KIKOSI
cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu
mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa
dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu
hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja
kambini hoteli ya Tansoma.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu)
itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati
keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa
Taifa.
Nayo
timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu)
saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya
Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.
Kiingilio
cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya
raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu
No comments:
Post a Comment