STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 6, 2014

Ajali nyingine basi la AM Coach lagongana na lori Tabora


Ajali mbaya ya basi la kampuni ya AM Coach lenya namba T 763 AYN imetokea leo asubuhi mkoani Tabora baada ya basi hilo kugongana na lori mali ya kampuni ya soda ya Coca Cola lenye namba za usajili T 256 BPP

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tabora ajali hiyo ilitokana lori hilo kutaka kulipita basi bila kuwa makini na kisha kwa ufinyu wa barabara hiyo ndipo ikatokea 'mzinga' huo.
Mmoja wa abiria aliyenusurika alinukuliwa akisema kuwa;

"Dereva wa lori kajaribu kutukwepa lakini ufinyu wa barabara, mbele kuna lori scania linakuja,kwa hiyo akajikuta kagonga kushoto kwake na kulia kwake ila lori la kushoto kwetu halikusimama

Dereva wetu akashindwa kurudi upande wa kushoto kwa sababu kulikuwa na lori ambalo alikuwa anataka kulipita, basi letu lilikuwa 'linaovertake'(linataka kupita), basi nia AM Coach na lori ni la Coca Cola"

Bado haijafahamika madhara makubwa ya ajali hiyo ila taarifa zinafuatiliwa.
Ajali hiyo imekuja siku chache baada ya watu saba kupoteza maisha yao katika ajali mbaya iliyotokea eneo la Chalinze mkoani Pwani ikihusisha magari mawili ikiwamo Coaster iliyokuwa imebeba abiria.
EDDY

Neymar ampagawisha 'dogo' Sauzi

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano jana usiku alivamia ndani ya uwanja wakati Brazil ilipokuwa ikimenyana na Afrika Kusini na kwenda moja kwa moja kwa mshambuliaji Neymar wa Brazil. 
Katika kuonyesha furaha ya kufuatwa na mchezaji huyo, Neymar aliamua kumkumbatia na kisha wachezaji wote wa Brazil waliamua kumbeba juu. Katika mechi hiyo, Brazil iliinyuka Afrika Kusini mabao 5-0, huku Neymar akifunga mabao matatu (hat trick).

Party maalum Siku ya Wanawake kufanyika Mango Garden




KATIKA kusherehekea siku ya Wanawake Jumamosi hii tarehe 08-03-2014 Bendi yako PENDWA ya Twanga Pepeta ikishirikiana na Mdau wake mkubwa Christer Bella Mwingira na Rukia Saloon, kwa pamoja wameandaa bonge la Pati kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hii.
Pati linataraji kufanyika ndani ya Twanga City Mango Garden ambapo muonekano wake utakuwa tofauti na siku za kawaida kwa kuwa ukumbi utapambwa vilivyo.
Mavazi rasmi yatakuwa ni ya ya rangi NYEKUNDU, NYEUPE na NYEUSI.
Zawadi kedekede zitatolewa na Rukia Saloon na Christer Bella Mwingira kama vitenge na Khanga ambayo ni mavazi rasmi ya mwanamke.
Kutakuwa na ofa maalum kwa ajili ya akina mama toka kwa Mkurugenzi wetu Asha Baraka kwa kila atakayefika katika onyesho atalipia Tshs 5,000. kuanzia saa mbili mpaka saa nne usiku.
Kiingilio kitakuwa ni Tshs 10,000. kwa VIP pamoja na kinywaji na kawaida ni Tshs 7,000/=

Shigongo afafanua madhara ya Ugonjwa wa Ini


Shigongo akizungumza kwa masikitiko jinsi watu wengi walivyo kwenye hatari ya kufa kwa ugonjwa wa ini.

…Akiwa na jopo la madaktari. Kushoto ni Dk. Mtebe Majigo, Mganga Mkuu wa Amana, Meshack Shing'wela (wa pili kulia) na Daktari Kiongozi Andrew Method.

