STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 16, 2015

Polisi Zanzibar, KMKM yaendeleza uteja Afrika

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi59R0MYcrxWHLeSNnC_vM50rvpo6pW4S079-xz073BM1qMzHu78BZ3M2A6-Rcffg0AKuCNlGJTx77XuEspNUQTYpSZxeIwClivBXmTswWbLyuGBKDZoXuu3mnXKpUwrCIZ62qjbxpxVhkw/s640/4.jpg
KMKM waliokufa 2-0 Sudan
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLCWb5BqldkVTcFvaO8san-9Nhbw4RdsAVAbuN1u3556K_TvVv67OvOYjoXCPZ7VpusnafOOpJiS6SLaDK-7wNEixcgcnDUbt54qaR2jof0UEU-xKJdBd0IUmCqdrNsyokdr0MSy0kmIY/s1600/IMG_3886.JPG
Polisi waliopigwa 'mkono' nchini Gabon
WAKATI wawakilishi wa Tanzania Bara, Azam na Yanga wakiwapa raha mashabiki wao, KMKM na Polisi Zanzibar zimeendelea kuwasononesha mashabiki wa soka wa visiwa hivyo baada ya kugeuzwa 'urojo' katika mechi zao za kimataifa zilizochezwa mwishoni mwa wiki.
Polisi wanaoiwakilisha Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kama Yanga, ilikutana na kipigo cha mabao 5-0 toka kwa Moumana ya Gabon wakati mabingwa wa visiwani, KMKM wakilala 2-0 nchini Sudan kwa Al Hilal na kujiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Tangu Zanzibar ilipopata uanachama wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, 2004, imekuwa ikifanya vibaya kwenye uwakilishi wa klabu kwa timu zao kuondolewa hatua za awali.
KMKM na Polisi maarufu kama Wazee wa Tunisia' watakuwa na mtihani mgumu swa na kupanda mlima mrefu kuweza kuzitoa Mounana na Al Hilal katika mechi zao za marudiano wakati wakiwa nyumbani.
Hiyo ni tofauti na wawakilishi wa Tanzania Bara, Yanga na Azam wenye kazi nyepesi kwenye mechi zao za marudiano wiki mbili zijazo ugenini dhidi ya timu za BDF XI ya Botswana na El Merreikh ya Sudan.
Yanga ilianza kwa kuizabua BDF kwa mabao 2-0 juzi kwenye Kombe la Shirikisho, kabla ya Azam kufuata mkumbo huo kwa kuilaza El Merreikh kwa idadi kama hiyo jana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo mengine ya michuano ya hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika yapo hivi;
Al Ahli Tripoli     1 - 0     Smouha
COB     2 - 0     Moghreb Tétouan        
Raja Casablanca     4 - 0     Diables Noirs
St Michel United     1 - 1     Mamelodi Sundowns       
KCCA     1 - 0     Cosmos de Bafia        
Gor Mahia     1 - 0     CNaPS Sport        
Al-Malakia     0 - 2     Kano Pillars  
Recreativo do Libolo  3 - 1     Sanga Balende      

Mangasport     1 - 0     Bantu         
LLB Académic     0 - 0     Kabuscorp        
Séwé Sport     1 - 2     Kaloum Star
Real de Banjul     1 - 1     BYC
Pikine     1 - 0     Etoile Filante
MC El Eulma     1 - 0     Kedus Giorgis
Kaizer Chiefs     2 - 1     Township Rollers
Fomboni Club     0 - 1     Big Bullets
Azam     2 - 0     Al Merreikh 
Enyimba     3 - 0     Buffles de Borgou
Liga Muçulmana     0 - 0     APR
Mbabane Swallows     1 - 1     ZESCO United
USM Alger     3 - 0     Foullah Edifice
Al Hilal Omdurman     2 - 0     KMKM
Matokeo ya Kombe la Shirikisho Afrika;
Al-Ghazal     0 - 1     Petrojet
URA     3 - 2     Elgeco Plus
Benfica Luanda     2 - 0     Le Messager Ngozi
RSB Berkane     2 - 1     Onze Créateurs
Petite Rivièr…     1 - 2     Ferroviário Beira
Côte d'Or     2 - 3     Dedebit
RC Bobo-Dioulasso     0 - 1     Warri Wolves
Volcan Club     0 - 1     Petro de Luanda
Young Africans     2 - 0     BDF XI
Panthère     0 - 1     Rayon Sports
MC Alger     0 - 0     Sahel 
Leones Vegetar…     1 - 0     Dolphins
Étoile du Congo     1 - 2     FC MK
BV Wits     3 - 0     Royal Leopards
Khartoum 3     1 - 0     Power Dynamos
Sofapaka     1 - 2     Platinum
Al-Ittihad     6 - 1     Elect-Sport
Unisport Bafang     1 - 0     Olympique Ngor
Mounana     5 - 0     Polisi
Hearts of Oak     1 - 0     Police
Togo Port     2 - 0     CARA Brazzaville
ASO Chlef     2 - 0     Kamboi Eagles
Horoya     1 - 0     Fassell

