Wachezaji wa Simba wakijifua asubuhi ya leo |
Mombeki |
Lazima tuwe fiti kwa mechi zijazo |
Chollo, Adeyum saleh na wenzao wakijifua |
Kwa tizi hizi Ruvu Shooting atoke salama Jumamosi...Mawe....! |
Fundi a.k.a Gaucho |
Ramadhani Singano 'Messi' naye alikuwepo |
Dua ni muhimu iwe kabla au baada ya mazoezi, vijana wa Simba wakiwa na benchi lao la ufundi likimshukuru Mungu kwa kumaliza salama mazoezi yao ya leo asubuhi |
Hata hivyo alisema anatumaini baada ya mechi nne zijazo atakuwa ameshafanikiwa kukipata kikosi hicho kwani alijiwekea lengo hilo ndani ya mechi 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara inayozidi kushika kasi.
Kwa maana ni kwamba Simba itaikabili Yanga Oktoba 20 ikiwa bado haijapata kikosi chake cha kwanza.
Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Kibadeni alisema bado hajafanikiwa kupata kikosi chake cha kwanza cha kukitegemea kwa vile anaendelea kuwaangalia nyota wake, ambapo alikiri wapo wanaomkuna kwa umahiri wao.
Kibadeni alisema kwa kuwa alijiwekea lengo la kukipata kikosi hicho katika mechi 10 anatarajia baada ya mechi nne kuanzia ile ya Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting, Prisons-Mbeya, Yanga na Coastal Union.
"Bado sijapata kikosi cha kwanza kwa sababu nilishatangaza tangu awali nitatumia mechi 10 kupata kikosi hicho na ndiyo kwanza tupo mechi ya sita, nadhani baada ya mechi nne zijazo ndipo nitakuwa na uhakika wa kikosi hicho, ila vijana wanajitahidi," alisema.
Kocha huyo mwenye rekodi nzuri nzuri kwa Simba na Tanzania kwa ujumla, aliizungumzia mechi yao ijayo dhidi ya Ruvu Shooting na kukiri itakuwa ngumu kama ilivyokuwa kwa JKT Ruvu kwa vile karibu timu zote za majeshi zinafanana, ila anashukuru baadhi ya nyota wake waliokuwa majeruhi wameanza kurejea uwanjani na kutumaini huenda akawatumia katika mchezo huo.
Wachezaji hao waliokuwa miongoni mwa majeruhi na jana walishiriki mazoezi ni kiungo Henry Joseph na beki wa pembeni Issa Rashid 'Baba Ubaya'.
"Nashukuru baadhi ya nyota wangu waliokuwa majeruhi wamerejea uwanjani na nina tumaini kuwatumia katika mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting, japo nitaendelea kuwakosa Miraji Adam na Abdallah Seseme bado wanaendelea kujiuguza," alisema.
Kuhusu ushindani katika Ligi Kuu ya msimu huu, Kibadeni alisema ni mkubwa na ndiyo maana hata kwenye msimamo timu zimepishana kwa idadi ndogo ya pointi kitu alichosema kinafanya ligi isisimue na kutabiri siyo rahisi bingwa kutangazwa mapema kama ilivyokuwa mwaka jana.
"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa na karibu timu zote zimejizatiti kunipa raha na hasa ikizingatiwa kuwa ligi ni ngumu na ina ushindani mkali kama ilivyokuwa msimu uliopita," alisema Kibadeni.