STRIKA
USILIKOSE
Friday, May 27, 2016
Kijana anusurika kufa kwa kujirusha kutoka mnara wa simu
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Tukio hilo
limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo
ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia
mnarani hadi majira ya saa sita mchana.
Mashuhuda wa tukio
hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda
kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao
amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na
matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.
Akizungumza kwa
niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja
wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye
minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari
inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana
huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa
ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati
ya mnara huo.
Baada ya kijana
huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na
kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa
ajili ya huduma ya kwanza.
Credit:Mwanaharakati Mzalendo
Fomu za Uchaguzi Yanga zadoda Karume
Manji (kati)n akitetea na Cannavaro na Chuji misimu kadhaa ya nyuma ya Ligi Kuu Bara |
Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitangaza leo Ijumaa ndio siku ya kufunguliwa kwa zoezi hilo, lakini mpaka jioni hii hakuna aliyejitokeza, huku kukiwa na taarifa kwamba Yanga wameugomea uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alloyce Komba amedokeza kuwa, hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu, lakini akiamini muda bado kwani wana siku 5 za zoezi hilo kufikia tamati.
Hata hivyo MICHARAZO imenasa taarifa kuwa, uchaguzi huo umesuswa na wana Yanga baada ya kutaka usifanyike kipindi hiki ambacho klabu yao itakuwa kwenye pilikapilika za kuelekea kwenye mechi zao za kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Yanga imepangwa Kundi A na timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya DR Congo na Medeama ya Ghana na itaanza mechi zao siku mbili kabla ya kuvaana na Bejaia mjini Algiers, Algeria.
Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Juni 15, lakini uongozi wa klabu hiyo ukitaka ufanyike tarehe moja na uchaguzi wao mdogo uliofanyika Julai 15, 2012 na kumuingiza Mwenyekiti na tajiri wao, Yusuf Manji.
Ronaldo kwa vijembe hajambo, awakejeli Barcelona kimtindo
HEBU msikieni CR7. Straika nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa na thamani kubwa zaidi kuliko mataji mawili yaliyonyakuliwa na wapinzani wao, Barcelona msimu huu.
Ronaldo aliye na umri wa miaka 31 aliyekuwa majeruhi katika wiki za karibuni na kumfanya akose mechi ya nusu fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City ni kama amewapiga kijembe wapinzani wao hao.
Hata hivyo juzi aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa atakuwa fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya fainali hiyo dhidi ya Atletico Madrid.
Akihojiwa Ronaldo amesema kama wakishinda taji hillo la Ligi ya Mabingwa itakuwa ni thamani kubwa zaidi kwao kuliko mataji mawili ya Barcelona waliyoshinda hivi karibuni, kwani taji la michuano hiyo ya Ulaya liko katika ndoto za kila mchezaji. Klabu hasimu za jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid zitakutana kesho Jumamosi katika fainali ya tatu zilizozikutanisha timu za Hispania na mechi ya fainali ya pili baina yao baada ya mwaka juzi 2014 kukutana na Real kushinda 4-1.

