STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Newz Alert! Jengo analohubiria TB Joshua laporomoka Nigeria


Watu kadhaa wanahofiwa kufariki mjini Lagos Nigeria baada ya jengo moja linalohusishwa na muhubiri mashuhuri nchini humo TB Joshua kuanguka.

Ripoti zinasema kuwa miili kadhaa imetolewa katika vifusi vya jengo hilo.
church collapses
Shirika la kusimamia dharura nchini humo NEMA ,limesema kuwa jengo hilo ni la nyumba za kulala za wanachama wa kanisa la All Nations katika wilaya ya Ikotun.
Jengo hilo la ghorofa mbili lilikuwa likiongezwa ghorofa nyengine mbili lilipoanguka.
Maelfu ya watu mara nyingi uhudhuria maombi yanayoongozwa na TB Joshua anayejulikana kama mtume,kwa kuwa wanavutiwa na uwezo wake wa kuwaponya watu

Bright Mbwilo: Mwanasoka Afande anayetesa ktk muziki wa Injili


Kava la albamu ya Afande Bright kama linavyoonekana kwa anayehitaji kupata burudani hiyo anaweza kuwasiliana naye kupitia namba zinazoonekana pembeni au  barua pepe

Afande Bright Mbwilo katika pozi

NDOTO zake za utotoni zilikuwa aje kuwa mmoja wa nyota wa soka nchini kutokana na kuupenda mchezo huo anaoendelea kuucheza mpaka sasa akiwa na klabu ya Polisi-Pwani.
Kiu kubwa ya mafanikio katika soka ndiyo iliyomfanya Bright Job Mbwilo kuanza kucheza tangu akisoma Shule ya Msingi Magoye-Makete na baadaye Songwe Mbeya.
Hata alipojiunga na masomo ya Sekondari katika Shule ya Kilombero Day ya Ifakara na baadaye Iyula-Mbozi bado alikuwa akisakata kandanda na kuamini ndoto zake zitatimia.
Haikuwa ajabu kwake kuanza kupata umaarufu akiwa Songwe Stars akicheza kama mshambuliaji na wakati mwingine kiungo au beki wa kati kabla ya kutua Oljoro JKT iliyomsaidia kupata mafunzo ya kijeshi.
Mafunzo hayo yaliyofahamika kama Operesheni Kasi Mpya yalimpa ajira JKT kabla ya kuhamishiwa Mafinga JKT.
Kambi ya Mafinga ilikuwa na kikundi cha sanaa na Mbwilo maarufu kama Afande Bright alianza kujifunza kuimba baada ya wenzake kugundua kipaji kikubwa cha muziki alichonacho.
Kipindi kifupi alijipatia umaarufu na kuteuliwa kuwa mwalimu kwa wenzake katika masuala ya utunzi baada ya kutunga nyimbo za Uhamasishaji za 'Mwanzilishi wa JKT' na 'Naipenda Nchi Yangu'..
"Safari yangu kimuziki ilianzia hapo na kujitosa muziki wa kizazi kipya kabla ya mwishoni mwa mwaka jana hasa nilipoteuliwa na Shaibu Issa kujiunga JKT Ruvu nikitokea Rhino ya Mafinga mwaka 2007."

 
KIPAJI
Mwaka 2008 alinyakuliwa na Prisons Mbeya na kupata mafunzo Magereza huku akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu msimu wa 2009 kabla ya kuhamishiwa Iringa.
Akiwa Iringa alijiunga na Polisi Iringa kabla ya kwenda kusomea Ukutubi Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo na kuanza kushiriki matamasha ya muziki na kufunguliwa neema.
Matamasha hayo yalimfanya apate nafasi ya kurekodi wimbo wake wa kwanza wa Bongofleva uitwao 'Tanzania' aliomshirikisha Mirror.
Baada ya hapo alirekodi nyimbo nyingine kadhaa zilizokuja kuzaa albamu yake ya kwanza iliyofahamika kama Tanzania iliyokuwa na nyimbo nane.
Baadhi ya nyimbo hizo ni; 'Ndani ya Dancehall', 'Zako Style', 'Kiza Kinene', 'Jakaya', 'Nimedata', 'Hawapendi', 'Watanzania', 'Nikiachwa leo' na 'Leave Me Alone'.
Novemba mwaka alipohitimu Stashahada ya Ukutubi, alirejea kwao Mbeya na kuwa miongoni mwa wachezaji waliojaribiwa na Mbeya City kwa ajili ya usajili.
Hata hivyo kwa namna ya ajabu wakati akiendelea na mazoezi ili kusubiri kutangazwa watakaosajiliwa aliugua ghafla kichwa.

