KLABU ya Yanga inasubiri kujua itacheza na nani kati yake na watani zao Simba au URA ya Uganda katika mechi za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
URA imekuwa timu ya tatu kutinga hatua hiyo baada ya jioni ya leo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba na kuiacha nafasi moja kwa 'Mnyama' ili kujua itaangukia kileleni au nafasi ya pili.
Kama Simba ambayo usiku huu itavaana na JKU ya Unguja, itashinda mchezo huo, itaikwepa Yanga na hivyo kusubiri kuona kama zitakutana fainali Jumatano ijayo.
Iwapo Simba itatokla sare au kupoteza itaangukia nafasi ya pili na kuingia 18 za vijana wa Jangwani ambao usiku wa jana ilipasta ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa.
Simba ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ya Mapinduzi iliyoasisiwa mwaka 2007 ina pointi nne mpaka sasa ikiwa nafasi ya pili, nyuma ya URA ilitimiza pointi 6 baada ya ushindi wake wa jioni huu kwa bao la Saio Kyayune la dakika za lala salama.
Kama timu hizo kongwe nchini zitakwepana hatua hiyo ya nusu fainali kulingana na matokeo ya usiku wa leo, basi zinaweza kukutana fainali na kurejea fainali za mwaka 2011 ambapo Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba kwa mabao ya Mussa Hassan Mgosi na Shija Mkina.
Nusu fainali:
J'Pili Jan 10
Samba/JKU v Mtibwa Sugar Saa 10:15 jioni
Yanga v Simba/JKU Saa2:15 usiku
Msimamo
Kundi A
P W D L F A Pts
URA 3 2 0 1 4 2 6*
Simba 2 1 1 0 3 2 4
JKU 2 1 0 1 4 3 3
Jamhuri 3 0 1 2 2 6 1
Kundi B
P W D L F A Pts
Yanga 3 2 1 0 6 2 7*
Mtibwa 3 1 1 1 3 3 4*
Mafunzo 3 1 0 2 2 5 3
Azam 3 0 2 1 3 4 2
* Zimefuzu nusu fainali
Wafungaji:
2-Donald Ngoma (Yanga)
Awadh Juma (Simba)
Villa Oromuchan (URA)
Mohammed Abdallah (JKU)
Kipre Tchetche (Azam)
1-Paul Nonga (Yanga)
Hussein Javu (Mtibwa)
John Bocco (Azam)
Oscar Aggaba (URA)
Emmanuel Martin (JKU)
Said Bahanuzi (Mtibwa)
Vincent Bossou (Yanga)
Mwalimu Khalfan (Jamhuri)
Ammy Bangaseka (Jamhuri)
Nassor Juma (JKU)
Ibrahim Ajib (Simba)
Rashid Abdalla (Mafunzo)
Sadick Rajab (Mafunzo)
Saio Kyayune (URA)
Shiza Kichuya (Mtibwa)
Issofou Boubacar (Yanga)
Malimi Busungu (Yanga)
Orodha ya Mabingwa
2007 Yanga SC
2008 Simba SC
2009 Miembeni
2010 Mtibwa Sugar
2011 Simba SC
2012 Azam FC
2013 Azam FC
2014 KCCA
2015 Simba SC
NB:Simba imeingia fainali nyingi za Mapinduzi (5) ikifuatiwa na Mtibwa (4)
No comments:
Post a Comment