STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 8, 2016

Simba yaikwepa Yanga kiaina, kuvaana na Mtibwa

Mashabiki wa Simba wanaosubiri kuipa sapoti timu yao Jumapili jioni dhidi ya Mtibwa Sugar
BAO pekee la Jonas Mkude la dakika ya 65 limeiwezesha Simba kutinga nusu fainali na sasa itaavana na Mtibwa Sugar jioni ya Jumapili, ikikwepana kuvaana na Yanga iliyotangulia mapema tangu jana.
Kulikuwa na dalili za Simba kuvaana na Yanga kama matokeo yangeisha kwa sare ya 0-0, lakini bao la Mkude liliweka mambo sawa na sasa vijana wa Msimbazi watakuwa wakinoa makucha yao ili kuvaana na Mtibwa waliocheza nao fainali za mwaka jana na kuichapa kwa mikwaju ya penalti.
Yanga wenyewe itakuwa na kibarua dhidi ya URA ambayo mapema jioni ya leo ilipata ushindi wa baoa 1-0 dhidi ya Jamhuri.
Kama Yanga na Simba zitavuka hatua hiyo zitaumana Jumatano usiku kwenye fainali ikirejea fainali za mwaka 2011, ambazo Simba ilitwaa taji lake la pili kwa kuizabua Yanga mabao 2-0.

Simba inaoongoza kwa bao 1-0 dhidi ya JKU

SIMBA inaongoza bao 1-0 baada ya Jonas Mkude kuipatia bao la kichwa katika dakika ya 65. Pambano bado ni kali na kuna dalili za wapinzani wajadi Simba na Yanga kutokutana katika hatua ya nusu fainali.

Claudio Makelele apewa shavu Monaco


http://img1.cfstatic.com/psg/claude-makelele_35549_wide.jpg
Claudio Makelele
KLABU ya Monaco ya Ufaransa, imemteua kiungo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Claudio Makelele kuwa Mkurugenzi Mpya wa Ufundi. 
Klabu hiyo ilitangaza jana Alhamisi uteuzi wa nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, ikielezea kuwa, kibarua chake kikubwa kitakuwa ni kumsaidia Makamu wa Rais Vadim Vasilyev kuongoza upande wa michezo wa timu hiyo. 
Makelele alitimuliwa kibarua cha kuinoa Bastia Novemba 24, 2014 baada ya kufanya kazi kama Kocha Msaidizi katika klabu ya Paris Saint-Germain. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo, Makelele amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo muhimu katika soka la Ufaransa na kuahidi kufanya bidii na kuisaidia timu hiyo.
Enzi za uchezaji wake, mkali huyo alikuwa akitawala dimba la kati kiasi cha kuwapa wakati mgumu wapinzani wake.
 

Simba yaisaka Yanga kimtindo

DAKIKA 45 za kwanza za pambano la kukamilisha ratiba kati ya Simba na JKU zimemalizika matokeo yakiwa bao 0-0.
Pambano ni kali na Simba itajilaumu kwa kukosa angalau bao hata moja katika dakika hizo kutokana na kukosa mabao ya wazi.
Kama matokeo yataendelea hivi Simba itakuwa imeangukia mikononi mwa Yanga waliomaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi B. URA wanaoongoza kundi A tayari imeshatinga nusu fainali, kama ilivyo kwa Mtibwa Sugar, lakini hakuna anayejua atacheza na nani Jumapili ijayo mechi za nusu fainali zitakazpochezwa jioni na usiku.

Sunderland wanasa kifaa toka Bayern Munich

https://i.guim.co.uk/img/media/714c8f8cc7ab15b56bb5fb6c9eb01c24b719ae6c/0_149_5128_3080/master/5128.jpg?w=620&q=85&auto=format&sharp=10&s=daec3160be3fec2cb53a6ae0d3112b65IKIWA na kibarua kigumu wikiendi hii dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Sunderland imetangaza kumsajili beki wa Bayern Munich, Jan Kirchhoff kwa ada ambayo haikuwekwa wazi.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25, alianza soka lake katika timu ya Mainz kabla ya kujiunga na Bayern mwaka 2013, akiwa pia amecheza kwa mkopo Schalke ametua kwa Paka Weusi hao kabla ya kuvaana na Arsenal kwenye mechi ya mzunguko wa tatu wa michuano ya Kombe la FA.
Meneja wa Sunderland, Sam Allardyce aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Jan ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu pamoja na umri mdogo alionao hivi sasa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anaamini beki huyo atazoea haraka mazingira katika klabu hiyo na kuwasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.
Sunderland iko katika mapambano ya kutoshuka daraja wakishika nafasi ya 19 katika msimamo wakiwa na alama 15 katika michezo 20 waliyocheza.

