STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, December 6, 2014

Man City yaiua Everton 1-0, yazidi kuipumulia Chelsea

Manchester City v Everton
Yaya Toure akitumbukiza penati yake wavuni kuibeba Manchester City dhidi ya Everton
BAO la mkwaju wa penati lililofungwa na Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure yameiwezesha Manchester City kupatya ushindi mwembamba nyumbani dhidi ya Everton na kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Chelsea kufikia pointi tatu tu.
Toure alifunga bao hilo katika dakika ya 24 baada ya Phil Jagielka kumchezea rafu James Milner na yeye kutofanya ajizi kuukwamisha mpira kimiani na kuifanya City ambao ni mabingwa watetezi kufikisha pointi 33 na kung'ang'ania nafasi ya pili nyuma ya Chelsea ambayo mapema leo mchana ilikubali kipigio cha mabao 2-1 toka kwa wenyeji wao Newcastle United na kusitishiwa mfululizo wake wa ushindi katika msimu huu.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Jumatatu kwa pambano moja tu litakaloikutanisha Southmapton dhidi ya Mashetani Wekundu, Manchester United.

Taifa Stars maboresho yarejea Dar, kuisubiri Burundi


KIKOSI cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.
Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu

AS Roma chupuchupu nyumbani

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Alessandro+Florenzi+Roma+v+Sassuolo+Calcio+ppMmPHbtvgel.jpg
KLABU ya AS Roma usiku huu imenusurika kuumbuliwa nyumbani baada ya kuchomoa mabao mawili dakika za 'jioni' na kuambulia sare dhidi ya Sassuolo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Italia, Serie A.
Roma walikuwa wakifukuzia nafasi ya kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Juventus, walishtykizwa kwa kufungwa mabao mawili ya haraka na wageni wao kupitia kwa Simone Zaza.
Zaza alifunga bao la kwanza dakika ya 15 kabla ya kuongeza la pili dakika tatu baadaye na kuwapa wakati mgumu wenyeji waliopigana kipindi cha pili na kufanikiwa kuyarushisha.
Mchezaji Adem Ljajić alianza kupunguza aibu katika dakika ya 78 kwa kufungwa kwa mkwaju wa penati kabla ya kupongeza la pili dakika za nyongeza na kuipa Roma sare hiyo ya 2-2 na kuambulia pointi moja.
Pointi hiyo imeifanya Roma kuendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na pointi  32, tatu na ilizonazo Juventus ambao jana waling'ang'aniwa na Fiorentina na kutoka nao suluhu ugenini ya bila kufungana.

Al Ahly mabingwa Kombe la Shirikisho

http://english.ahram.org.eg/Media/News/2014/9/20/2014-635468104658720940-872.jpg
http://news.bbcimg.co.uk/media/images/71031000/jpg/_71031520_187561109.jpgKLABU ya Al Ahly ya Misri imeweka rekodi ya aina yake baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuicharaza Sewe Sports ya Ivory Coast bao 1-0 katikka mchezo wa pili wqa fainali za michuano hiyo.
Al Ahly walikuwa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kung'olewa na kutupwa kwenye michuano hiyo ya Shirikisho, imetwaa taji hilo kwa faida ya bao la ugenini baada ya wiki iliyopita kucharazwa mabao 2-1 na hivyo kwa ushindi wake wa nyumbani umefanya matokeo kuwa 2-2.
Bao lililowahihikishia wababe hao wa Misri ambao walinyolewa bao 1-0 na Yanga katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kwenda kuitoa Yanga kwa matuta nyumbani, lilifungwa Emad Moteab katika dakika za nyongeza na kuipa timu hiyo taji lake la kwanza la michuano hiyo na kuweka rekodi ya kutwaa mataji ya Kombe la Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa kufuatana.

Zlatan Ibrahimovic aipaisha PSG Ufaransa

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/70314000/jpg/_70314410_019566211-2.jpgMSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic amerejea dimbani kwa kishindo baada ya kuiongoza timu yake ya PSG kupata ushindi nyumbani wa mabao 2-1 dhidi ya Nates.
Ushindi huo umeifanya PSG kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Ufaransa.
Ibrahimovic aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu alifunga mabao hayo katika dakika ya 34  akimalizia kazi ya Lucas na katika dakika ya 48 kwa mkwaju wa adhabu ndogo na kuifanya watetezi hao wa Ligue 1 kufikisha pointi 37 kwa michezo 17 na kukaa kileleni.
Bao la wageni lilifungwa mapema katika dakika ya nane kupitia kwa Bedoya kabla ya wenyeji kucharuka na kulisawazisha na kuongeza la ushindi.

