Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka asubuhi hii katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 29, 2013. |
Tukio hilo limetokea mishale ya asubuhi katika mitaa ya Posta, jirani na msikiti wa Shia katika eneo la makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi na hadi sasa, miili ya maiti 12 na pia majeruhi 30 wameshachomolewa.
Aidha, harakati zaidi za uokoaji zingali zikiendelea kufanywa na vikosi vya uokoaji. Katika eneo la tukio hilo, tayari viongozi kadhaa wa serikali na makamanda wa Polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam wamefika kusaidia shughuli za uokoaji, miongoni mwao akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa mabaki ya jengo hilo yanaonyesha kuwa mchanga ulikuwa mwingi mno kulinganisha na saruji, hali inayodhaniwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa mjengo huo uliogharimu mamilioni ya pesa.
Pamoja na mashuhuda wa tukio hilo kudai kuna zaidi ya miili ya watu 10 iliyotolewa kwenye uokozi na wengine 30 kukimbizwa hospitalini kwa matibabu kutokana na kujeruhiwa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema ni watu wawili tu waliogundulika kufa mpaka sasa na waliokimbizwa hospitali ni 17 japo shughuli za uokozi zinaendelea.
awa makandarasi wetu wa ss wanatamaa sana ndo wanasababisha kupoteza maisha ya ndugu zetu inaniuma sana jamani.
ReplyDeletemungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi
ReplyDelete