Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi na watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na tukio hilo, na kumtaja mwenzao John Tesha kwamba ndiye aliyekimbia na fedha hizo.
Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bernards Mashamba, Steven Thadeo, Adams Isudor, Johns Benja na Sultanis Kipensa huku juhudi za kumtafuta mwenzao aliyekimbia zikiendelea.
Alisema pesa hizo zilikuwa zimewekwa katika boksi kwa ajili ya kupelekwa benki ya BOA ghafla mfanyabiashara huyo akavamiwa na watuhumiwa hao waliokuwa na bunduki kubwa moja na bastola mbili wakitumia pikipiki mbili aina ya Boxer mojawapo ikiwa na namba za usajili T 311 CGE rangi nyekundu.
Kova alitaja maeneo waliyokamatiwa majambazi hao ni Chamanzi, Manzese, Keko, Kongowe Kizinga na Mtoni Mtongani.
Katika hatua nyingine, Kova alisema pikipiki 300 zimekamatwa kati ya hizo 201 ni aina ya Boxer ambazo zinasadikiwa kuwa kwa kiasi kikubwa zinatumiwa na majambazi.
Aliongeza kuwa wanaandaa utaratibu wa kuzipaka rangi pikipiki zote kama zilivyo teksi ili zijulikane wilaya zinakotoka na wamiliki wake.
Kamanda Kova alisema mpango huo utasaidia kudhibiti uhalifu na ajali zinazotokea mara kwa mara.