 
MATESO
Mbwilo anayezishabikia Chelsea, Barcelona na JKT Ruvu anasema kichwa kilimpa mateso makubwa, licha ya kuzunguka hospitali kadhaa kubwa ikiwamo ya Aga Khan.
"Mateso niliyopata kwa maumivu ya kichwa yaliyoshindwa kubainika katika hospitali zote nilizoenda kutibiwa kiasi cha kukata tamaa na kutamani kujiua kwa kujirusha ghorafani."
Anasema siku aliyokusudia kujiua ilitokea miujiza kwa kuokolewa na mama zake kabla ya kupelekwa kanisani kuombewa na ndipo ikawa sababu ya kupona kwake na kumpokea Yesu.
"Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walibaini mimi nilikuwa mmoja wa waimbaji wa muziki wa kizazi kipya na kunishawishi kumuimbia Bwana na sikuwa na hiyana," anasema.
Anasema kupitia ufadhili wa Papaa Delinson alirekodi albamu nzima ya Asante Bwana yenye nyimbo nane ambazo ameanza kuzitengenezea video kupitia kampuni ya HMC ya mjini Moshi.
Nyimbo za albamu ya msanii huyo anayeshukuru soka kumpa ajira jeshini ni 'Asante Bwana', 'Upendo', 'Vita', 'Hamjui', 'Itakuwaje', 'Twakuheshimu', 'Jinsi Gani' na 'Vita Remix'
Mbwilo anasema ndoto zake kumtumikia Mungu kwa kadri awezavyo ili kurejesha shukrani kwa wema aliomtendea kwa kumuokoa na kifo na tayari ameanzisha kundi liitwalo Makomandoo wa Yesu.
Kundi hilo linalotoa huduma katika makongamano na makanisani linaundwa na wasanii watatu akiwamo yeye (Afande Bright), mdogo wake Robert Mbwilo na Eliah Michael.
Pia anatamani kulitanua kundi hilo na kusaidia wasanii wenye vipaji vya sanaa ili kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa madai kuwa asilimia kubwa ya vijana kwa sasa wamejiajiri kwenye sanaa.

 
WITO
Mbwilo mwenye ndoto za kufika mbali kisanii anawataka wasanii wenzake kuwa wabunifu na kuacha    kujikita kwenye matumizi ya dawa za kulevya kadhalika wajitambua kama waelimishaji umma.
Pia ameiomba serikali kutunga sheria kali zitakazoweza kumkomboa msanii kupitia jasho lake sawia na kumwezesha kujiweza kisha ndipo wawakamua 'kodi' kinyume na inavyofanyika sasa.
"Huwezi kumkama Ng'ombe bila kumpa malisho, serikali imekuwa ikimbana na kumkamua msanii kupitia stika bila msanii kuanza kukusanya mapato, hii ni ajabu na inakatisha tamaa," anasema.
Mbwilo mwenye mke na mtoto mmoja hupenda kula wali kwa maharage na kunywa Fanta anamshukuru familia yake yote hasa mama yake mzazi Mwalimu Nesi Mziho, Papa Delinson na Enock Masanja wa HMC Production aliyebeba jukumu la kumrekodi video.
"Namshukuru sana Enock Masanja kwa kukubali kubeba jukumu la kurekodi na kusambaza video ya albamu yangu, pia Papaa Denilson na familia yangu nzima kwa kunisapoti kwa hali na mali pamoja na wanasoka wenzangu wote." anasema askari Magereza huyo.

Ni shidaa leo England, Arsenal uso kwa uso na watetezi Man City


KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England, kinatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii baada ya kupisha michezo ya Kimataifa wiki mbili zilizopita ambapo leo Jumamosi Arsenal itavaana na watetezi Manchester City.
Mwezi uliopita, Arsenal iliichapa Man City Bao 3-0 Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Hisani lakini kwenye Ligi Arsenal wameshinda Mechi moja na kutoka Sare Mechi 2 zilizopita.
Nao Man City walianza kwa ushindi katika Mechi mbili za kwanza lakini kwenye Mechi yao ya mwisho Uwanjani kwao Etihad walitandikwa 1-0 na Stoke City.
Mbali ya Mechi hii, Chelsea, ambao wanaongoza Ligi kwa kushinda Mechi zao zote 3, watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Swansea City ambao ndio wamefungana nao kileleni na ambao pia wameshinda Mechi zao zote 3.
Lakini Chelsea huenda wakamkosa Straika wao Diego Costa mwenye  mabao manne na aliyeshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti kutokana na kuwa majeruhi.

