BAADA YA kuzikanusha taarifa kwamba amerudiana na zilipendwa wake, Wema Sepetu imefahamika wazi kwamba Diamond Platnumz sasa ni kitu na box na mlimbwende huyo.
aada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Awali kulikuwa na taarifa wawili hao wamerudiana walipokuwa Malaysia Diamond alipoenda kutumbuiza na Wema kwa shughuli zake binafsi, lakini msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya alikanusha.
Hata hivyo picha zilizonaswa zimewaonyesha wawili hao walikuwa wakiuhadaa umma kwani hakuna ubishi ni ng'ari ng'ari mwanzo mwisho.
Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa
mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine
ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real
boyfriend wa Penny
Nini nitakachofuata...TUSUBIRI!
BaabKubwa
STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, October 9, 2013
Mbeya City yazidi kupepea, Azam, Mtibwa Sugar wazinduka
Mbeya City |
WAKATI Azam ikizinduka na kuondoka na 'mdudu' wa sare baada ya kuitungua Mgambo JKT mabao 2-0, wageni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mbeya City ya jijini Mbeya imeendelea kutakata baada ya kuisasambua Rhino Rangers nyumbani kwao mjini Tabora kwa kuilaza mabao 3-1.
Ushindi wa timu hizo mbili zimezifanya ziisogelee Simba kwa kufikisha pointi 14, moja pungufu na zile ilizonazo vinara hao ambao leo hawakushuka dimbani.
Azam ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na shukrani zikienda kwa kinda Faridi Mussa Maliki na Kipre Tchetche na kuipeleka Azam hadi nafasi ya pili mbele ya Mbeya City wakizidi kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine, Ruvu Shooting imetoshana nguvu dhidi ya maafande wenzao wa Oljoro JKT baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, mabao ya timu hizo yakifungwa na Elias Maguri wa Ruvu na Fikiri Mohammed wa Oljoro waliyofunga kila mmoja mawili.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Mtibwa Sugar imezinduka nyumbani kwao Manungu Morogoro baada ya kuwatungua JKT Ruvu mabao 2-1 na kujivuta hadi nafasi ya tisa.
Mabao mawili ya Juma Luizio yalitosha kuibeba Mtibwa ambao mwishoni mwa wiki walinyanyaswa na Yanga kwa kulazwa mabao 2-0, na mkongwe Salum Machaku akiifungia JKT bao pekee la kufutia machozi.
Mfanyabiashara mwingine amwagiwa Tindikali, safari hii Arusha
MFANYABIASHARA mkazi wa Sakina jijini Arusha, Japhet Minja anadaiwa kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni tindikali na watu wasiofahamika na kuachwa na majeraha usoni na mikononi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha zinasema kuwa Minja alikumbwa na tukio hilo eneo la Shamsi Kata ya Elarai baada ya kumwagiwa kimiminika hicho na kuachwa na maumivu makali.
Akizungumza katika hospital ya Seriani alikola wa, Minja ambae ni mfanyabiashara adai alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya masuala ya kibiashara na ghafla wakiwa njiani ghafla alizuiwa na watu hao waliofunga njia na kumdhuru.Daktari wa zamu aliyempokea mgonjwa huyo Godbless Masawe amesema walimpokea
mgonjwa huyo jana asubuhi akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na
kulazimika kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi na kwa sasa Minja anaendela vyema kwa sasa.
Yaillah Toba, Ajali nyingine tena yahusisha magari matatu
GA
Lori
la Mizigo likiwa limeacha njia leo, baada ya kugongana na basi katika
eneo la Kabuku mkoani Tanga na kuyahusisha magari matatu katika ajali
hiyo. (Picha na Francis Dande)
Askari wa usalama barabara wakiwa katika eneo la tukio.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali iliyoyakutanisha malori mawili pamoja na basi la abiria lenye namba za usajili T 158 BXG, iliyotokea leo katika eneo la Kabuku, mkoani TangaUchaguzi Bodi ya Ligi wapigwa dochi, Rufaa za wagoimbea TFF kupitiwa kesho
Na Boniface Wambura
UCHAGUZI wa viongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) sasa utafanyika Oktoba 25 mwaka huu badala ya Oktoba 18 mwaka huu.
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesogeza
mbele uchaguzi huo kutokana na maombi ya Kamati ya Ligi kwa vile baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Bodi hiyo kuwa vilevile wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa TFF.
TFF
itafanya Mkutano Mkuu wake Oktoba 26 mwaka huu ambao utakuwa na ajenda
za kawaida kama zilivyoainishwa katika Katiba yake wakati ajenda ya
uchaguzi itakuwa Oktoba 27 mwaka huu.
Wagombea
uongozi TPL Board ni Hamad Yahya Juma anayewania nafasi ya Mwenyekiti
wakati Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Abeid. Wanaowania nafasi za
ujumbe katika Kamati ya Uongozi ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib
Mwindadi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni
inatarajia wakati wowote kutangaza tarehe ya kuanza kampeni kwa wagombea
katika uchaguzi huo. Baraza la Bodi linaundwa na wajumbe 38 ambao ni
wenyeviti 14 wa klabu za Ligi Kuu na wenyeviti 24 wa klabu za Daraja la
Kwanza.
Wakati huo huo Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda
itakutana keshokutwa (Oktoba 10 mwaka huu) kusikiliza rufani
zilizowasilishwa mbele yake.
Waombaji
uongozi watatu wamekata rufani katika Kamati ya Jaji Luanda wakipinga
kutopitishwa kugombea katika uchaguzi wa TFF, uamuzi uliofanywa na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ajili ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba
27 mwaka huu.
Warufani
ni Samwel Nyalla aliyeondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji
kupitia Kanda namba 2 ya mikoa ya Mara na Mwanza kwa kutojaza kikamilifu
fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi TFF kwa kutoonesha malengo
yake.
Ayoub
Nyaulingo yeye anapinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya
Utendaji kupitia Kanda namba 6 (Katavi na Rukwa) kwa kutokuwa na uzoefu
uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
Naye
Ayoub Nyenzi amekata rufani kupinga kuondolewa kugombea ujumbe wa
Kamati ya Utendaji kuwakilisha Kanda namba 7 (Iringa na Mbeya) kwa
kushindwa kuthibitisha uraia wake.
Ndanda, Green Warriors hapatoshi leo FDL
Na Boniface Wambura
GREEN
Warriors ya Dar es Salaam na Ndanda ya Mtwara zinaumana kesho (Oktoba 9
mwaka huu) katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mshindi
atakamata uongozi wa kundi A.
Mechi
hiyo ya raundi ya tano itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam ambapo timu itakayoshinda itafikisha pointi kumi na kuipiku
African Lyon inayoongoza sasa kundi hilo ikiwa na pointi tisa.
Kwa
upande wa kundi B kutakuwa na mechi tatu ambapo Polisi Morogoro
inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi tisa itakuwa ugenini dhidi ya
Majimaji inayokamata mkia ikiwa na pointi moja. Mechi itachezwa Uwanja
wa Majimaji mjini Songea.
Kurugenzi
itakuwa kwenye uwanja wake wa Wambi ulioko Mafinga mkoani Iringa
kuikabili Burkina Faso ya Morogoro wakati Uwanja wa CCM Vwawa, Mbozi
mkoani Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Kimondo na Mkamba
Rangers.
Subscribe to:
Posts (Atom)