Ndeonasio Towo kutoka Damu Salama akielezea umuhimu wa wananchi kupima damu kubaini maradhi mbalimbali bila kusahau virusi vya homa ya ini.
Mwakilishi kutoka SD Tanzania ambao ni wadau wa ugonjwa huo, Phillip Sawe, akielezea umuhimu wa kupima mapema ugonjwa huo kabla mwili haujashambuliwa.
Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Andrew Method (kulia) akisistiza jambo.
Mapaparazi kazini.
Shigongo akimueleza jambo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kushoto) na Mwakilishi kutoka Sanofa, Edwin Kisimbo, wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikiendelea.
Dk. Majigo (wa pili kulia) akielezea ugonjwa huo unavyoambukiza kwa njia ambazo huambukiza Ukimwi.
Meshack Shing'wela akifafanua jambo.
…Akimshukuru Shigongo kwa kuanzisha kampeni za kutokomeza ugonjwa huo.
MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, na wadau mbalimbali wa afya leo walizungumzia madhara ya ugonjwa hatari wa homa ya ini kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana Jijini Dar.
Miongoni mwa wadau waliokuwa kwenye mkutano huyo ni madaktari mbalimbali, Sanofa ambao huhusika na vipimo vya ugonjwa huo, Damu Salama ambao huhusika na upimaji wa damu na SD Tanzania.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Ujerumani, England, Ureno zaua kirafiki Ulaya


article-2574068-1C10556200000578-473_634x396
Ujerumani wakishangilia goli lao dhidi ya Chile
Ronaldo akipambana na kuweka rekodi ya mabao dhidi ya Cameroon walioizabua 5-1

Messi alishindwa kuibeba Argentina dhidi ya Romania
Italia walitepeta kwa Hispania 1-0, Diego Costa akiichezea timu yake hiyo kwa mara ya kwanza

Sturridge akishangilia bao liliuloibeba England jana
UJERUMANI usiku wa jana imefanikiwa kuizabua Chile kwa kuwalaza bao 1-0, huku England nayo ikipata ushindi kama huo kwa Denmark, na Brazili ikiifanyizia Afrika Kusini kwa kuifunga kwao mabao 5-0.
Bao la Ujerumani katika mechi yake na Chile lilifungwa na Mario Gotze aliyeshirikiana vyema na Mesut Ozil.
Matokeo mengine ya michezo ya kirafiki ya kimataifa inayotambuliwa na FIFA iliyochezwa jana na alfajiri ya leo Hispania iliilaza Italia baop 1-0 na kudhihirisha haikuiotea kwenye Fainali za Ulaya walipoisasambua mabao 4-0 mpaka kumfanya Mario Balotelli kumwaga chozi.
Mexixo na Nigeria zenyewe zilishindwa kufungana, Ivory Coast ikitoka sare ya mabao 2-2  na Belgiaum, huku Ureno ikiifumua Cameroon kwa mabao 5-1 Cristiano Ronaldo akifunga mawili na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji wenye mabao mengi kwa timu ya taifa lake akimzidi Pauleta.
amabaoUshirikiano wa kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil ulizaa matunda jana usiku katika mchezo wa kirafiki baina ya Ujerumani dhidi ya Chile.
Wachezaji wawili walishirikiana vizuri katika goli la ushindi lilofungwa na Gotze kutoka na pasi nzuri ya mwisho ya Ozil. Mchezo ulimalizika kwa matokeo ya 1-0.

Matokeo Mengine ni kama ifuatavyo
Japan     4 - 2     New Zealand    
Iran     1 - 2     Guinea    
Russia     2 - 0     Armenia    
Bulgaria     2 - 1     Belarus    
South Africa     0 - 5     Brazil    
Algeria     2 - 0     Slovenia    
Namibia 1-1 Tanzania
Greece     0 - 2     Korea Republic    
Hungary     1 - 2     Finland    
Montenegro     1 - 0     Ghana    
Czech Republic     2 - 2     Norway    
Israel     1 - 3     Slovakia    
Bosnia-Herzegovina     0 - 2     Egypt    
Cyprus     0 - 0     Northern Ireland    
Colombia     1 - 1     Tunisia    
Turkey     2 - 1     Sweden    
Romania     0 - 0     Argentina        
Ukraine     2 - 0     United States    
Austria     1 - 1     Uruguay    
Switzerland     2 - 2     Croatia    
Germany     1 - 0     Chile    
Republic of Ireland   1 - 2     Serbia    
Belgium     2 - 2     Côte d'Ivoire    
Poland     0 - 1     Scotland    
Wales     3 - 1     Iceland    
France     2 - 0     Netherlands    
England     1 - 0     Denmark    
Australia     3 - 4     Ecuador    
Portugal     5 - 1     Cameroon    
Spain     1 - 0     Italy    
Honduras     2 - 1     Venezuela    
Mexico     0 - 0     Nigeria        
Costa Rica     2 - 1     Paraguay

