Vialli (kati) na Sure Boy wakijifua kuwakabilia AS FAR Rabat
Kikosi cha Azam kinachotarajiwa kuwatoa kimasomaso Watanzania leo nchini Morocco.
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Azam jioni hii wanatarajiwa kushuka dimbani nchini Morocco kupepetana na wenyeji wao, AS FAR Rabat katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam ambayo ipo nchini humo karibu wiki nzima sasa katika mbinu za kuzoea mazingira ya kuwakabili wapinzani wao, inahitaji sare ya aina yoyote ya magoli kuweza kufuzu hatua ya 16 Bora.
Katika pambano la kwanza lililochezwa nchini Tanzania wiki mbili zilizopita, Azam walilazimishwa suluhu na maafande hao wa jeshi la Morocco licha ya kosakosa za hapa na pale katika mchezo huo.
Azam ina matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi ugenini katika pambano hilo kwa kile kinachoelezwa ari waliyonayo wachezaji na maandalizi waliyoyafanya mpaka sasa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Morocco mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 11:00 jioni kwa saa za Morocco sawa na saa 1 usiku kwa hapa Tanzania na tayari silaha za 'maangamizi' za Azam zimeshaanikwa tayari ya kufanya 'maafa' ugenini.
Kikosi kitakachoanza pambano hilo ambalo litatangazwa na kituo cha runinga cha Clouds na RFA Masafa ya Kati na Kiss FM ni kama kifuatavyo;
1. Mwadini
2. Himidi Mao
3. Waziri Seif
4. David Mwantika
5. Atudo
6. Bolou
7. Umony
8. Salum 'sure boy'
9. Bocco (C)
10. Mieno
11. Kipre
Akiba
Aishi
Ibrahim Mwaipopo
Gaudence Mwaikimba
Abdi Kassim 'Babi'
Mcha Khamis 'Vialli'
Jabir Aziz Stima
Luckson Kakolaki
Mungu Ibariki Azam Mungu Ibariki Tanzania
Vialli (kati) na Sure Boy wakijifua kuwakabilia AS FAR Rabat |
Kikosi cha Azam kinachotarajiwa kuwatoa kimasomaso Watanzania leo nchini Morocco. |

No comments:
Post a Comment