Atletico Madrid yaipumulia Real Madrid Hispania

Atletico Madrid's Jose Maria Gimenez (left) celebrates scoring the opening goalKLABU ya Atletico Madrid imewapumulia wapinzani wao wa jadi, Real Madrid baada ya jioni ya leo kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Elche.
Mabao ya Giménez dakika ya 16 na lingine la Mario Mandžukić dakika ya 53 yaliwapa ushindi mabingwa hao watetezi wa La Liga na kupunguza pengo lao la pointi dhidi ya Real Madrid na kuwa moja.
Atletico wamefikisha pointi 32 dhidi ya 33 za Real Madrid ambayo baadaye usiku huu itamenyana na Celta de Vigo.
Mbali na pambano la Real Madrid na Celta Vigo pia viwanja vingine vitawaka moto katika ligi hiyo ya Hispania.

Kocha Kibadeni azushiwa kifo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIr7CA9EVODV1M5m645oWLJL-5j77KmrzS3qA_nGob2Ld5JeDwq3CKoQK7AauIsYbHjXNJA6t9cV-SMYPzkTeUc7s_GbXVJiUUc0sSl842p0Gc6YxiT7Ck5QKkO1SY-0BY6z_M2nX94vTW/s1600/Kinesi.jpgKOCHA na nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.
Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara, na wengine kuipigia MICHARAZO kutaka ufafanuzi ambao hata hivyto ilikuja kubainika kuwa ni uongo.
Kocha huyo aliyewahi kuwa nyota wa klabu za Simba na Majimaji na Taifa Stars alisema hajui aliyezua jambo hilo alikuwa na lengo gani kwani limempa usumbufu yeye na watu wengine.
"Mimi ni mzima buheri, siumwi wala sijapata ajali wala jambo lolote baya na sijui aliyefanya hivi alikuwa na lengo gani, ila nadhani ni uhuru uliopo sasa kuanzia mitandao ya kijamii," alisema na kuongeza;
“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.
“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.
“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.
“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.”

Ubaguzi! Mchezaji afungiwa kwa kubaguliwa Urusi

Kanga (kushoto) aliyefungiwa Russia kwa kutoa ishara za matusi baada ya kubaguliwa na mashabiki wa Spartak Moscow
KIUNGO wa kimataifa wa Gabon, Guelor Kanga amefungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la Urusi, RFU baada ya kuonyeaha ishara ya matusi akikerwa na ubaguzi aliofanyiwa na mashabiki wa Spartak Moscow.
Kanga alionyesha ishara hiyo baada ya kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Spartak Moscow ambao walimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi. 
Kiungo huyo wa klabu ya FC Rostov mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akipigiwa kelele za nyani na mashabiki wa Spartak wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini humo uliofanyika jijini Moscow.
Katika kujibu mapigo ya kejeli hizo nyota huyo alitoa ishara hizo hatua ambayo RFU ilibidi kuchukua hatua kwa kumtoza pia na faini ya paundi 600. 
Spartak nao walitozwa faini ya paundi 830 kutokana na mashabiki wao kuonyesha vitendo vya kibaguzi. 
Septemba mwaka huu beki wa Dynamo Moscow Christopher Samba alifungiwa mechi mbili kwa kufanya tukio kama hilo wakati mashabiki wa timu ya Torpedo Moscow walivyomfanyia vitendo vya kibaguzi.
KIUNGO wa kimataifa wa Gabon, Guelor Kanga amefungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la Urusi-RFU kwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Spartak Moscow ambao walimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi. Kiungo huyo wa klabu ya FC Rostov mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akipigiwa kelele za nyani na mashabiki wa Spartak wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini humo uliofanyika jijini Moscow jana. Nyota huyo naye alijibu mapigo hatua ambayo RFU ilibidi kuchukua hatua kwa kumtoza pia na faini ya paundi 600. Spartak nao walitozwa faini ya paundi 830 kutokana na mashabiki wao kuonyesha vitendo vya kibaguzi. Septemba mwaka huu beki wa Dynamo Moscow Christopher Samba alifungiwa mechi mbili kwa kufanya tukio kama hilo wakati mashabiki wa timu ya Torpedo Moscow walivyomfanyia vitendo vya kibaguzi.

Make Money