Yanga wapaa kuifuata Al Ahly ikijiamini

KIKOSI cha wachezaji 18 na viongozi wa klabu ya Yanga wameodnoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea Misri kwa ajili ya pambano lao la marudiano dhidi ya Al Ahly wakijiamini wanaenda kumaliza kazi.

Msafara huo umeondoka bila nyota wake kutoka Uganda,Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokuwa nchini Zambia kuichezea timu yao ya taifa Uganda The Cranes ambao walilala 2-1 kwa wenyeji wao Chipolopolo.
Hata hivyo wachezaji hao wanatarajiwa kuungana nao wenzao nchini Misri baadaye leo mchana wakitokea Zambia tayari kuivusha Yanga kwenye hatua ya 32 na kuipeleka katika 16 Bora mbele ya mabingwa wateteziu hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo.
Wachezaji waliondoka kwenda kuiua Al Ahly ni  Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Kaseja, Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Oscar Jushua, Nizar Alfan, Franck Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, David Luhende na Jerry Tegete.
Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga mpaka sasa hawajajua mechi yao itakayochezwa Jumapili usiku itafanyika kwenye uwanja gani baada ya uongozi wa Al Ahly kuficha taarifa hizo mpaka jana mchana.
Hata hivyo, Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto aliyetangulia Cairo alsema huenda  mchezo huo ukachezwa kwenye Uwanja wa Arab Contractors uliopo jijini Cairo. na kwamba maandalizi ya kuipokea timu yao inaendelea vyema kujipanga kuivaa wenyeji wao ambao hawaamini mpaka sasa kama walefungwa na timu ya Afrika Mashariki .

Cannavaro atamba Yanga itafanya maajabu Cairo

 
NAHODHA wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kwamba kikosi chao kitafanya maajabu kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, Al Ahly ya Misri siku ya Jumapili.
Yanga itaumana na Al Ahly katika mechi yao ya marudiano ya hatua ya kwanza itakayochezwa usiku wakiwa na ushindi wa 1-0 waliopata katika pambano lao la awali jijini Dar es Salaam kupitia goli lililofungwa kwa kichwa katika dakika ya 82 na nahodha huyo.
Akizungumza na MICHARAZO, Cannavaro alisema wanajua wa mchezo huo utakuwa ni mgumu, lakini wanaenda Cairo kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kuivusha Yanga kwenye 16 Bora.
"Tutaenda kupambana japo tunatarajia ushindani mkubwa baada ya kuwafunga hapa nyumbani," alisema beki huyo wa kati.
Cannavaro alisema wachezaji karibu wote watakaokuwa kwenye msafara wao uliotarajiwa kuondoka usiku wa jana, wamepania kuhakikisha Yanga inaing'oa Al Ahly na kurejea kilichowahi kufanywa na watani zao Simba mwaka 2003.
Katika mwaka huo Simba iliwafunga waliokuwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa, Zamalek pia ya Misri kisha kwenda kukubali kipigo cha 1-0 ugenini na kufanya timu hizo zikipigiane penalti na Simba kushinda kwa mikwaju 3-2.
"Tupo tayari kwa vita na Inshallah tutapambana mpaka kieleweke mjini Cairo kwa sababu tumepania kuifikisha mbali timu yetu, " alisema Cannavaro.
Bao la Cannavaro alililofungwa kwa kichwa cha kuchupia liliiwezesha Yanga kuvunja uteja kwa timu za Afrika Kaskazini zikiwamo kutoka Misri uliodumu kwa miaka zaidi ya 30 na watalazimika kupata japo sare ugenini ili kusonga mbele.

