MWANDISHI WETU
WASANII wametakiwa kufaidika na kazi zao za sanaa, ambapo
Serikali pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe, wako tayari kuwasaidia.
Waziri aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa Sarafu na Kampuni, ambazo zitaoneshwa na
kisimbuzi cha DStv.
Tamthilia hizo zitakuwa zikionekana kupitia chaneli ya
Maisha Magic Bongo ili kuwapa burudani zaidi wateja wa DStv.
Mwakyembe alisema kuwa amefurahishwa na kiwango cha hali
ya juu kilichooneshwa katika tamthilia hizo mpya, ambazo zote zimebuniwa na
kutengenezwa hapa nchini na waigizaji wake, wahariri na waongozaji wote ni
Watanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harishon Mwakyembe (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo (wa pili kulia), Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwuingereza (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande (wa pili kushoto) na Mbunge wa Makete Prof. Norman Sigalla King wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI |
Pia amewaasa wasanii kuhakikisha kuwa wanazingatia
maadili ya jamii wakati wote wanapofanya kazi zao za sanaa, kwani sanaa ni kioo
cha jamii na kwamba ikitumika vibaya inaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii
yetu.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Maharage Chande alisema Kapuni ni tamthilia
iliyojaa vituko na misukosuko, ambavyo ni kivutio kwa watazamaji. Alisema Kapuni
imeandaliwa na muandaaji maarufu wa filamu nchini, Leah Mwendamseke na vituko
na misukosuko ya mahusiano na usaliti wa kimapenzi.
Tamthilia hizo zitaanza kurushwa hewa kuanzia wiki ijayo
katika DStv chaneli 160 – Maisha Magic Bongo.
Tamthilia hiyo imechezwa na waigizaji maarufu akiwemo,
Jacqueline Wolper, Gabo, Kajala, Masanja, Jenifer Kyaka (Odama),
Mwanamuziki Quick Rocka, DJ maarufu Rommy Jones na mastaa
wengine wengi.
Wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu hapa nchini wakifuatilia
kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI zitakazoonekana
katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu wakati wa uzinduzi wa
tamthilia hizo jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Tamthilia
hizo zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala,
Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Irene Uwoya,
Idris Sultan na wengineo.
|
Chande aliongeza kusema kuwa tamthilia ya Sarafu iliyoandaliwa
na John Samwel Isike, nayo ni maridadi iliyobeba marafiki wawili ambao
wanaingia kwenye chuki na uadui mkubwa mpaka kuingiza familia zao kwenye
hatari, kisa ni fedha zinazozaa kiburi, dharau na anasa za kupitiliza.
Waigizaji maarufu
akiwemo Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Mzee Chilo, Elizabeth Michael
(Lulu), Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa
wengineo wamo kwenye tamthilia hiyo.
DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhiu ya
Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato
kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishawa tarehe 1 Octoba
2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na pia
kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.
Kwa kipindi chote
hiki Chanel hii imekuwa kwa haraka sana, ambapo kwa sasa ni miongoni mwa
Channel zenye watazamaji wengi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Channel
hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya wasanii hapa nchini, huku mamia ya wasanii
wakipata fursa mbalimbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na
pia kupata mafuzo na kipato kupitia Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha Magic
Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa katika soko
kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania,
pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU, KITIMTIM ambazo
zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
Kuingizwa kwa tamthilia mpya za Kapuni na Sarafu, nu
muendelezo wa mkakati wa Chaneli hii kuongeza maudhui ya kitanzania, na kuwapa
watanzania burudani inayoendana na wakati na yenye kuakisi maisha halisi ya
kitanzania.Credit:MLEKANI
No comments:
Post a Comment