RATIBA kamili ipo hivi:
Leo Jumamosi
14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa
Kesho Jumapili
18:00 Man United v QPR
Jumatatu
22:00 Hull v West Ham

Steve Nyerere abwanga manyanga Bongo Movie Unity kama Mtitu

http://api.ning.com/files/ZZRe-BUg83mT6Wyu86ZmDINS*-9-PEciDm-LquUgZ8-ItEbclBzA4sJFyXnJzi40YGDHA2Fg4GGg3Ljg2km*PE0f884ZqnJu/SteveNyerere_full.jpg 
MUIGIZAJI na mchekeshaji anayenakili sauti za watu mashuhuri, Steve Nyerere aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.
Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake.
“Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani tulifurahi pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja.” 
Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa filamu za kitanzania ambao wengine wamemtaka kutofanya hivyo huku wakitaja ‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote.
“Khaaaaaaa asa @stevenyerere2 kujihuzur sio suluhisho la tatizo kaanza willy umefata ww sasa c kamat nzima itajiuzur!?? Why mnashindwa kukaa km wasanii mkasuluhisha penye makosa mambo yakaendelea? Majungu yapo kila sehem kusemwa kupo kila sehem @stevenyerere2 mnapoelekea bongomovie kila mtu atakaa mwenyewe wallah.” Ameandika shabiki anaetumia jina la Neyjd.

Yanga wakubali yaishe kwa Twite yawaita Fc Lupopo mezani

http://api.ning.com/files/3I-9LvQkoOSAPbzeGPW5yP6OSfiIe*zDKxvTvEruLBnPGhxkE3j8HJX2IRwtbIWsugVPQAhAda5j3SU7tPM2CI5dsqk6mOCF/MBUYUTWITESALAMAJAMANIPIXNO5.jpg
Mbuyu Twite
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema umeshangazwa na wenzao wa timu ya a FC Lupopo ya JK Kongo kudai Mbuyi Twite alijiunga nao kwa mkopo, hata hivyo wameamua kuwaita mezani kumaliza mambo kiutu uzima tofautis na tisho la Lupopo kutaka kukimbilia FIFA kushtaki.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Beno Njovu, alisema Yanga haikumsajili Twite kwa mkopo.
Akifafanua zaidi, Njovu, alisema Lupopo inataka ilipwe fedha zaidi mara baada ya Yanga kumuongezea mkataba Twite baada ya ule wa awali kumalizika.
"Mbali na malalamiko mengine ya wenzetu, pia wanataka walipwe pesa baada ya Twite kuongezewa mkataba.. lakini kwenye mkataba hakuna makubaliano kama hayo wakati tunamchukua Twite," alisema Njovu.
Aidha, alisema kuwa ili kuweka mambo sawa, Yanga imewasiliana na viongozi wa Lupopo ambao siku yoyote kuanzia leo watawasili nchini kwa ajili ya mazungumzo.
"Tumewapigia simu hao jamaa na watawasili nchini kuanzia kesho, tutakaa kuwaelewesha na naamini tutaelewana..., ila nataka muelewe kuwa hatukumchukua Twite kwa mkopo," aliongezea kusema Njovu.

Halima Mdee aibuka kidedea CHADEMA, asema la moyoni

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/HalimaMdee.jpg
MWANASIASA machachari ambaye pia ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee CHADEMA amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chama hicho (BAVICHA) unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mdee aliwaasa wanawake kwa wanawake kuwa wamoja badala ya kupigana vijembe wao kwa wao ili maendeleo ya mwanamke yaweze kupatina na na kuondokana na mfumo dume
“Nimezoea kuona watu wanaotukashifu ni wa upande wa pili kutokana na mfumo dume uliojengeka na sio wanawake wenyewe kukashifiana,” alisema.
Alisema mwanamke ana nguvu ya kuleta mabadiliko na kueleza kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kipo madarakani kwa sababu kinawatumia wanawake na kutaka nao kuungana na kuwa kitu kimoja.
“Mwanamke ana nguvu ya kuleta mabadiliko, bila kuwatumia  hakuna ushindi na wanawake siku zote wanamsimamo na sio wasaliti hata kidogo,” alisema Mdee.
Aidha aliwataka wanawake wakafanye kazi majimboni kwa umoja licha ya kufahamu wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha.
“Harakati zetu sio za starehe na hata ikiwezekana pindi mnapokuwa majimboni bila kujali mnalala wapi, mnatumia choo cha ‘pasipoti size’ ili mradi ushindi unapatikana,” alisema.
Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana, Arcado Ntagazwa, alisema Mdee alipata kura 165 akifuatiwa na Janeth Rithe 35, Sophia Mwakagenda 18, Chiku Abwao 15, Lilian Wassira 11 na Rebecca Magwishe kura 4.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti upande wa Bara, alitangazwa Hawa Mwaifunga aliyejinyakulia kura 136 akifuatiwa na Victoria Benedict kura 99.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ilichukuliwa na Hamida Abdalah Huewishi aliyepata kura 194 akifuatiwa na Mariamu Msabaha kura 36.

