RAHIM JUNIOR
BAADA ya mechi za jana za makundi ya Kombe la Mapinduzi, cheki ratiba na msimamo wa michuano hiyo inayozidi kushika kasi visiwani Zanzibara na itakayofikia tamati Januari 13 ambapo bingwa wa mwaka huu atafahamika.
Kwa sasa Azam ndio wanaoshikilia taji hilo baada ya kuipokonya Simba katika fainali za mwaka jana. Timu hizo zitakutana tena katika mechi kali itakayopigwa usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja.
RATIBA:
Leo Jumamosi
JKU v Singida United
Simba v Azam
Kesho Jumapili
Zimamoto v Yanga
Jumatatu
Simba v URA
Yanga v Singida United
Jumatano, Jan 10, 2018
NUSU FAINALI
Kinara Kundi A v
Mshindi wa Pili Kundi B
Kinara Kundi B v
Mshindi wa Pili Kundi A
Saa 2:15 usiku
Jan 13, 2018
FAINALI
Saa 2:15 usiku
Msimamo:
Kundi A
P W D L F A Pts
1.Singida 3 3 0 0 9 3 9
2.Yanga 3 3 0 0 5 1 9
3.M'ndege 5 2 0 3 5 7 6
4.Taifa 5 1 1 3 3 7 4
5.JKU 4 1 1 2 2 3 4
6. Z'moto 3 1 0 2 3 4 3
Kundi B
P W D L F A Pts
1.URA 3 2 1 0 3 1 7
2.Azam 3 2 0 1 6 1 6
3.Simba 2 1 1 0 4 1 4
4.Mwenge4 1 1 2 2 4 4
5.Jamhuri4 0 1 3 2 9 1
STRIKA
USILIKOSE
Saturday, January 6, 2018
Dk Mwakyembe azindua tamthilia zitakazorushwa DStv, Maisha Magic Bongo
MWANDISHI WETU
WASANII wametakiwa kufaidika na kazi zao za sanaa, ambapo
Serikali pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe, wako tayari kuwasaidia.
Waziri aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa Sarafu na Kampuni, ambazo zitaoneshwa na
kisimbuzi cha DStv.
Tamthilia hizo zitakuwa zikionekana kupitia chaneli ya
Maisha Magic Bongo ili kuwapa burudani zaidi wateja wa DStv.
Mwakyembe alisema kuwa amefurahishwa na kiwango cha hali
ya juu kilichooneshwa katika tamthilia hizo mpya, ambazo zote zimebuniwa na
kutengenezwa hapa nchini na waigizaji wake, wahariri na waongozaji wote ni
Watanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harishon Mwakyembe (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo (wa pili kulia), Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwuingereza (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande (wa pili kushoto) na Mbunge wa Makete Prof. Norman Sigalla King wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI |
Pia amewaasa wasanii kuhakikisha kuwa wanazingatia
maadili ya jamii wakati wote wanapofanya kazi zao za sanaa, kwani sanaa ni kioo
cha jamii na kwamba ikitumika vibaya inaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii
yetu.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Maharage Chande alisema Kapuni ni tamthilia
iliyojaa vituko na misukosuko, ambavyo ni kivutio kwa watazamaji. Alisema Kapuni
imeandaliwa na muandaaji maarufu wa filamu nchini, Leah Mwendamseke na vituko
na misukosuko ya mahusiano na usaliti wa kimapenzi.
Tamthilia hizo zitaanza kurushwa hewa kuanzia wiki ijayo
katika DStv chaneli 160 – Maisha Magic Bongo.
Tamthilia hiyo imechezwa na waigizaji maarufu akiwemo,
Jacqueline Wolper, Gabo, Kajala, Masanja, Jenifer Kyaka (Odama),
Mwanamuziki Quick Rocka, DJ maarufu Rommy Jones na mastaa
wengine wengi.
Wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu hapa nchini wakifuatilia
kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI zitakazoonekana
katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu wakati wa uzinduzi wa
tamthilia hizo jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Tamthilia
hizo zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala,
Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Irene Uwoya,
Idris Sultan na wengineo.
|
Chande aliongeza kusema kuwa tamthilia ya Sarafu iliyoandaliwa
na John Samwel Isike, nayo ni maridadi iliyobeba marafiki wawili ambao
wanaingia kwenye chuki na uadui mkubwa mpaka kuingiza familia zao kwenye
hatari, kisa ni fedha zinazozaa kiburi, dharau na anasa za kupitiliza.
Waigizaji maarufu
akiwemo Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Mzee Chilo, Elizabeth Michael
(Lulu), Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa
wengineo wamo kwenye tamthilia hiyo.
DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhiu ya
Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato
kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishawa tarehe 1 Octoba
2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na pia
kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.
Kwa kipindi chote
hiki Chanel hii imekuwa kwa haraka sana, ambapo kwa sasa ni miongoni mwa
Channel zenye watazamaji wengi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Channel
hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya wasanii hapa nchini, huku mamia ya wasanii
wakipata fursa mbalimbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na
pia kupata mafuzo na kipato kupitia Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha Magic
Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa katika soko
kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania,
pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU, KITIMTIM ambazo
zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
Kuingizwa kwa tamthilia mpya za Kapuni na Sarafu, nu
muendelezo wa mkakati wa Chaneli hii kuongeza maudhui ya kitanzania, na kuwapa
watanzania burudani inayoendana na wakati na yenye kuakisi maisha halisi ya
kitanzania.Credit:MLEKANI
Wenger apewa kibano, kisa kumkoromea refa
Kiocha Arsene Wenger akikoromeana na mwamuzi |
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich Jumapili iliyopita.
