Di Maria akishangilia bao lake |
Furaha ya ushindi Manchester wakifurahia baada ya kuypata moja ya mabao yao |
Mata akishangilia bao lake |
Di Maria aliwainua mashabiki wa Old Trafford kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kabla ya Herrera kupachika la pili katika dakika ya 36 akimalizia kazi ya nahodha Wayne Rooney.
Dakika moja kabla ya mapumziko, nahodha huyo Rooney alifunga bao la tatu akimalizia kazi murua ya Herrera na bao la mwisho la vijana wa Luis Van Gaal lilifungwa na Juan Mata katika dakika ya 58 kwa kazi safi ya Di Maria aliyeonyesha ubora wake na kuifanya Mashetani Wekundu kupumua baada ya kuanza vibaya ligi na msimu mzima kwa ujumla.
Radamel Falcao aliingia uwanjani katika kipindi cha pili na kuonyesha makeke yake ikiwa ni mara ya kwanza tangu asajiliwe kutoka Monaco.