Sikiliza ngoma mpya ya Shaa iitwayo For You


KOCHA JULIO AWAUMBUA WALIOMBEZA

Kocha jamhuri Kihwelu 'Julio'
KOCHA Jamhuri Kihwelu 'Julio' ni maarufu kwa kuwa mzungumzaji na mtu mwenye tambo nyingi zinazokera, lakini kwa kitendo alichofanya cha kuipandisha Ligi Kuu timu ya Mwadui Shinyanga mwaka mmoja baada ya kubaniwa na TFF ni kama amewaumbua wabaya wake.
Waliombeza na kumtimua ndani ya Simba katikati ya msimu uliopita wakati Simba ikiwa nafasi ya nne pamoja na bosi wake Abdallah Kibadeni 'King' huenda sasa wakatafuta mahali pa kuficha sura zao kwa aibu baada ya Julio kufanya kweli kwa kuirejesha Mwadui Ligi Kuu baada ya miaka zaidi ya 30 tangu ishuke daraja.
Msimu uliopita mara baada ya kutemwa na Simba, Julio alipewa mikoba ya kuinoa timu hiyo na kumaliza vinara wa kundi lao na kuonekana kama wamepanda daraja kabla ya TFF kuwaengua kutokana na rufaa ya JKT Kanembwa kuwaacha nafasi ya tatu nma ya pili ikitwaliwa na Stand United kama utani.
Kocha huyo aliyewahi kutamba na klabu mbalimbali ikiwamo Pilsner na Simba na timu ya taifa, akiwa mmoja wa mabeki mahiri wa kati, hakukata tamaa na badala yake alisuka kikosi chake na kuwezesha kupata msimu huu baada ya kumaliza kinara wa kundi lao wakifuatiwa na Toto Africans ambao nao wanarejea ligi chinio ya kocha John Tegete.
Akihojiwa mara baada ya kupata ushindi wa mabao 4-3, Julio alituma salamu zake kwa vigogo vya Ligi Kuu kuwa wajiandae kupata upinzani mkali msimu wa 2015-2016 kwani Mwadui haitacheza chini ya Nafasi ya Tatu Bora.
"Wajiandae tunakuja, tunajipanga kuhakikisha tunakuwa miongoni mwa timu Tatu Bora," alisema Julio hata ikiwa ligi yenyewe bado haijaanza.
Julio mmoja wa makocha wenye elimu ya juu ya ukocha na ambaye amekuwa akipata mafanikio licha ya utamaduni wa kupuuzwa kwa makocha wazalendo wanaotumiwa kama 'spea tairi' ameuthibitishia umma kwamba makocha Wazalendo wanaweza.
Mbali na kutwaa mataji kama mchezaji wa Simba, Julio pia ameshatwaa ubingwa wa Kombe la taifa kama kocha wa timu ya soka ya Ilala iliyoundwa na nyota wa Simba na Yanga kama ambavyo kikosi chake cha Mwadui kilivyoundwa na wakali wa timu hizo ambao walipigana na kuibeba kurudi Ligi Kuu msimu ujao.
MICHARAZO inampongeza Julio na timu yake sambamba na kuzipongeza timu zote nne za Majimaji Songea, Africans Sports na Totyo Africans kwa kurejea tena ligi kuu baada ya muda mrefu kuwa nje ya lifgi hiyo kubwa nchini.
Jambo la muhimu jipangeni mapema sasa ili msije mkainusa na kurejea tena ligi daraja la kwanza kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa kwa baadhi ya timu zinazopanda ligi hiyo na kudumu kwa msimu mmoja.

Yamoto Band kwenda kutumbuiza kwa Malkia Elizabeth II

Kundi la Yamoto Band
Bango la onyesho hilo la Yamoto kwa Malkia
KUNDI linalofanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Yamoto Band, linatarajiwa kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kutumbuiza.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Said Fella, alisema Yamoto itaondoka nchini kesho kwa ajili ya kufanya onyesho lao siku ya Jumamosi.
Fella alisema onyesho lao litafanyika kwenye ukumbi wa Royal Regency, jijini London ikiwa ni mara ya kwanza kwa Yamoto kutua kwenye nchi hiyo ya Malkia.
Fella alisema ziara yao imeandaliwa na baadhi ya Watanzania wanaoishi Uingereza na taarifa walizonazo watafanya onyesho Februari 21 na kama kutakuwa na onyesho jingine la ziada watafahamu huko huko.
"Bendi itaondoka Febaruari 17 na onyesho litafanyika Februari 21 mjini London kwenye ukumbi wa Royal Regency," alisema Fella.
Kundi la Yamoto linaundwa na wasanii wanne wakali ambao ni Aslay, Maromboso, Enock Bella na Beka na limekuwa likitamba na nyimbo mbalimbali zikiwamo 'Yamoto', 'Nitajuta', 'Niseme', 'Tulia' na sasa wanatingisha na 'Nitakupwelepweta'

Shamsa Ford 'awauma' sikio wenzie, msikie...!

Kimwana Shamsa Ford
SHAMSA Ford ambaye ameufungua mwaka kwa kuuza sura ndani ya filamu ya 'Kudra' amewataka wasanii wenzake wa kike kujipanga mwaka 2015 ili kuhakikisha wanafika mbali kimataifa.
Shamsa anayejiandaa kupakua filamu yake mpya ya 'Mama Muuza' alisema kuwa mwaka 2015 uwe mwaka wa mipango kwa wasanii wa filamu nchini hasa wa kike kwa kuhakikisha wanakuwa namba moja badala ya kuridhika na nafasi walizonazo.
Mwanadada huyo alisema kwa upande wake amejipanga kuhakikisha anafanya kila jitihada ili kung'ara ikiwamo kunyakua tuzo kwa vile uwezo na sababu ya kufanya hivyo anayo.
"Ningependa kuwakumbusha wasanii wenzangu wa kike kuamka na kuufanya mwaka 2015 uwe wa mwaka wa mafanikio kwao, tujipange tuweze kuona tunatamba kimataifa," alisema.
Shamsa aliyekimbiza mwaka jana kupitia filamu kadhaa ikiwamo 'Hukumu ya Ndoa Yangu' na ile yake ya 'Chausiku', alisema imefika wakati wasanii nchini waelekeze nguvu zao kwenye soko la kimataifa badala na kuridhika na mafanikio ya nyumbani

Sikiliza ngoma mpya ya Diamond f P Square

Diamond