WINGA wa Bayern Munich, Arjen Robben anaona kwamba mambo yamekuzwa mno tangu walipotolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Mabingwa hao waliokuwa watetezi walitolewa kwa jumla ya mabao 5-0, na kusababisha mbinu za ufundishaji za kocha Pep Guardiola kupingwa kufuatia kipigo cha 4-0 nyumbani katika mechi yao ya marudiano.
Wakiwa wameshatwaa ubingwa wa Bundesliga mapema zaidi katika historia msimu huu, kikosi cha Guardiola kinawania taji la pili la Kombe la 'FA' (DFB-Pokal), dhidi ya Borussia Dortmund katika fainali na Robben anaona kwamba hawastahili kusakamwa kama vile hamna walichofanya.
STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, May 6, 2014
Uchaguzi Mkuu Simba Waiva, Hanspope ndiyo basi tena!
Zakaria Hanspope |
Kugonga mwamba kwa kipengele hicho kunamaanisha kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba wa kuteuliwa, Zacharia Hanspoppe, hataweza kuwania uongozi ndani ya klabu hiyo.
Kipengele hicho kinachoelezea sifa ya mgombea kwamba ni lazima asiwe mtu aliyewahi kufungwa/ kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, ndiyo kilimuondoa Hanspoppe aliyekuwa anawania uenyekiti katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 ambao ulimuweka madarakani Mwenyekiti, Ismail Aden Rage na wenzake.
Akizungumza jana jijini, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kwamba kipengele hicho hakikufika kwa msajili na kiliondolewa na Kamati ya Katiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa sababu inapingana na katiba ya shirikisho hilo linalosimamia mchezo huo nchini.
Kamwaga alisema kuwa kukamilika kwa katiba hiyo ni fursa kwa klabu yao kutangaza tarehe mpya ya kufanya uchaguzi utakaowaweka madarakani viongozi wapya.
Kamwaga alisema kuwa marekebisho mengine ambayo yalifanyiwa marekebisho na wanachama wa Simba yamepitishwa mojawapo ni kiongozi wa juu sasa atajulikana kwa jina la Rais badala ya Mwenyekiti na kutakuwa na Makamu wa Rais.
Alisema kuwa mabadiliko yaliyopitishwa ni pamoja na kuundwa kwa Kamati ya Rufaa, Kamati ya Maadili na pia ndani ya kata moja sasa inaruhusiwa kuwa na tawi zaidi ya moja lakini liwe na wanachama kuanzia 50 na wasiozidi 250.
Pia Kamwaga alisema kwamba kati ya wajumbe watano wa watakaochaguliwa, nafasi moja itakuwa ni kwa mjumbe mwanamke na hiyo wamelenga kuleta mawazo ya jinsi hiyo ndani ya uongozi.
"Kuundwa kwa kamati hizi kunaashiria kwamba matatizo yetu ndani ya Simba yanaweza kumalizwa na kamati hizi kabla ya kuvuka ngazi nyingine," alisema Kamwaga.
Alieleza kwamba kufuatia katiba hiyo kusajiliwa, Kamati ya Uchaguzi ambayo iko chini ya Mwenyekiti wake, Damas Ndumbaro, inatarajia kukutana leo jioni kwa ajili ya kupanga tarehe ya uchaguzi na mchakato mzima utakaohusisha zoezi hilo.
Tanki la mafuta lateketea na kuleta hopfu Singida
BAADHI ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B.
Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa
Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita
40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika
barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki
za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto.
Jambo
lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya
Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha
na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha
madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea.
Katika tukio hilo
lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari
kushindwa kupita katika eneo hilo kutokana na moto mkubwa
uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine.
Hata
hivyo baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama barabarani
waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea
na safari. Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio
hilo.
Angalia matukio zaidi ya picha hapo chini.
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
Liverpool yaduwazwa ugenini, ubingwa kwao ni majaliwa sasa!
Hekaheka uwanjani kati ya Crystal Palace na Liverpool jana |
Liverpool wakipongezana baada ya kufunga moja ya mabao yao matatu |
Suarez akioyesha makali yake kabla ya kufuga bao la tatu la Liverpool |
Liverpool waliokuwa ugenini walifanikiwa kuongoza zaidi ya nusu ya mchezo huo wakiwa mbele kwa mabao 3-0, lakini cha ajabu mabao yote yalikuja kurejeshwa na wenyeji na kufanya wagane pointi moja moja, ambazo zinawarejesha Liverpool kileleni lakini wakiweka rehani matumaini yao ya ubingwa msimu huu.