Sanchez bado hakijaeleweka Emirates

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2015/01/11/14/Alexis-Sanchez.jpgBADO hakijaeleweka tu. Kocha wa  Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa straika wake matata, Alexis Sanchez ataukosa mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Sunderland ikiwa kama tahadhari.
Nyota huyo wa kimataifa wa Chile amekuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kupata majeruhi ya misuli katika mchezo dhidi ya Norwich City, Novemba 29 mwaka jana.
Sanchez alikuwa akitegemewa kurejea uwanjani kabla ya Krismasi, lakini alichelewa kupona na Wenger hayuko tayari kumwahisha kutokana na kukabiliwa na mechi ngumu za za Ligi Kuu dhidi ya Liverpool na Stoke City wiki ijayo.
Akizungumza katika mtandao wa klabu hiyo, Kocha Wenger amesema taarifa mbaya aliyonayo wiki hii ni kukosekana kwa Sanchez ambaye pamoja na kupona, lakini ameamua kumpa muda zaidi kama tahadhari.
Wenger ameendelea kudai kuwa kiungo Mikel Arteta atakuwepo katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza toka Novemba 21 wakati Tomas Rosicky naye ataanza mazoezi rasmi wiki ijayo baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Arsenal ndio wanaoongoza kwa sasa msimamo wa Ligi Kuu ya England  ikiwa na pointi 42, mbili zaidi na ilizonazo Manchester City wanaofuata nyuma yao.

Dortmund na sizitaki mbichi kwa Januzaj

http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/67/590x/Adananjjjj-604533.jpgKLABU ya Borussia Dortmund imedai ulikuwa ni uamuzi wa Adnan Januzaj mwenyewe kurejea Manchester United na kukiri dili lake halikuwa na manufaa kwa klabu yoyote. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Dortmund kwa mkopo wa msimu mzima mwishoni wa Agosti mwaka jana, lakini amefanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 12 pekee. 
Kurejea kwa Januzaj Old Trafford kulifanywa rasmi jana na mkurugenzi wa michezo wa Dortmund amekiri kuwa kusitisha mkataba wa nyota huyo ni jambo bora kwa pande zote husika. 
Mkurugenzi huyo amesema yalikuwa ni mapendekezo ya Januzaj mwenyewe kurejea United na uwepo wake Dortmund haukuwa na faida yeyote kwa klabu hiyo.
Man imemrejesha winga huyo kwa ajili ya kuimatrisha kikosi chake baada ya Kocha Louis Van Gaal kuuza wachezaji wake kadhaa nyota akiwamo Nani, Chicharito na Angel di Maria

Samatta sasa kina kona, anukia Nantes

KLABU ya Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 ya Nantes inaripotiwa kuanza mazungumzo rasmi na wawakilishi wa Mbwana Samatta pamoja na klabu ya TP Mazembe. 
Klabu hiyo imedaiwa kuwa ina nia ya kupata saini ya Samatta katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ili iweze kumtumia kwa msimu uliobakia. 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa Samatta, Nantes inataka kila kitu kimalizike kabla ya Januari 20. Nantes inamtaka Samatta ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo msimu huu inaonekana kuwa butu kwa kufunga mabao 14 pekee. 
Nantes inashikilia nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 19 ikikusanya jumla ya pointi 24.
Timu hiyo Jumapili itashuka uwanjani kuvaana na St Entienne katika mfululizo wa ligi hiyo.

HIKI NDIKO KIKOSI AMBACHO SAMATTA NAYE NDANI

MBWANA Samatta jana alirejea tukio lililowahi kufanywa na straika wa kimataifa nchini, Haji Dilunga alipoteuliwa timu ya Afrika sambamba na kipa Omary Mahadhi mwaka 1973 baada ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Afrika 2015 sambamba na nyota wengine.
Kikosi kamili kipo hivi;


NI SIMBA VS YANGA MAPINDUZI AU YANGA V JKU?

http://24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/09/9072Simba-Yanga.jpgKLABU ya Yanga inasubiri kujua itacheza na nani kati yake na watani zao Simba au URA ya Uganda katika mechi za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
URA imekuwa timu ya tatu kutinga hatua hiyo baada ya jioni ya leo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba na kuiacha nafasi moja kwa 'Mnyama' ili kujua itaangukia kileleni au nafasi ya pili.
Kama Simba ambayo usiku huu itavaana na JKU ya Unguja, itashinda mchezo huo, itaikwepa Yanga na hivyo kusubiri kuona kama zitakutana fainali Jumatano ijayo.
Iwapo Simba itatokla sare au kupoteza itaangukia nafasi ya pili na kuingia 18 za vijana wa Jangwani ambao usiku wa jana ilipasta ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa.
Simba ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ya Mapinduzi iliyoasisiwa mwaka 2007 ina pointi nne mpaka sasa ikiwa nafasi ya pili, nyuma ya URA ilitimiza pointi 6 baada  ya ushindi wake wa jioni huu kwa bao la Saio Kyayune  la dakika za lala salama.
Kama timu hizo kongwe nchini zitakwepana hatua hiyo ya nusu fainali kulingana na matokeo ya usiku wa leo, basi zinaweza kukutana fainali na kurejea fainali za mwaka 2011 ambapo Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba kwa mabao ya Mussa Hassan Mgosi na Shija Mkina.