Kaka akumbukwa Brazil, aitwa kuziba pengo la Costa
Kaka akiwajibika kwa klabu yake ya Orlando |
Costa mwenye umri wa miaka 25, amepata majeraha ya misuli ambayo yatamfanya akose michuano hiyo maalumu ya kuadhimisha miaka 100 toka kuanzishwa kwake. Kaka mwenye umri wa miaka 34 ameichezea Brazil mechi 91 na kufunga mabao 29 katika kikosi hicho.
Costa alikuwa sehemu ya kikosi cha Bayern Munich ambacho kimeshinda taji la Bundesliga na Kombe la Ujerumani katika msimu wa mwisho wa Pep Guardiola na timu hiyo.
Brazil imepangwa kufungua pazia la Copa America kwa kucheza na Ecuador katika Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena, California Juni 4 mwaka huu, huku mechi zao nyingine mbili za kundi B zitakuwa dhidi ya Haiti na Peru.
Yanga yaibania Simba kucheza kimataifa
Yanga |
Simba |
Simba ilikuwa ikijipa matumaini ya kuwemo kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika kuanzia mwezi ujao nchini, lakini michuano hiyo sasa haitafanyika tena Tanzania baada ya TFF kuchomoa kuiandaa.
Shirikisho hilo la Soka Tanzana, limetangaza kutoandaa michuano hiyo inayohusisha timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa.
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagame.
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya.
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga.
Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.
Watetezi wa taji hilo ni Azam na tayari Yanga ilikuwa ikisita kushiriki na kutoa nafasi kubwa kwa Simba kubeba jukumu, lakini kwa hali ilivyo watabidi wasubiri sana.
Dani Alves ainyima ubingwa Real Madrid Ulaya
Dani Alves |
Atletico Madrid |
Atletico na Madrid zitavaana kesho, katika mechi ya kisasi kwea kocha Diego Simeone ambaye alifungwa kwenye fainali ya mwaka juzi na mabingwa hao wa kihistoria wa michuano hiyo ya Ulaya kwa mabao 4-1.
Atletico walio chini Diego Simeone ndio waliowang’oa mabingwa watetezi Barcelona katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kabla ya kuitoa tena Bayern Munich kwenye hatua ya nusu fainali.
Madrid ndio timu pekee iliyopo mbele ya Atletico kwasasa ikiwa ni kama marudiano baada ya ile fainali ya mwaka 2014 ambapo Madrid waliibuka kidedea kwa kushinda mabao 4-1 katika muda wa nyongeza.
Hata hivyo, Alves ana mawazo tofauti katika fainali hiyo itakayofanyika katika Uwanja wa San Siro jijini Milan nchini Italia kwani anadhani Atletico wanastahili zaidi taji hilo kuliko Madrid. Alves amesema Atletico ni timu ambayo imepambana sana mpaka kufikia hapo walipo hivyo anadhani wanastahili taji hilo
Juventus kumng'oa Mascherano Nou Camp
MABINGWA wa Italia, Juventus imepanga kumng'oa Kiungo mahiri wa Barcelona, Javier Mascherano.
Inadaiwa kuwa Muargentina huyo amekubali dili la kujiunga na mabingwa wa Serie A.
Duru za kimichezo zinasema kuwa, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amefanya mazungumzo na Juventus na anajiandaa kuhamia jijini Turin kiangazi hiki.
Mpaka sasa inadaiwa kuwa hakuna makubaliano yoyote kati ya Barcelona na Juventus na mabingwa hao wa Hispania wanahisiwa kutokuwa na mpango wowote wa kumuachia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.
Mascherano alijiunga na Barcelona mwaka 2010 akitokea Liverpool na kufanikiwa kushinda mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Camp Nou.

Ufaransa yaapa fainali za Euro 2016
UTAWALA wa nchi ya Ufaransa umesema kuwa inatarajia kuweka polisi zaidi ya 60,000 ili kulinda usalama katika michuano ya Euro 2016 itakayopanza Juni 10 wakiapa kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanazuia shambulio lolote la kigaidi katika kipindi chote cha mashindano hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, Bernard Cazeneuve ndiye aliyetoa kauli hiyo baada ya Uwanja wa Ufaransa uliopo jijini Paris ambao ndio utatumika kwa ajili ya mechi ya ufunguzi na fainali, kuleta rabsha Jumamosi iliyopita kabla ya fainali ya Kombe la Taifa.
Moshi mkubwa uliohisiwa kuwa bomu ulilipuka ndani ya uwanja na kusababisha mashabiki kuchanganyikiwa na kukimbia hovyo kuelekea milango ya kutoka nje ya uwanja.
Akihojiwa Waziri huyo amesema tukio la Jumamosi iliyopita halihusiani na maandalizi yao kwani waandaaji walikuwa tofauti.
Waziri huyo aliongeza kuwa katika michuano ya Euro 2016 inayotarajiwa usalama utakuwa ni kipaumbele chao cha kwanza ili kuhakikisha hakuna tukio lolote hatarishi ya kigaidi litakaloweza kutokea.

Jose Mourinho atambulishwa rasmi Man United
Jose Mourinho akitua rasmi Man United |
Mourinho, mwenye miaka 53 ametangazwa na klabuni na kuchapishwa picha akiwa na jezi za klabu yake mpya ambayo ilikuwa ikimsaka tangu alipotemwa Chelsea katikati ya msimu uliomalizika wa EPL.
Kocha huyo alisaini mkataba huo jana jioni baada ya mazungumzo ya siku tatu kabla ya kutambulishwa akiwa kavalia suti kali nyeusi jambo linaloashiria kuwa, Special One sasa ni mali ya Mashetani Wekundu na wapinzani wao wajipange kwa mikakati anayokuja nayo kocha huyo mjuzi.
Moja ya mikakati inayotajwa kuwa mikononi mwa Mourinho ni kumnyakua Willian anayekipiga Chelsea ambaye alinunuliwa na kocha huyo wakati akiinoa klabu hiyo ya The Blues.
Subscribe to:
Posts (Atom)