Hivi ndivyo wahitimu wa la 7 Brain Trust School walivyoagwa jana

Skauti walioongoza maandamano wa kuingia kwenye eneo la tukio
Ni wakakamavu kudhihirisha ni mashujaa wa kesho
Kwa mwendo wa pole mbele tembeaaaaaa!

Matarumbeta yalikuwapo kusapoti sherehe hizo
Wahitimu wakielekea kwenye eneo la tukio



Maandamano fulani ya kuonyesha furaha yao ya kuhitimu Darasa la Saba
Mkuu wa Shule ya Msingi, Neville Marandu akizungumza machache, huku Mkuu wa Shule za Brain Trust, Irene Makinda (pembeni yake kulia) akiwa bize


Hawa nao walikuwapo kushuhudia kila kitu kwa umakini zaidi
Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria sherehe hizo jana Yombo Vituka

Wazazi na walezi wakiwa makini kufuatilia kila tukio katika mahafali hayo
Hakuna aliyetaka kupitwa na jambo au asimuliwe na mtu



Gift Marandu akisoma shairi mbele ya hadhira kwa umahiri mkubwa

Kama Mwanamalenga katika ughani mashairi
Dada zao wa Sekondari nao walikuwapo kuwapa mkono wa kwaheri

Kwa herini wadogo zetu, heri twawatakia, makini muwapo makwenu....
Dada zao wa Sekondari wakiendelea kuwaburudisha kwa kuwaimbia ngonjera na nyimbo

Ikawa zamu ya wahitimu wenyewe kuingia kilingeni kuonyesha umahiri wao
Kwa kujiamini wahitimu wakiingia uwanjani kuangusha burudani la mwisho mwisho


Kazi ikaanza kwa kuimba wimbo
Wakaangusha na ngonjera

Mashairi pia yalikuwapo
Wahitimu wa Elimu ya msingi wa Shule ya Brain Trust wakiendeleza kutoa burudani

Samuel Robert (kulia) akawaongoza wenzake kuangusha njongera
Dogo achana naye ana kipaji cha kughani acha bhana!


Kwa mbwembwe ndiyo kabisaaaaa
 

Ikawa zamu ya mwanadada naye kuonyesha makeke yake

Skauti nao wakaingia uwanjani kuonyesha umahiri wao katika sanaa hiyo
Hayaaaa twende

Ni nyuma geuka, kulia geuka kwa ukakamavu kama maafande
 






Ikaja zamu ya mwnafunzi huyo wa Chekechea Mereciana Ronald ambaye aliangusha burudani ya kufa mtu
Anacheza kwa pozi taratibu kama hataki

Kadri mzuka ulivyokuwa ukimpanda ndivyo alivyoongeza makeke kwa kunengua muziki
 

Akachanganya kasi we kama Aisha Madinda

Hapo chachaaaa! Yebaaaa
Mkuu wa Shule ya Msingi Brain Trust, Neville Marandu akisoma wasifu wa shule
Mgeni rasmi ikafika zamu yake kutoa nasaha zake ni Richard Mngomo wa Tanzania Printers
Msiridhike na kumaliza kwenu la Saba bado mna kazi kubwa mbele yenu, ndivyo alivyowanasihi wahitimu
Wahitimu wakaanza kukabidhiwa vyeti vyao

Immaculata Justine Limonga, naye alitunukiwa cheti na mgeni rasmi wa mahafali hayo
Ilikuwa furaha kwa wahitimu baada ya kukabidhiwa vyeti vyao
Immaculata Justine akiwa katika picha mbalimbali na familia yake baada ya kukabidhiwa cheti cha kuhitimu darasa la saba katika shule ya Brain Trust

Anafanyiwa surprise
 

Pokea keki ya zawadi mwanangu

Mdogo mtu anampokea keki ya zawadi

Daa nitaifaidije hiii
Akifurahia zawadi ya Mwanafunzi Mwenye Nidhamu na Msafi kuliko wote Brain Trust School