemu Mahali Pepa Peponi. Innalillah Waina Illah Rajiun.
MICHARAZO inatoa pole kwa ndugu, familia na jamaa wa marehemu Aziza Mbogulume na kuwatakiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
No comments:
Post a Comment