Picha tofauti zikionyesha Juventus wakipasha kwenye Uwanja wa Nou Camp kabla ya leo usiku uliamsha dude dhidi ya Barcelona |
KAZI imeanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati mechi za makundi kwa msimu huu wa 2017-2018 ukianza rasmi usiku wa leo kwa kushuhudiwa mechi nane, lakini macho na masikio yakielekezwa Nou Camp, wakati Kibibi Kizee cha Turin, Juventus itakapoifuata Barcelona katika mechi iliyovuta mashabiki wengi wa michuano hiyo.
Juventus imeenda Hispania ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa fainali zilizopita dhidi ya mahasimu wa Barcelona, Real Madrid, lakini wakijivunia rekodi ya kuanza Ligi Kuu ya Italia Serie A ikishinda mechi zao tatu zote na kufunga mabao 10 na kukaa kileleni ikizizidi ujanja Napoli na Inter Milan kwa tofauti na uwiano wa mabao.
Kikosi hicho cha Juve kilifanya mazoezi jana kwenye Uwanja wa Nou Camp kikiwa na nyota wake wote wakiwamo wakali kinara wa mabao Paul Dyabala, Gonzalo Higuain na Mario Mandzukic.
Wenyeji wataendelea kumtegemea zaidi nyota wao Lionel Messi na Luis Suarez kuweza kulinda heshima yao katika michuano hiyo baada ya msimu uliopita kukwamia njiani kwa aibu.
Mbali na mechi hiyo, pia leo kuna gemu kali yenye mvuto Manchester United waliorejea kwenye michuano hiyo kwa mlango wa uwani itakuwa nyumbani kukabiliana na Basel, huku Chelsea wakicheza na Qarabag, PSG ikiwa na wachezaji ngali zaidi kwa sasa duniani Neymar na Kylian Mbappe watakuwa ugenini nchini Scotland kuvaana na Celtic.
RATIBA KAMILI LIGI YA MABINGWA ULAYA
Leo, Jumanne
Celtic v PSG (Saa 3:45 usiku)
Benfica v CSKA Moskva (Saa 3:45 usiku)
Man United v Basel (Saa 3:45 usiku)
Olympiakos v Sporting CP (Saa 3:45 usiku)
Bayern Munichv Anderlecht (Saa 3:45 usiku)
Roma v At.Madrid (Saa 3:45 usiku)
Chelsea v Qarabag (Saa 3:45 usiku)
Barcelona v Juventus (Saa 3:45 usiku)
Kesho Jumatano
Maribor v Spartak Moskva (Saa 3:45 usiku)
Tottenham v B.Dortmund (Saa 3:45 usiku)
RB Leipzig v Monaco (Saa 3:45 usiku)
Feyenoord v Man City (Saa 3:45 usiku)
Shakhtar v Napoli (Saa 3:45 usiku)
Liverpool v Sevilla (Saa 3:45 usiku)
Porto v Besiktas (Saa 3:45 usiku)
Real Madrid v APOEL (Saa 3:45 usiku)
EUROPA LEAGUE
Alhamis, Septemba 14, 2017
Young Boys v Partizan (Saa 2:00 usiku)
Atalanta v Everton (Saa 2:00 usiku)
Slavia Praha v Maccabi Tel Aviv(Saa 2:00 usiku)
Dynamo Kyiv v Skënderbeu Korçë(Saa 2:00 usiku)0
Hoffenheim v Sporting Braga (Saa 2:00 usiku)
Apollon v Lyon (Saa 2:00 usiku)
Zlín v Sheriff (Saa 2:00 usiku)
Rijeka v AEK Athens (Saa 2:00 usiku)
Istanbul Basaksehir v Ludogorets (Saa 2:00 usiku)
København v L'tiv Moskva (Saa 2:00 usiku)
Austria Wien v Milan (Saa 2:00 usiku)
Villarreal v Astana (Saa 2:00 usiku)
Hapoel B.Sheva v Lugano (Saa 4:05 usiku)
Zorya v Östersunds FK (Saa 4:05 usiku)
Real Sociedad v Rosenborg (Saa 4:05 usiku)
Vitesse v Lazio (Saa 4:05 usiku)
Zulte-Waregemv Nice (Saa 4:05 usiku)
Arsenal v Koöln (Saa 4:05 usiku)
Marseille v Konyaspor (Saa 4:05 usiku)
Vitoria Guimarães v Salzburg (Saa 4:05 usiku)
Crvena Zvezda v BATE (Saa 4:05 usiku)
Hertha BSC v At.Bilbao (Saa 4:05 usiku)
Vardar v Zenit (Saa 4:05 usiku)
FCSB v Viktoria Plzen (Saa 4:05 usiku)