STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 3, 2015

Uchafu waikwaza Rio de Jeneiro Olimpiki 2016

Maeneo ya Fukwe za Rio De Jeneiro yatakayofanyika mashindano ya Olimpiki ya mwakani

Rais wa Kamati Kuu ya Kimataifa ya Olimpiki (OIC), Thomas Bach, amesema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo kwa jiji la Rio de Janeiro, Brazili katika maandalizi ya michuano ya hapo mwakani.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki.
Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao.
Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya wanariadha walioko kwenye mafunzo katika pwani hiyo wameona mizoga ya wanyama na uchafu ukiwa ukingoni mwa eneo hilo ambalo mashindano hayo yatafanyika.

Shule ya Joyland wahimiza amani Uchaguzi Mkuu 2015

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Wanafunzi  shule Darasa la nne Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wanafunzi  wa Darasa la awali  Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Capt 5
Wanafunzi waDarasa pili Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakicheza ngoma ya utamaduni (Ndolela) wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, Fedrick Otieno akiwasaidia watoto wa darasa la awali kupanda juu ya jukwaa kuimba wimbo maalum wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Skauti wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiruka sarakasi  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mhitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, Colin Christopher akisoma hotuba wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira akitoa hotupa ya awali kabla ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi akizungumza Tuangoma Kigamboni Dar es Salaam wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo
Na Tariq Badru
UONGOZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, umewaomba kuwa kuwakumbusha watanzania na hasa viongozi na wanasiasa kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Fredrick Otieno alisema vurugu za aina yoyote kutokana na ushindani wa kisiasa unaweza kuiweka Tanzania pabaya na kuvuruga kila kitu na kuwapa wakati mgumu watoto na watu wengine wasiojiweka ambao wanahitaji utulivu na amani kufanya mambo yao.
Otieno aliyasema hayo wakati wa hotuba yake katika mafahari ya wanafunzi wa masomo ya awali wa shule hiyo ya Joyland yaliyonyika mwishoni mwa wiki Tuangoma Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
"Leo wanafunzi na watoto wanafurahi na sisi wazazi na walezi tunajumuika pamoja shuleni kuwapongeza wahitimu wetu, kama kunakuwa na vurugu hili haliwezi kufanyika na watoto hawatapata haki yao ya kusoma au kufurahia maisha yao duniani," alisema Otieno.
Aliongeza ni vema wanasiasa, viongozi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi uliopo mbele yetu kwa amani na utulivu kwa hizo ni neema ambazo kwa mataifa mengine wanatafuta kwa vile nchi zao zimevurugwa kwa sababu na mambo hayo na mengine yaliyokimiza amani na utulivu.
Aidha aliwakumbusha wazazi nchini kote kujenga utamaduni wa kuwalipa ada watoto wao na kufuatilia nyendo za watoto wao wanapokuwa likizo na hata shuleni ili kurahisisha kazi kwa walimu katika kuwapa elimu itakayojenga misingi imara ya maisha yao ya baadaye. Alisema kwa mfano shuleni kwake wazazi na walezi wamekuwa wazito wa kulipa ada kiasi kwamba shule inadai zaidi ya Sh milioni 100, lakini wanashindwa kuwafukuza watoto kwa vile wanaamini hawana makosa yoyote na ndiyo maana wanataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika suala la elimu za watoto wao.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa hakuna hazina bora kama mtoto kupewa elimu ambayo huja kumsaidia ukubwani kwa kuzingatia kuwa dunia ya sasa inaendeshwa kisasa na bila elimu bora na ya kutosha ni vigumu kijana kusimama na kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira aliwasisitiza wazazi kutumia kujitolea na kutimiza wajibu wao kuwasomesha watoto badala ya kutumia fedha nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa watoto na familia zao kwa ujumla.
Shani alitoa nasaha yake kabla ya kumpisha Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi aliyesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga utamaduni wa ushirikiano dhidi ya walimu wa shule wanazosoma watoto wao.
Makingi alisema siyo kila jambo la wanafunzi kuachwa mikononi mwa walimu tu, kadhalika alikumbusha kuwasaidia watoto katika kuwalea katika maadili mema ili kulifanya taifa kuwa na raia wema na viongozi wazuri na waadilifu wa baadaye.