Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa
Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bugando.
Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina enzi za uhai wake
---
MWENYEKITI
wa zamani wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza Clement Mabina,
ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza
ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.
Tukio
la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa
katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana
na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo
lilitokea jana katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa
wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya
saa mbili asubuhi.
ODC
Mkapa alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti
huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya
wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa
eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda
kupanda miti.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema
kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira
kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na
kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.
Taarifa
zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza
kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM alifika katika eneo hilo majira ya
asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama
ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina
yake na wananchi.
Baada
ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na
kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro
wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.
Baada
ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira
Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo
kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa
katika eneo hilo na kupoteza maisha.
Taarifa
hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio
hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha
mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha
kifo chake papo hapo.
Kabla
ya kurejea chama cha mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata
ya Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi
kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge
katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo
hilo, Malaki Lupondije.
No comments:
Post a Comment