Kipa Valdes akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Manchester United |
Daley Blind akifanya mazoezi hapa akiwa na Dogo Andreas Pereira
Rojo naye alipasha na wenzake |
Mashetani Wekundu wanatarajiwa kuwa nyumbani kuwavaa Southampton baada ya kupata sare mbili mfululizo ugenini katika Ligi Kuu ya England, lakini ikiwa na furaha kurejea kwa nyota hao sambamba na kumnasa kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes waliyemsainisha.
Kama ilivyo kwa Manchester, Arsenal wenyewe wanafurahi baada ya Ozil kurejea Ligi Kuu
England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.
Kocha Arsene Wenger amesema
Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo
inaonekana ataanzia benchi.
Mjerumani huyo aliyejiunga
na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka
jana.
Ozil ndiye mchezaji ghali
zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.