|
Rais wa TFF, Jamal Malinzi |
MCHAKATO wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya timu ya
soka ya Tanzania, Taifa Stars, ulioshirikisha wang’amuzi wa vipaji zaidi
ya 40 umekamilika jana na majina ya nyota hao yataanikwa kesho
Jumatatu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Boniface Wambura, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya kabla ya
kuingia kambini Tukuyu, Mbeya na watakaoingia kambini ni wale
watakaokuwa wamefaulu vipimo.
Wang’amuzi wa vipaji waliokuwa Lushoto ni Abdul Mingange, Ayoub
Nyenzi, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo
Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John
Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Kidao Wilfred, Madaraka
Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa
Kissoky, Nicholas Mihayo, Pelegrinius Rutayuga, Peter Mhina, Salum
Mayanga, Salvatory Edward, Salum Madadi, Sebastian Nkoma, Sekilojo
Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred na Ayoub Nyenzi ambaye
mbali ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana.
Yumo pia Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.
Mkakati huo umebuniwa na TFF kwa lengo la kupata nyota wa kujumuishwa
katika kikosi cha sasa cha Stars inayokabliwa na kampeni ya kuwania
nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON),
zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.