Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda akiwa amelazwa kwenye chumba maalumu katika taasisi ya mifupa
Muhimbili (MOI), muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapojana.
Picha na Venance Nestory.
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa
majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka
Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa
bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisind
ikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
ikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema
kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh
walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku
huo huo. Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda
alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda
alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna
aliyeruhusiwa kumsogelea.
Muhimbili
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana
zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18
mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye
alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo.
Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi
kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo
alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada
ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.
“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja
asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa
analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate
matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
Taarifa ya polisi
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana
katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili
akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi
wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha.
MWANANCHI.