'Simba hatuhusiki uvunjwaji wa viti Taifa'

UONGOZI wa Klabu ya Soka ya Simba umesema kuwa hauhusiki na vurugu za kuvunja viti zilizotokea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga inacheza mechi yake ya mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, Al Ahly ya Misri.
Simba ilisema jana kuwa imeamua kutoa taarifa hiyo kutokana na kuwapo kwa 'uvumi' kwamba klabu hiyo huenda ikapigwa faini kufuatia baadhi ya mashabiki wake kudaiwa kuvunja viti siku ya mchezo huo.
Baadhi ya picha zilizoonekana kwenye vyombo vya habari zilionyesha mashabiki waliovaa jezi nyekundu na wengine njano wakirushiana viti na kuacha kushangilia.
Afisa Habari wa klabu hiyo, Asha Muhaji, alisema kuwa mashabiki wa Simba hawawezi kuvunja viti kwa sababu mechi hiyo ilikuwa inawahusu wapinzani wao, Yanga na Al Ahly.
Muhaji alisema kuwa si kila shabiki aliyevaa jezi nyekundu ni wa Simba kwa sababu rangi hiyo inavaliwa na klabu mbalimbali za hapa nchini kama Coastal Union, Small Simba na Al Ahly iliyokuwa inashiriki mchezo huo.
"Sisi tunaamini waliofanya vurugu ni mashabiki wa Al Ahly ambao ndio walikuwa na wapinzani wa Yanga, inashangaza Simba tunatajwa kuhusika na vurugu hizo katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo," alisema Muhaji.
Aliongeza kwamba Simba inataka kuweka wazi kuwa vurugu zilizofanyika katika mchezo huo haziwezi kuhusishwa na klabu yao kwa namna yoyote.
Mara kadhaa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amekuwa akisisitiza mashabiki wa soka kuwa wazalendo pale timu mojawapo inapokuwa inapeperusha bendera ya nchi kushangilia na kuacha mazoea ya kuzomea.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema linaendelea kufanya uchunguiz juu ya tukio hilo kabla ya kutoa tamko, japo imelaani vurugu hizo na kuwaonya mashabiki kuwa wastaarabu kwa kuwa uwanja wa Taifa siyo wa klabu chache bali ni wa Watanzania wote.

Taifa Stars angalau, yatoka sare ya 1-1 ugenini Namibia

Na Prince Akbar, Windhoek, Namibia
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado hazijafungana na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni, Ramadhani Singano ‘Messi’ na juma Luizio na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Athanas Mdam na khamisi Mcha ‘Vialli’.
Kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa, Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Namibia, Brave Warriors na kutoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mchezaji wa Taifa Stars, Jonas Mkude  (katikati) akijaribu kupiga mpira katikati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma  jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Saidi Morad  (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ Lous Jereme  wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Erasto Nyoni (kulia) akijaribu kuudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ Puriza Hosea wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma  jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 baada ya kona  iliyopigwa na Khamisi Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi na kuingia moja kwa moja nyavuni bila kuguswa.
Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni kwa adhabu.
Refa wa mechi hiyo aliingia lawamani kwa kuzidisha muda kupita kiasi, kwani mwamuzi wa mezani alionyesha dakika tano za nyongeza lakini muamuzi alichezesha dakika tano nyingine hivi kuwawezesha Namibia kupata bao.
Lakini katika hali ya kushangaza waamuzi toka nchini Zambia na msimamizi wa mechi toka nchini Afrika Kusini waliopangiwa kuchezesha mchezo huo hawakutokea, na badala yake shirikisho la soka Namibia NFA, wakaamuru mchezo huo uchezeshwe na waamuzi wa Namibia kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mwalimu Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana.
Wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha Stars ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto ambao hawakuruhusiwa na vilabu vyao kutokana na kukosekana na usafiri wa kuwarudisha vilabuni kwa muda unaotakiwa.
Wengine walioshindwa kufika ni Edward Charles na Hassan Masapili ambao hati zao za kusafiri hazikuwa zimekamilika. Viwango
Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.
BIN ZUBEIRY