Rais
wa Kamati Kuu ya Kimataifa ya Olimpiki (OIC), Thomas Bach, amesema kuwa
uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo kwa jiji la Rio de Janeiro, Brazili katika maandalizi
ya michuano ya hapo mwakani.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo
waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila
linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki.Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao.
Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya wanariadha walioko kwenye mafunzo katika pwani hiyo wameona mizoga ya wanyama na uchafu ukiwa ukingoni mwa eneo hilo ambalo mashindano hayo yatafanyika.
No comments:
Post a Comment