Aliyekuwa kocha wa Spurs, AVB alipokuwa wakiajibika kibaruani kabla ya kusitishiwa mkataba wake |
KLABU ya Tottenham Hotspur ya England imetangaza kumtimua aliyekuwa kocha wake mkuu, Andre Villa Boas kutokana na matokeo mabaya iliyopata timu hiyo jana kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyyo toka kwa Liverpool.
Timu hiyo ilikung'utwa mabao 5-0 na Liverpool ikiwa nyumbani na kukasirisha mabosi na mashabiki wa timu hiyo ambayo imekuwa ikifanywa asuswa kwenye ligi hiyo tofauti na usajili wa kishindo uliofanya msimu huu.
taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa wameafikiana na AVB kuachana naye na kwa sasa wanasaka kocha mkuu mpya wa kuinoa timu hiyo ambayo ilimnyakua Mreno huyo miezi 18 iliyopita baada ya kumtema Harry Redknapp aliyeipaisha barani Ulaya.
Miongoni mwa makocha wa awali wanaotajwa kumrithi AVB aliyeishuhudia vijana wake wakinyukwa mabao 6-0 wiki mbili zilizopita na Manchester City ugenini, ni bosi wa zamani wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello anayeinoa timu ya taifa ya Russia.
Pia wanatajwa Glenn Hoddle, kocha wa Swansea City Michael Laudrup na mtu anayetajwa haswa kuchukua nafasi hiyo ni Guus Hiddink.