Wageni walianza kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Joe Allen katika dakika ya 18 kwa kumalizia kazi nzuri ya nahodha wake, Steven Gerrard na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Dakika nane baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Daniel Sturridge aliifungia Liverpool bao la pili kabla ya dakika mbili baadaye Suarez kufunga bao lake la 31 katika msimu huu na kuifanya timu yake iongoze kwa mabao 3-0.
Hata hjivyo wenyeji walicharuka na kurejesha mabao hayo kupitia kwa Delaney aliyefunga dakika ya 79 na Gayle aliyefunga mabao mawili katiika dakika ya 81 na 88 na kuiduwaza Liverpool ambao wamesaliwa na mchezo mmoja,huku wapinzani wao,Manchester City waliowaoindoa kileleni kwa sare hiyo ya jana wamesaliwa na mechi mbili wakiwa na pointi 80.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa pambano moja kati ya Manchestert United iliyotoka kupokea kipigo cha baoa 1-0 toka kwa Sunderland itakapoumana na Hull City.
Network Love ya Ruvu Stars videoni
Kiongozi wa Ruvu Stars, Khamis Amigolas |
Akizungumza na MICHARAZO mmoja wa viongozi wa bendi hiyo ya maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Rogart Hegga 'Katapila' alisema kuwa video hiyo itahusisha nyimbo zao za 'Network Love', 'Spirit' na 'Jua Kali' ambazo ndizo zilizolitambulisha kundi hilo kwa mashabiki wa muziki baada ya kusukwa upya likiwahusisha wanamuziki mahiri nchini.
Baadhi ya wanamuziki walionyakuliwa na kundi hilo ili kulisuka upya ni pamoja na Hegga, Khamis Kayumbu 'Amigolas', Khadija Mnoga 'Kimobitel', Jojo Jumanne, Victor Nkambi na rapa Msafiri Diouf.
Hegga alisema kazi hiyo ya kurekodi video hizo itaanza wiki hii na zoezi hilo litakapomalizika wataingia studio kumalizia nyimbo zao tatu za mwisho za kukamilisha albamu yao ya kwanza waliyopanga kuizindua baadaye mwaka huu.
"Tumesitisha zoezi la kumalizia nyimbo zetu tatu za kuhitimisha albamu ili kurekodi video za nyimbo za awali na kazi hiyo itafanywa katikati ya wiki chini ya kampuni moja ya jijini Dar es Salaam," alisema Hegga.
Alisema nyimbo za mwisho walizokuwa wameanza kurekodi ni 'Kioo' utunzi wake kiongozi mkuu wa bendi hiyo, Khamis Amigolas, 'Chewa Original' wa Seleman Muhumba na 'Facebook' wa Mkuu wa Jukwaa, Victor Nkambi ambaye pia ni 'mpapasa' kinanda mahiri nchini.
Matumla, Miyeyusho kuyeyushana Jumamosi PTA
Miyeyusho na Matumla wakiwa katika pozi. Wawili haowatapigana siku ya Jumamosi pale PTA |
Aidha, mabondia hao wanatarajiwa kupima uzito na afya zao siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni kabla ya kuvaana siku inayofuata kwenye ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao awali walipangwa kupigana Aprili 26, lakini likasogezwa mbele ili kupisha pigano la Miyeyusho dhidi ya Mthailand Sukkasem Kietyngyuth ambaye alimchapa Miyeyusho kwa TKO ya raundi ya kwanza.
Akizungumza na MICHARAZO, Rais wa TPBO-Limited inayosimamia pambano hilo, Yasin 'Ustaadh' Abdallah alisema pambano hilo lipo kama lilivyopangwa siku ya Mei 10.
Ustaadh alisema mabondia wote wapo kambini kujiandaa kwa ajili ya pambano hilo la kukata mzizi wa fitina baina yao baada ya kuwapo kwa tambo za muda mrefu. Miyeyusho amejichimbia mjini Bagamoyo na mpinzani wake yuko jijini Dar.
Rais huyo wa TPBO-Limited alisema maandalizi ya pambano hilo lililoandaliwa na promota Ally Mwazoa na litakalokuwa na michezo kadhaa ya utangulizi, yanaendelea vizuri.
Ustaadh alisema mapambano ya utangulizi siku hiyo yatakuwa kama ifuatavyo; Simon Zablon dhidi ya Keis Amary (kg 60), Mane Patrick dhidi ya Sadiq Abdul (kg 50), Kassim Gamboo dhidi ya Kassim Rajab (Kg55), Azizi Abdallah atapigana na Ide Mnali (kg 60) na mkongwe Rashid Ally dhidi ya Suma Ninja (kg 60).
Subscribe to:
Posts (Atom)