STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 29, 2013

PICHA ZA TUKIUO LA KUPOROMOKA KWA JENGO KATIKATI YA JIJI



 Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira Gandhi.

 Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
 Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.
 Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.


 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Waokoaji wakiwa kazini.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.
 
PICHA ZIMEHAMISHWA HABARI MSETO

Maiti zaidi zapatikana ajali ya ghorofa lililoporomoka Dar


Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka asubuhi hii katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 29, 2013.
MIILI zaidi imedaiwa kupatikana katika tukio la ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa linalodaiwa kuwa 19 lililokuwa likiendelea kujengwa kuporomoka na kuwafunika watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 6o

Tukio hilo limetokea mishale ya asubuhi katika mitaa ya Posta, jirani na msikiti wa Shia katika eneo la makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi na hadi sasa, miili ya maiti 12 na pia majeruhi 30 wameshachomolewa.

Aidha, harakati zaidi za uokoaji zingali zikiendelea kufanywa na vikosi vya uokoaji. Katika eneo la tukio hilo, tayari viongozi kadhaa wa serikali na makamanda wa Polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam wamefika kusaidia shughuli za uokoaji, miongoni mwao akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa mabaki ya jengo hilo yanaonyesha kuwa mchanga ulikuwa mwingi mno kulinganisha na saruji, hali inayodhaniwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa mjengo huo uliogharimu mamilioni ya pesa.

Pamoja na mashuhuda wa tukio hilo kudai kuna zaidi ya miili ya watu 10 iliyotolewa kwenye uokozi na wengine 30 kukimbizwa hospitalini kwa matibabu kutokana na kujeruhiwa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema ni watu wawili tu waliogundulika kufa mpaka sasa na waliokimbizwa hospitali ni 17 japo shughuli za uokozi zinaendelea.

BREAKING NEWSSSS: GHOROFA LAPOROMOKA DAR 60 wadaiwa kufukiwa


HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema jengo la ghorofa lililokuwa likiendelea kujengwa mitaa ya Indra Gandi jijini Dar es Salaam limeporomoka na kuwafukia watu wasiopungua 60.
MICHARAZO imedokezwa kuwa mpaka sasa watu 17 wameshaokolewa na miili ya watu wawili imepatikana katika mkasa huo unaohusisha ghorofa hilo la orofa 19.
Mtandao unaendelea kuzifuatilia taarifa hizo kisha tutawajulisha kinachoendelea, japo inaeleza juhudi za uokozi katika tukio hilo zinaendelea kunusu watu waliozikwa na kifusi cha jengo hilo.
Pia imeelezwa kuwa viongozi wa mkoa akiwemo Rc Mecky Sadick ametua katika eneo hilo akiambatana na wenzake kwa ajili ya kujua kinachoendelea. 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova amethibitisha kuokolewa kwa watu 17 na wawili kupoteza maisha na kusema taarifa kamili itatolewa baadaye.

UCHAGUZI MIKUU BFT KUFANYIKA JIJINI MWANZA

Viongozi wa sasa BFT, Rasi Joan Minja (kulia) na Katibu Mkuu, Mashaga makore

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BFT, Mashaga Makore, aliiambia MICHARAZO asubuhi ya leo kuwa, kuwa uchaguzi huo utafanyika mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kimataifa ya Majiji yanayotarajiwa kufanyika jijini humo kati ya Mei 20-25.
Makore alisema mchakato wa kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho kitatanguliwa na Mkutano Mkuu wa shirikishi hilo utatangazwa mara baada ya shamrashamra za sikukuu ya Pasaka.
"Uchaguzi Mkuu wa BFT utafanyika mwezi Mei jijini Mwanza mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kimataifa ya ngumi inayoshiriki miji mikuu ya Afrika Mashariki na Kati, ambapo utatanguliwa na Mkutano Mkuu," alisema Makore.
Makore alisema maamuzi hayo yalifikiwa na Kamati yao ya Utendaji iliyokaa hivi karibuni na kutoa wito kwa wadau wa mchezo huo wenye uwezo na sifa za kuongoza shirikisho hilo kujiandaa kuijitosa kuwania uongozi kwenye uchaguzi huo.

Goti lamtia hofu Zahoro Pazi


MSHAMBULIAJI wa timu ya JKT Ruvu, Zahoro Pazi ameingiwa hofu na jeraha la goti alilopata wakati wa pambano lao dhidi ya Polisi Morogoro huenda ikamvurugia mipango ya safari yake ya kurejea Afrika Kusini kujaribu kuchezas soka la kulipwa.
Pazi ametakiwa kurejea tena nchini humo Mei mwaka huu kulingana na makubaliano yake na klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini Bloemfotein Celtic, iliyomfanyia majaribio ya kuichezea yaliyofanyika Januari mwaka huu.

Hata hivyo mchezaji huyo alisema ameanza kupatwa hofu baada ya kupata maumivu makali alipoumia kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Moro, pambano lililoisha kwa JKT Ruvu kushinda mabao 3-2.
Akizungumza na MICHARAZO, Pazi alisema pamoja na uvimbe uliokuwapo katika goti hilo kuisha bado anahisi maumivu makali kwa ndani japo linalomnyima raha, ingawa alisema benchi la utabibu la klabu yake linamshughulikia vyema.
"Haya maumivu ya goti niliyonayo yananikatisha tamaa, nashindwa kuitumikia klabu yangu na wakati huo huo nina mwezi mmoja tu wa kujiandaa kabla ya kurejea Afrika Kusini kuendelea na majaribio yangu klabu ya Bloemfotein Celtic," alisema Pazi.
Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Idd Pazi 'Father' anayeichezea JKT kwa mkopo akitokea Azam, alisema anatamani apone haraka goti hilo ili ajifue zaidi kusudi akienda Afrika Kusini awaridhishe mabosi wa Bloemfotein.

Humud apaa zake kwenda Jomo Cosmo



KIUNGO mahiri wa timu ya Azam, Abdulhalim Humud 'Gaucho' ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika kalbu ya Jomo Cosmo.
Meneja wa klabu ya Azam, Patrick Kahemele aliiambia MICHARAZO mapema leo kuwa, Humud
atakuwa nchini humo kwa muda wa siku 10 akifanyiwa majaribio na klabu hiyo  inayopigana kutaka kurejea kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Kahemele alisema Humud ameenda Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya klabu yao ya Azam ya kupanua wigo wa wachezaji wa kitanzania kucheza soka nje ya nchi kwa manufaa ya nchi siku za baadaye.
"Humud ameondoka asubuhi hii (jana) kuelekea Afrika Kusini kufanyiwa majaribio katika klabu ya Jomo Cosmo na atakuwa huko kwa siku 10 kabla ya kurejea nchini" alisema Kahemele.
Klabu hiyo ya Cosmo inamilikiwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) Jomo 'Black Prince' Sono, na iwapo Humud atafaulu majaribio yake atafuata nyayo za wachezaji wa Kitanzani kuwahi kuichezea timu hiyo akitanguliwa na nyota wa zamani  Nteze John na Ally Shah kuwahi kufanya hivyo miaka ya nyuma.