STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 6, 2014

Hatari! Njemba yanaswa na Dawa za Kulevya,


unnamed
Mtuhumiwa Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa aliyekamatwa eneo la Mianzini jijini Arusha akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi iliyokuwa inasafirishwa toka nchi jirani ya Kenya kuelekea Kondoa mkoani Dodoma (Picha:Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
MTU mmoja aitwaye Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma, amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina yake.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni eneo la Mianzini ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo kwenye gari aina ya Fusso basi lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo aliihifadhi kwenye magunia mawili huku juu na pembeni ya magunia hayo akiweka viatu.
‘’Katika magunia yale alikuwa ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya madawa hayo aina ya mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini Kenya kupeleka Kondoa mkoani Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni viatu pekee’’. Alifafanua Kamanda Sabas.
Alisema tukio hilo lilifanikiwa kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya Jeshi hilo na raia wema ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka na asakari wa Jeshi hilo.
Baada ya askari hao kupata taarifa hiyo walianza kulifuatilia gari hilo na lilipofika maeneo ya Mianzini jijini hapa kwenye maegesho ya basi hilo ndipo walipoanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata magunia hayo yaliyokuwa na viatu vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda Sabas alisema kwamba mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Newz Alert! Rais JK aenda USA kucheki afya yake

  
Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe said Meck Sadik na Meneja wa Huduma za Shirika la ndege la Emirates katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere Bw.  Aboubakar Juma leo Novemba 6, 2014 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya leo, Alhamisi Novemba 6, 2014, kwenda Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Rais Kikwete atakuwa Marekeni kwa muda wa siku kumi.

Mwisho.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
06 Novemba,2014

Watatu kati ya waliokufa ajalini Ifakara watambuliwa!

http://api.ning.com/files/st-pA-4csCGQ4-t4jx12MikAxzFvyvUW-zC35WxKpbGhYiXhPqU4H5di0w8j4TwMDjoHYFJKlkEAnto0riRQW1TncFQ-7kLz/5ajali5.jpg
Mabaki ya basi la Al Jabir (Picha zote na Global Publishers)
 

Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
Basi hilo likiwa limepinduka.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
MIILI ya watu watatu kati ya 12 waliofariki katika ajali mbaya ya gari dhidi ya treni huko Ifaraka mchana wa leo imetambuliwa.
Watu hao walifariki dunia papo hapo na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi walililokuwa wakisafiria la Kampuni ya Al Jabir kugonga treni eneo la Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.
 Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema basi hilo lilokuwa likitokea Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya – jijini Dar es Salaam.
 Kamanda huyo  aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda Paulo alisema chanzo cha ajali hiyo ni  dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na reli bila ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.
Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mtakatifu Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Paulo alisema miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu Francis Ifakara.
Alisema dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

Ndege ya Rais wa China yadaiwa kutorosha nyara za Tanzania


Rais Xi JinPing wa Uchina alipozuru Tanzania mwaka uliopitaINADAIWA kuwa, Ndege ya Rais wa China, aliyekuwa ziarani nchini Tanzania mwaka uliopita ilihusija kutorosha nyara za taifa zikiwamo Pembe za Ndovu.
Inaelezwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za Pembe za Ndovu Tanzania kisha kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping, wakati alipozuru bara Afrika. 
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London. 
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini Tanzania mwaka uliopita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa. 
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu. 
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Hata hivyo serikali imekanusha taarifa hizo za kuwepo kwa biashara ya Pembe za Ndovu nchini.
Msemaji wa serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Mwambene amesema serikali ya Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China.
Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo.
BBC  

TANGAZO KWA WANABLOGU WOTE TANZANIA

RAIS JK APANGUA WAKUU WA MIKOA, KANALI MASSAWE NJE!

http://api.ning.com/files/Hu6bOG3IkcRAJl9pt5BZONEg5d6srRLFuULjOo7Y1CbfmS7EUBSjP7yla0ZaLravxPaTvFQrk**5S7QDlPeW7XvoWqo9qwB9/RaisKikwete.jpg
Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na
Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi. Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Mwisho.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

Simanzi! Ajali yachinja watu 12 Ifakara

http://rantsofasassystew.com/wp-content/uploads/2011/10/Breaking_News.jpg
HABARI zilizotufiki hivi punde zinasema kuwa kumetokea ajali mbaya iliyohusisha basi la Al Jabir ambalo lililigonga Treni na kusababisha vifo vya watu 12 papo hapo wakiwamo watoto wawili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Morogoro ni kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 katika eneo la Kiberege, Ifaraka wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Taarifa hizo zinasema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 725 ATD liliigonga Treni ya TAZARA na kusababisha roho za wanaume sita, wanawake wanne na watoto wawili waliokuwa kwenye basi hilo kupotea huku abiria wengine kuachwa na majeraha ya kutisha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul amethibitisha taarifa hiyo na uchunguzi dhidi ya ajali hiyo unaendelea kujua chanzo chake.

