Kocha jamhuri Kihwelu 'Julio' |
Waliombeza na kumtimua ndani ya Simba katikati ya msimu uliopita wakati Simba ikiwa nafasi ya nne pamoja na bosi wake Abdallah Kibadeni 'King' huenda sasa wakatafuta mahali pa kuficha sura zao kwa aibu baada ya Julio kufanya kweli kwa kuirejesha Mwadui Ligi Kuu baada ya miaka zaidi ya 30 tangu ishuke daraja.
Msimu uliopita mara baada ya kutemwa na Simba, Julio alipewa mikoba ya kuinoa timu hiyo na kumaliza vinara wa kundi lao na kuonekana kama wamepanda daraja kabla ya TFF kuwaengua kutokana na rufaa ya JKT Kanembwa kuwaacha nafasi ya tatu nma ya pili ikitwaliwa na Stand United kama utani.
Kocha huyo aliyewahi kutamba na klabu mbalimbali ikiwamo Pilsner na Simba na timu ya taifa, akiwa mmoja wa mabeki mahiri wa kati, hakukata tamaa na badala yake alisuka kikosi chake na kuwezesha kupata msimu huu baada ya kumaliza kinara wa kundi lao wakifuatiwa na Toto Africans ambao nao wanarejea ligi chinio ya kocha John Tegete.
Akihojiwa mara baada ya kupata ushindi wa mabao 4-3, Julio alituma salamu zake kwa vigogo vya Ligi Kuu kuwa wajiandae kupata upinzani mkali msimu wa 2015-2016 kwani Mwadui haitacheza chini ya Nafasi ya Tatu Bora.
"Wajiandae tunakuja, tunajipanga kuhakikisha tunakuwa miongoni mwa timu Tatu Bora," alisema Julio hata ikiwa ligi yenyewe bado haijaanza.
Julio mmoja wa makocha wenye elimu ya juu ya ukocha na ambaye amekuwa akipata mafanikio licha ya utamaduni wa kupuuzwa kwa makocha wazalendo wanaotumiwa kama 'spea tairi' ameuthibitishia umma kwamba makocha Wazalendo wanaweza.
Mbali na kutwaa mataji kama mchezaji wa Simba, Julio pia ameshatwaa ubingwa wa Kombe la taifa kama kocha wa timu ya soka ya Ilala iliyoundwa na nyota wa Simba na Yanga kama ambavyo kikosi chake cha Mwadui kilivyoundwa na wakali wa timu hizo ambao walipigana na kuibeba kurudi Ligi Kuu msimu ujao.
MICHARAZO inampongeza Julio na timu yake sambamba na kuzipongeza timu zote nne za Majimaji Songea, Africans Sports na Totyo Africans kwa kurejea tena ligi kuu baada ya muda mrefu kuwa nje ya lifgi hiyo kubwa nchini.
Jambo la muhimu jipangeni mapema sasa ili msije mkainusa na kurejea tena ligi daraja la kwanza kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa kwa baadhi ya timu zinazopanda ligi hiyo na kudumu kwa msimu mmoja.
No comments:
Post a Comment