BAADA ya kupakaziwa kuwa ni majeruhi wa goti, Kiungo wa Juventus, Arturo Vidal amejibu mapigo juu ya taarifa hiyo ya kupata majeraha akiwa katika majukumu ya kimataifa na Chile.
Ripoti zilieleza kuwa Vidal, ambaye alihusishwa kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu, aliondoka mazoezini mjini Miami baada ya kuumia goti kwa mara nyingine.
Hata hivyo, Vidal kupitia akaunti yake ya Twitter amekanusha taarifa hizi akisema alikuwepo muda wote katika mazoezi ya timu hiyo.
“Goti langu liko sawa,” Vidal aliandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii. “Tafadhali acheni kuzusha taarifa. Njooni Chile”.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita na alionekana kutokuwa fiti sana katika fainali za kombe la dunia.
Majeruhi imemuathiri Vidal katika haraka zake za kujijenga kuwa miongoni mwa viungo bora wa dunia.
STRIKA
USILIKOSE
Saturday, September 6, 2014
Coastal Union kutambulisha wapya Coastal Day
KLABU ya Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa kutambulisha wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi
kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaotazamiwa kuanza Septemba 20 mwaka huu.
Utambulisho huo utafanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga katika siku maalum ya Coastal 'Coastal Union Day' ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7.
Utambulisho huo utafanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga katika siku maalum ya Coastal 'Coastal Union Day' ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7.
Katika utambulisho huo Coastal maarufu kama Wagosi wa Kaya wataumana na timu iliyorejea Ligi Kuu Polisi Morogoro.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa.
Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa.
Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya mazungumzo kumalizika.
"Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara"
Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu, Assenga amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
Balotelli alizua Liverpool mechi ya kirafiki
MSHAMBULIAJI
wa Liverpool, Mario Balotelli alitolewa nje katika mchezo wa kirafiki
ambao mashabiki hawakuhudhuria dhidi ya Wolves baada ya kuanza kuzozana
na refa Chris Foy.
Balotelli, 24, aliyehamia Anfield kutoka AC Milan kwa
Pauni Milioni 16 mwezi uliopita, alizuiwa na Kolo Toure wakati Foy
akizungumza naye kwenye mchezo huo Melwood.
Chanzo cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo kugongana na mchezaji wa Wolves. Baada ya mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
Toure
aliweka bega lake kumdhibiti mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa
Manchester City asiendelee kuzozana na Foy juu ya tukio hilo kabla ya
Balotelli kutolewa aingie mchezaji mwingine.
Nyota
huyo wa zamani wa Inter Milan alianza pamoja na wachezaji kama Adam
Lallana, Jose Enrique na Lucas Liverpool ikishinda 1-0 dhidi ya timu ya
Daraja la Kwanza, bao pekee la Lallana.
Balotelli alichukua mpira kwenye himaya ya kipa wa Wolves katika mchezo huo
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City aliisumbua mno ngome ya Wolves katika mchezo huo
Yanga kuwavaa Wamalawi, Simba kupimana na Gor Mahia leo
Yanga |
Simba |
WAKATI watani zao wa jadi wakishuka dimbani leo kuvaana na Gor Mahia ya Kenya, timu ya Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani kesho kuwavaa Wamalawi wa timu ya Big Bullets (zamani Bata Bullets).
Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zikiwa ni za kirafiki za kimataifa kujiandaa na Ligi Kuu itakayoanza wiki mbili zijazo.
Yanga itashuka dimbani kesho ikiwa ni siku chache baada ya kutoka kuwagonga, Thika United bao 1-0 katika mechi nyingine ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo itachezwa kuanzai saa 10 jioni na viingilio vyake vitakuwa kama ifuatavyo:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
Wakati huo huo Simba itashuka dimbani leo kuvaana na Gor Mahia katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Taifa, na Wakenya hao tayari wameshatua Bongo tangu jana tayari kwa mechi hiyo.
Hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya kocha Patrick Phiri kwenye uwanja wa Taifa akitoka kumrithi Zdravkov Logarusic aliyetimuliwa siku moja baada ya kipigo cha mabao 3-0 toka kwa ZESCO siku ya Simba Day.
Simba waliokuwa wameweka kambi ya mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu visiwani Zanzibar imeshatua jijini Dar es Salaam tayari kuwavaa Wakenya hao na kuwaonyesha mashabiki wao baadhi ya vifaa vipya vilivyosajiliwa wakti timu ikiwa kambini.
Simanzi! Ajali yachinja 39, wengine 75 hoi
AJALI ya kutisha iliyohusisha magari matatu yakiwamo mabasi mawili ya abiria na gari ndogo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 39 huku wengine zaidi ya 70 wakiwa majeruhi.
Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaligongana uso kwa uso na kuumia vijana katika eneo la Sabasaba, Musoma mjini na kusababisha simanzi katika eneo la tukio kutokana na miili ya abiria na madereva pamoja na makondakta wa magari hayo kukatikakatika vibaya.
Mabasi hayo moja lenye nambaza usajili T 677 CYC lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Sirari, Mara na Mwanza Coach lenye nambari za usajili T 736 AWJ yaligongana uso kwa uso. Kwa mujibu taarifa toka eneo la tukio na kuthibitisha na Polisi Mkoa wa Mara, zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo
lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja
linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo, kutokana na kuwa basi hilo
lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo
ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia
na kwenda kuingia mtoni.
Hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa
itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine
linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi
kupita kwenye daraja hilo.
Basi
la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4
EXPRESS.
Umati
wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya
na kusababisha watu 39 kupoteza maisha pamoja hapo wakishuhudia tukio
hilo la ajali.
Buldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia
mtoni. Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na
mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)