Nusu fainali:
J'Pili Jan 10
Samba/JKU v Mtibwa Sugar Saa 10:15 jioni
Yanga v Simba/JKU Saa2:15 usiku

Msimamo
Kundi A

                P  W D  L  F A Pts
URA          3   2  0  1 4 2  6*
Simba       2   1  1  0 3 2  4
JKU           2   1  0  1 4 3  3
Jamhuri     3   0  1  2 2 6  1

Kundi B

               P  W D  L  F  A Pts
Yanga      3   2  1  0  6  2  7*
Mtibwa     3   1  1  1  3  3  4*
Mafunzo   3   1  0  2  2  5  3
Azam       3   0  2  1  3  4  2
* Zimefuzu nusu fainali

Wafungaji:

2-Donald Ngoma (Yanga)
   Awadh Juma (Simba)
   Villa Oromuchan (URA)
   Mohammed Abdallah (JKU)
  Kipre Tchetche (Azam)
1-Paul Nonga (Yanga)
  Hussein Javu (Mtibwa)
  John Bocco (Azam)
  Oscar Aggaba (URA)
  Emmanuel Martin (JKU)
  Said Bahanuzi (Mtibwa)
  Vincent Bossou (Yanga)
  Mwalimu Khalfan (Jamhuri)
  Ammy Bangaseka (Jamhuri)
  Nassor Juma      (JKU)
  Ibrahim Ajib      (Simba)
  Rashid Abdalla (Mafunzo)
  Sadick Rajab   (Mafunzo)
  Saio Kyayune   (URA)
  Shiza Kichuya  (Mtibwa)
  Issofou Boubacar (Yanga)
  Malimi Busungu  (Yanga)

Orodha ya Mabingwa

2007  Yanga SC
2008  Simba SC
2009  Miembeni
2010  Mtibwa Sugar
2011  Simba SC
2012  Azam FC 
2013   Azam FC
2014  KCCA      
2015  Simba SC
NB:Simba imeingia fainali nyingi za Mapinduzi (5) ikifuatiwa na Mtibwa (4)

Samatta aanza kupokea pongezi za tuzo yake

HONGERA. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa shirika la ndege la Ethiopia.
Wakati Huo huo Shirikisho la Soka Tanzania, TFF limetuma salamu za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani Zanzibar.
Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.
Mazishi ya marehemu Suleiman Ally Hemed yamefanyika jana Alhamisi jioni mjini Zanzibar.

MWANAUMEEEEEEEEEEEEEEEE NI MBWANA SAMATTA

 
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/01/samatta-1.jpg
Add caption
MWANASOKA Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ni Mbwana Samatta, huku Yaya Toure MBWANA Samatta kila kona. Mwanasoka wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa kuamkia leo ameweka rekodi ya kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani. Samatta amekuwa Mtanzania wa kwanza kunyakua tuzo hiyo baada ya kuwashinda Robert Kidiaba na Baghdad Bounedjah.
Hiyo ni tuzo ya pili kwa Samatta baada ya ile ya Mfungaji Bora wa Afrika akiwa ameisaidia klabu yake ya TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2015.
Klabu hiyo ya Mazembe ilishinda tuzo ya Klabu Bora Afrika, huku timu ya taifa ya Ivory Coast ikishinda tuzo Timu bora ya Afrika kwa wanaume na Cameroon ikishinda kwa upande wa wanawake.
Mfaransa Herve Renard, Kocha wa Ivory Coast alitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka kwa mara ya pili baada ya mwaka 2012 kunyakua pia tuzo kama hiyo alipoisaidia Zambia kutwaa ubingwa wa Afrika na  kufikia rekodi ya  Bruno Metsu aliyenyakua mwaka 2001-2002
Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2015 ni Pierre-Emerick Aubameyang, akimpikua Yaya Toure wa Ivory Coast na Andre Ayew wa Ghana.

ORODHA KAMILI YA WASHINDI
MCHEZAJI BORA WA AFRIKA - Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA – Mbwana Aly SAMATTA
MCHEZAJI BORA WA KIKE - Gaelle ENGANAMOUIT (Cameroon)
MCHEZAJI BORA KIJANA - Victor OSIMHEN (Nigeria)
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA VIZURI - Etebo Peter OGHENEKARO (Nigeria)
KOCHA BORA WA MWAKA- Herve RENARD (Ufaransa) – Kocha wa zamani wa Ivory Coast
REFA BORA WA MWAKA - Bakary Papa GASSAMA (Gambia)
TIMU BORA YA TAIFA – Ivory Coast
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE- Cameroon
KLABU BORA YA MWAKA - TP Mazembe (DRC)
GWIJI WA AFRIKA - Charles Kumi GYAMFI (Ghana)
Samuel MBAPPE LEPPE (Cameroon)

KIKOSI BORA AFRIKA

Kipa: Robert Muteba KIDIABA (DRC)
Mabeki: Serge AURIER (Ivory Coast), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)
Viungo: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Ivory Coast), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria),    
Washambuliaji: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria) 

WACHEZAJI WA AKIBA;

Djigui DIARRA (Mali)
Azubuike OKECHUKWU (Nigeria)
Kelechi NWAKALI (Nigeria)
Zinedine FERHAT (Algeria)
Adama TRAORE (Mali)
Victor OSIMHEN (Nigeria)

Kermit ERASMUS (Afrika Kusini)