Kocha huyo alifanya kitendo hicho baada ya kukasirikia kitendo cha mwamuzi huyo Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia mkononi Calum Chambers.
Alimfuata Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya 1-1.
Wenger alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carabao dhidi ya Chelsea.
Liver, Man Utd watakata, Lukaku, Virgil watupia
Virgil akishangilia bao lake |
Lukaku akishiangilia bao akiwa na Lingard |
Man United wakipongezana |
Liverpool wakipongezana |
MANCHESTER United imeendelea kugawa dozi baada ya usiku wa kuamkia leo kuitungua Derby Count kwa mabao 2-0, huku LIverpool wakiitoa nishai Everton kwa kuichapa mabao 2-1 katika mchezo mwingine mkali wa michuano hiyo.
Romelu Lukaku aliifungia Man United bao la pili dakika ya 90 huku Jesse Lingard akitupia kambani bao la kuongoza dakika ya 84 katika mechi kali iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford.
Katika pambao jingine Liverpool ikiwa uwanja wa nyumbani wa Anfield iliitandika wapinzani wao wa jadi Everton kwa mabao 2-1 na kuing'oa kwenye michuano hiyo.
Beki wa Liverpool, Mholanzi Virgil van Dijk akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Wenyeji walitangulia kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kupitia James Milner dakika ya 34 kabla ya Gylfi Sigurosson kuisawazisha Everton katika dakika ya 65 na kwenye dakika ya beki mpya wa Liverpool, Virgil van Dijk alitupia kambani bao la ushindi dakika sita kabla ya kumalizika kwa pambano hilo.
Ushindi huo umeifanya Liverpool kuungana na Man United kutinga Raundi ya Nne ya michuano hiyo na leo Jumamosi na kesho Jumapili michezo mingine kibao itapigwa katika mfululizo wa michuano hiyo mikongwe nchini England.
Yanga hiyooo, Simba, Azam mechi ya kisasi
Azam FC itakayovaana na Simba usiku wa leo |
Simba watakaokuwa na kibarua mbele ya watetezi wa Mapinduzi, Azam FC |
Yanga waliotangulia nusu fainali ya Mapinduzi usiku wa jana |
WAKATI Simba usiku huu ikishuka uwanjani katika mechi ya kisasi dhidi ya Azam, watani zao usiku wa kuamkia leo wametangulia nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi wakiungana na Singida United.
Singida inayoongoza Kundi A ikiwa na alama 9 sawa na Yanga ila ikiwa na faida ya mabao ya kufungwa na kufungwa, itashuka tena uwanjani jioni ya leo kuvaana na JKU katika pambano jingine linalotarajiwa kuwa kali itakayochezwa Uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Maafande wa JKU wataivaa Singida ikiwa inauguza kidonda cha kutunguliwa bao 1-0 na Yanga katika mechi yao iliyopita na itakuwa ikikamilisha ratiba tu kwani hata kama itaifunga Singida itafikisha pointi 7 ambazo zimeshapitwa na wapinzani wao.
Yanga ilitinga nusu fainali baada ya kuifunga Taifa Jang'ombe kwa mabao 2-0, mabao yaliyowekwa kimiani katika vipindi vyote. La kwanza likifungwa na Ibrahim Ajib dakika chache kabla ya mapumziko na jingine la Yohana Mkomola kwenye dakika ya 60 na kuifanya Yanga kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ikiwa na michezo miwili mkononi dhidi ya Zimamoto na Singida United zitakazopigwa kati ya kesho Jumapili na Jumatatu mtawalia.
Hata hivyo Yanga na Singida zikitangulia mapema nusu fainali, wapinzani wao Simba watakuwa na kibarua kizito usiku wa leo kwa kuvaana na Azam katika mechi ya kisasi na inayorejesha kumbukumbu ya fainali ya michuano iliyopita.
Simba ilicharazwa na Azam kwa bao 1-0 katika fainali ya mwaka jana ya michuano hiyo na kuwaacha matajiri hao wa Chamazi wakibeba taji kwa mara ya tatu wakifikia rekodi ya Wekundu wa Msimbazi.
Mchezo wa leo ni vita baada ya Azam jana kulala 1-0 mbele ya URA wanaoongoza kundi lao la B na ushindi pekee ndio utakawanusuru wasiliteme taji hilo la sivyo itawaacha Simba wakiungana na Waganda kucheza hatua hiyo itakayoanza Januari 10.
Simba kupitia Kocha wake, Masudi Djuma imetamba kukata tiketi hiyo kwa sababu imepanga mwaka huu kubeba kila taji baada ya kutemeshwa taji lao la Kombe la FA na timu ya Green Warriors iliyopo Ligi Daraja la Pili (SDL).
Simba ipo nafasi ya tatu nyuma ya URA na Azam ikiwa na alama nne baada ya kupata sare moja na kushinda mchezo mwingine wa mwisho na kama itaichapa Azam, licha ya kulipa kisasi cha mwaka jana, lakini itafuzu nusu fainali.
Watetezi ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu na kufungwa bao la kwanza katika Mapinduzi tangu mwaka jana walipobeba taji bila kupoteza wala kufungwa bao, imetamba tiketi yao ya nusu fainali wanayo Simba na lazima wawape. Ngoja tuone itakavyokuwa baada ya kipyenga cha mwisho usiku wa leo.
Subscribe to:
Posts (Atom)