STRIKA
USILIKOSE
Saturday, December 6, 2014
Al Ahly mabingwa Kombe la Shirikisho
KLABU ya Al Ahly ya Misri imeweka rekodi ya aina yake baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuicharaza Sewe Sports ya Ivory Coast bao 1-0 katikka mchezo wa pili wqa fainali za michuano hiyo.
Al Ahly walikuwa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kung'olewa na kutupwa kwenye michuano hiyo ya Shirikisho, imetwaa taji hilo kwa faida ya bao la ugenini baada ya wiki iliyopita kucharazwa mabao 2-1 na hivyo kwa ushindi wake wa nyumbani umefanya matokeo kuwa 2-2.
Bao lililowahihikishia wababe hao wa Misri ambao walinyolewa bao 1-0 na Yanga katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kwenda kuitoa Yanga kwa matuta nyumbani, lilifungwa Emad Moteab katika dakika za nyongeza na kuipa timu hiyo taji lake la kwanza la michuano hiyo na kuweka rekodi ya kutwaa mataji ya Kombe la Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa kufuatana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment