MECHI
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana
(Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh.
26,455,000.
Watazamaji
4,741 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na
ushindi wa mabao 2-1. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh.
20,000.
Mgawanyo
kwa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47,
gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh.
5,460,687.63.
Uwanja
sh. 2,776,620.83, gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh.
1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.
|
Jamal Malinzi |
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha daktari wa
tiba ya michezo, Dk. Hemed Mziray kilichotokea juzi jijini Dar es
Salaam.
Dk.
Mziray ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Manispaa ya Temeke na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Tiba ya Michezo Tanzania
(TASMA) amesafirishwa kwenda kwao mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya
mazishi.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Dk. Mziray ameshirikiana na TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu
katika masuala ya tiba na uongozi.
Alikuwa
kiungo kati ya Uwanja wa Taifa ambapo mechi za kimataifa, za ligi na za
kirafiki zimekuwa zikichezwa na Hospitali ya Temeke kwa wagonjwa
wanaohitaji huduma zaidi, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
imetoa pole kwa familia ya marehemu Dk. Mziray, TASMA na wafanyakazi wa
Hospitali ya Temeke na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia TFF inatoa ubani wa sh.
200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake. Bwana alitoa,
Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina