Na Prince Akbar, Windhoek, Namibia
TIMU
ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imetoka sare ya kufungana bao
1-1 na Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na
Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini
Namibia.
Hadi
dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado
hazijafungana na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi
cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni, Ramadhani Singano ‘Messi’ na juma
Luizio na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Athanas Mdam na
khamisi Mcha ‘Vialli’.
Kikosi
cha kwanza cha Timu ya Taifa, Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja
kabla ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Namibia, Brave Warriors na
kutoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager.
Mchezaji wa Taifa Stars, Jonas Mkude
(katikati) akijaribu kupiga mpira katikati ya wachezaji wa timu ya
taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ wakati wa mchezo wa kimataifa wa
kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma jana
usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Saidi Morad
(kulia) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave
Warriors’ Lous Jereme wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina
ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma jana usiku. Tumu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Erasto Nyoni
(kulia) akijaribu kuudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa timu ya taifa ya
Namibia ‘Brave Warriors’ Puriza Hosea wakati wa mchezo wa kimataifa wa
kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma jana
usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Stars,
inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ndio walikuwa wa
kwanza kupata bao katika dakika ya 86 baada ya kona iliyopigwa na
Khamisi Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi na kuingia moja kwa moja nyavuni
bila kuguswa.
Namibia
walisawazisha bao hilo katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada
ya kutimu dakika 90 za kawaida, lililofungwa na Nekundi Haleluya
Panduleni kwa adhabu.
Refa
wa mechi hiyo aliingia lawamani kwa kuzidisha muda kupita kiasi, kwani
mwamuzi wa mezani alionyesha dakika tano za nyongeza lakini muamuzi
alichezesha dakika tano nyingine hivi kuwawezesha Namibia kupata bao.
Lakini
katika hali ya kushangaza waamuzi toka nchini Zambia na msimamizi wa
mechi toka nchini Afrika Kusini waliopangiwa kuchezesha mchezo huo
hawakutokea, na badala yake shirikisho la soka Namibia NFA, wakaamuru
mchezo huo uchezeshwe na waamuzi wa Namibia kwa makubaliano ya pande
zote mbili.
Mwalimu
Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi
hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo
yaliyopatikana.
Wachezaji
walioshindwa kujiunga na kikosi cha Stars ni Mbwana Samatta, Thomas
Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto ambao hawakuruhusiwa na vilabu vyao
kutokana na kukosekana na usafiri wa kuwarudisha vilabuni kwa muda
unaotakiwa.
Wengine walioshindwa kufika ni Edward Charles na Hassan Masapili ambao hati zao za kusafiri hazikuwa zimekamilika. Viwango
Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.
BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment