Gareth Bale akiwajibika dimbani |
Hata hivyo huenda Tottenham inayowania kumaliza kwenye Nne Bora na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani itakali nafasi hiyo kwa muda kwani mpaka sasa Arsenal iliyopo ugenini inaongoza kwa bao 1-0.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jioni na kumalizika waliokuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Manchester City imelazimishwa suluhu ugenini na Swansea City, huku Reading iliyokwisha kushuka daraja ikimaliza hasira kwa Fulham kwa kuikandika nyumbani kwao mabao 4-2.
Nao vijana wa Paul Lambert , Aston Villa waliendelea kupigana kuepuka kushuka daraja kwa kupata ushindi ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Norwich City, huku West Ham ikiwa nyumbani ililazimishwa suluhu na Newcastle United na Wigan Athletic ikiitambia West Bromwich Albion ikiwa kwao kwa mabao 3-2.
Kitimtim cha ligi hiyo kinatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mechi inasubiriwa kwa hamu kati ya Mabingwa wa ligi hiyo, Manchester United itawakaribisha Chelsea uwanja wa Old Traffod huku wapinzani wa jadi Liverpool na Everton zitapepetana kwenye uwanja wa Anfield.