YANGA kweli wanaume! Ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia kwenye michuano ya kimataifa kwa mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Polisi Zanzibar kung'olewa mapema. Pia ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa, kadhalika ni moja ya klabu tatu pekee za ukanda wa CECAFA zilizopenya katika raundi ya pili ya michuano ya Afrika 2015.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwishoni mwa wiki kwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Yanga ni timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati kusalia katika Kombe la Shirikisho, lakini ikiungana na klabu za Al Merreikh na Al Hilal za Sudan zilizopenya raundi hiyo kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Yanga ilipata nafasi hiyo ya kuvuka hatua hiyo na kukabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Watunisia wa Etoile du Sahel baada ya kuing'oa FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2. Mwishoni mwa wiki walitandikwa bao 1-0, lakini ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mechi ya awali umewabeba.
Kwa mujibu wa 16 Bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu zilizopenya raundi ya pili katika Kombe la Shirikisho ni; Onze Créateurs ya Mali, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali, Hearts of Oak ya Ghana, ASO Chief ya Algeria, Club Africain ya Tunisia, Warri Wolves ya Nigeria MK Etancheite wa DR Congo, Zamalek ya Misri na FUS Rabat ya Morocco.
Nyingine ni CF Mounana ya Gabon, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Yanga ya Tanzania, Etoile du Sahel ya Tunia, Royal Leopards ya Swaziland na AS Vita ya DR Congo.
Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, zipo timu za USM Alger ya Algeria, AS Kaloum ya Guinea,
SM Sanga Balende ya DR Congo, Al-Hilal ya Sudan, Al-Merreikh ya Sudan, Espérance de Tunis ya Tunisia, MC El Eulma ya Algeria, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Léopards ya Congo na Smouha ya Misri.
Klabu nyingine ni Moghreb Tétouan ya Morocco, Al-Ahly ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco, watetezi ES Sétif ya Algeria, Stade Malien ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.
Mechi za awali ya hatua hizo zitachezwa kati ya Aprili 17-19 na marudiano kufanyika Mei 1-3 na timu ambazo zitapenya katika Kombe la Shirikisho zitaumana na zile zitakazoangushwa katika Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya kuwania kutinga hatua ya makundi kuanza safari ya kusaka mamilioni ya CAF.
STRIKA
USILIKOSE
Monday, April 6, 2015
Simba wanacheka, walipa kisasi kwa Kagera, Mtibwa hoi
Simba katika moja ya mechi zao za Ligi Kuu msimu huu |
WANAUMEEEE! |
Kagera Sugar katika mechi ya kiporo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Simba ambayo inaendelea kuomboleza vifo vya wanachama wake wa tawi la Maendeleo maarufu
kama Simba Ukawa waliofariki kwa ajali ya gari mjini Morogoro wakati wakielekea Shinyanga
kuwahi pambano hilo pamoja na kifo cha baba wa nahodha wao msaidizi, Jonas Mkude imepumua.
Ushindi huo wa mjini Shinyanga licha ya kusaidia kulipa kisasi kwa wapinzani wao, lakini pia
imewafanya wapunguze pengo la pointi dhidi ya mabingwa watetezi Azam wanashika nafasi ya
pili.
Simba imefikisha pointi 35, moja pungufu na ilizonazo Azam ambao keshokutwa watashuka dimba
la Taifa kuvaana na Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao ya washindi katika pambano hilo lililoahirishwa toka Jumamosi kutokana na uwanja wa
Kambarage kujaa maji ya mvua, yaliwekwa kimiani na Ramadhani Singano 'Messi' katika dakika ya
49 kwa shuti kali la mbali na panalti ya Ibrahim Ajibu katika dakika ya 65.
Penalti hiyo ilikuja baada ya mabeki wa Kagera kunawa mpira langoni mwao katika harakati za
kuokoa goli na Ajibu kufunga kiufundi. Kabla ya hapo Rashid Mandawa alifunga bao lake la 10
msimu huu na kumkamata Didier Kavumbagu pale aliposawazisha bao la Messi dakika ya 60.
Katika mechi ya kiporo kingine mapema leo asubuhi Mtibwa Sugar walishindwa kuhimili vishindo vya Stand United na kukubali kichapo cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha pili kwao mjini Shinyanga.
Awali wiki iliyopita walicharazwa mabao 2-1 na Kagera Sugar na kwa kichapo hicho wameifanya timu hiyo waliokuwa wakiongoza Ligi kwa muda mrefu kuporomoka hadi nafasi ya 12. Nafasi moja juu ya mstari wa timu mbili za kushuka daraja msimu huu kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Msimamo baada ya matokeo ya leo ni kama ufuatavyo;
P W D L F A Pts
1. Yanga 19 12 4 3 28 11 40
2. Azam FC 18 10 6 2 25 12 36
3. Simba 21 9 8 4 27 15 35
4. Kagera 21 7 7 7 19 20 28
5. Mgambo 20 8 3 9 17 19 27
6. Ruvu 19 6 8 5 13 16 26
7.Coastal 21 5 9 7 14 15 24
8. Mbeya City 20 5 9 6 15 17 24
9. JKT Ruvu 21 6 6 9 16 20 24
10. Ndanda 21 6 6 9 18 24 24
11. Stand 20 6 6 8 15 23 24
12. Mtibwa 21 5 8 7 19 20 23
13. Polisi Moro 21 4 9 8 13 21 21
14. Prisons 19 3 11 5 14 20 20
Mechi zijazo:
KESHO JUMATANO
Azam vs Mbeya City
Subscribe to:
Posts (Atom)