|
Nicklas Bendtner akifunga bao la kwanza la Arsenal |
|
Torres alipoondoa 'gundu' kwa kuifungia Chelsea bao la kwanza |
|
Liverpool ilipoisulubu Hully City uwanja wa Anfield |
|
West Bromwich walipoilaza Newcastle United kwa bao la mkwaju wa penati |
MABAO ya dakika za lala salama wameiwezesha Arsenal kurejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England, huku Chelsea ikiendelea kuonyesha makali yake kwa kupata ushindi ugenini dhidi ya Southampton.
Aidha Liverpool nayo imerejesha makali yake baada ya kusimamishwa hivi karibu kwa kupokea vipigo viwili mfululizo baada ya kushinda nyumba mabao 2-0, Luis Suarez akifunga bao lake la 20 katika ligi ya msimu huu.
Nicklas Bendtner aliifungia Arsenal bao dakika ya 88' na Tim Walcott kuongeza bao la pili dakika za nyongeza za mchezo huo kumalizia kazi ya Jack Walshere iliifanya Arsenal ipumue kwa kuilaza Cardiff City na kurejea tena kileleni ilipokuwa imeshushwa na Manchester City iliyoshinda ugenini jioni hii.
Arsenal imefikisha pointi 45 moja zaidi ya City na kurejesha msimamo wa awali uliokuwapo baada ya timu zote za Top 4 kushinda jioni hii, Chelsea ikiinyoa Southampton mabao 3-0 huku Liverpool ikiwa nyumbani ikiitambia Hull City mabao 2-0.
Katika mechi ya Chelsea mabao yao yalifungwa na Fernando Torres dakika ya 60 kabla ya William kuongea la pili dakika ya 71 akimalizia kazi ya Oscar.
Oscar aliihakikisha Chelsea inayonolewa na Jose Mourinho ushindi kwa kufunga bao la tatu dakika nane kabla ya kumalizika kwa mchezo huo akimalizia kazi ya Eden Hazard.
Liverpool ilipata ushindi wake nyumbani kupitia kwa Daniel Agger dakika ya 36 na Luis Suarez akafunga bao lake la 20 katika dakika ya 50 na kuipa 'vijogoo' hao wa Anfield ushindi muhimu katika mbio zake za kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Manchester United.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizomalizika hivi punde, Crystal Palace ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Norwich City, Fulham iliinyoa West Ham United kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani na Stoke City iliing'ang'ania Everton na kutoka sare ya 1-1.
Nayo West Bromwich baada ya kufanywa asusa kwa muda mrefu imejitutumua nyumbani kwa kuilaza Newcastle United kwa bao 1-0.
Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha Arsenal wapo kileleni ikiwa na pointi 45 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 44, kisha Chelsea ikifuatia ikiwa na pointi zake 43 na Livewrpool kurejea kwenye Top 4 kwa kufikisha pointi 39 na Everton ikikamilisha Tano Bora na pointi zake 38.
Pambano la mwisho la ligi hiyo itazikutanisha Manchester United itakayokuwa nyumbani dhidi ya Tottenham ambapo hata zikifungana haziwezi kubadili msimamo wa juu kwani zote zina pointi 34.