FifPro yatishia kugomea Fainali za Kombe la Dunia za Qatar

http://s1.reutersmedia.net/resources/r/?m=02&d=20110914&t=2&i=500889270&w=580&fh=&fw=&ll=&pl=&r=img-2011-09-14T173158Z_01_NOOTR_RTRMDNC_0_India-593363-1
UMOJA wa Wachezaji wa Kulipwa FIFPro, umetishia kuigomea michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022 nchini Qatar.
Kiongozi wa umoja huo, Theo van Seggelen amesema kuwa wachezaji wanaweza kugomea kushiriki michuano hiyo iwapo itaendelea kushinikizwa kuchezwa katika majira ya kiangazi.
Joto katika nchi hiyo ya barani Asia hufikia hadi nyuzi joto 40 katika kipindi cha kati ya mwezi Mei na Septemba, ingawa muda haswa wa kufanyika michuano hiyo bado haujapangwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA.
Van Seggelen amesema Fifpro haitawaruhusu wachezaji kuhatarisha afya zao kwa kushiriki fainali hizo ambazo zimeleta mzozo tangu zilipotangazwa na shirikisho la sokla duniani, FIFA miakla michache iliyopita.
Aliongeza kwa kudai kuwa kama ikibidi anaweza kulipeleka suala hilo mahakamani ili kupata haki ya msingi.
Kiongozi huo amesema ana uhakika FIFA haitaweza kupingana na washauri wao wenyewe wa masuala ya afya kwa kuruhusu michuano hiyo kuchezwa majira ya kiangazi.
Van Seggelen pia aliponda ombi la vilabu vya Ulaya kutaka michuano hiyo kufanyika katika kipindi cha Aprili na Mei akidai kuwa halina mashiko kwani bado kipindi hicho kinaweza kuhatarisha afya za wachezaji.

Polisi wanasa Konyagi Feki Dar, wahusika watiwa mbaroni


BAADHI ya vibarua waliokodiwa kwa ajili ya kupakia Konyagi ili wapeleke kituo cha polisi Buguruni wakifanya kazi ya kujaza katika marobota ili waweke katika gari baada ya konyagi hiyo feki kukamatwa Dar es salaam jana kwenye moja ya Godown maeneo ya vingunguti karibu na kituo cha mchicha watuhumiwa walikamatwa na kupelekwa polisi
Baadhi ya watuhumiwa wa Konyagi feki wakifanya kazi ya  kupakia kwenye mabox konyagi hizo ambapo walikamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa kituo cha polisi buguruni kwa uchunguzi zaidi

Baadhi ya watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi ambapo jana waliswekwa lumande na kulala ndani ya kituo cha polisi buguruni baada ya kukamatwa wakipakia Konyagi feki maeneo ya vingunguti Dar es salaam jana
MMOJA YA WATUHUMIWA AMBAYE ALIJITAMBULISHA KUWA YEYE NI MMILIKI WA KONYAGI FEKI AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA JANA

Baadhi ya watumiwa waliokutwa katika godown lenye konyagi feki wakiendelea na kazi ya kupakia katika mabox watumiwa hawo walikamatwa na kulala lumande katika kituo cha polisi Buguruni Dar es salaam jana kwa uchunguzi zaidi
Baadhi ya maofisa usalama wakiangalia mzigo uliokamatwa ukipandishwa katika gari kwa ajili ya kuelekea kituo cha polisi buguruni


Baadhi ya vibarua waliokodiwa kwa ajili ya kupakia Konyagi ili wapeleke kituo cha polisi Buguruni wakifanya kazi ya kujaza katikaq marobota ili waweke katika gari baada ya konyagi hiyo feki kukamatwa Dar es salaam jana kwenye moja ya Godown maeneo ya vingunguti karibu na kituo cha mchicha watuhumiwa walikamatwa na kupelekwa polisi

Man City Majanga, Chelsea yabanwa Ulaya, Bayern haoooo!

Eden Hazard missed the chance to win the match for Chelsea against Maribor late on when his penalty was saved
Hazard akipiga penati iliyookolewa wakati Chelsea wakitoka sare ya 1-1
Seydou Doumbia heads CSKA Moscow into an early lead as he takes advantage of a static Manchester City defence
Man City wakiadhibiwa na Doumbia
Toure jumps for joy as he celebrates levelling the score in what was a crunch match for City in the Champions League
Yaya Toure akishangilia bao lake jana
City's miserable night, and their campaign, was summed up by Toure's red card as he followed Fernandinho to the dressing room
Kisha akaja akalimwa kadi nyekundu ya kwamba maisha yake Etihad
Gotze is mobbed by his Bayern team-mates after doubling the Germans' lead late in the second half
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia mabao yao yaliyowapeleka kwenye 16 Bora ya Ulaya
Ribery celebrates opening the scoring after Bayern had dominated possession in the first half
Fracky Ribery akishangilia bao la kwanza la Bavarians
WAKATI mabingwa watetezi wa England Manchester City wakigaragazwa nyumbani na kujiweka katika nafasi finyu ya kufuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya mabingwa, Chelsea wameponea chupuchupu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Maribor walioitandika vibaya wiki iliyopita.
Cheslea katika mechi ya Kungi G ilishtukizwa kwa bao lililofungwa dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya Agim Ibraimi kuifungia Maribor, kabla ya Nemanja Matic kusawazisha katika dakika ya 73.
Wakiwa na nafasi ya kuendeleza rekodi ya kipigo cha Maribor, Chelsea walipoteza penati baada ya mshambuliaji Eden Hazard kushindwa kukwamisha mpira wavuni.
Hata hivyo matokoe hayo bado yameiacha Chelsea kileleni mwa msimamo wa kundi hilo wakiwa na pointi nane wakifuatiwa na Schalke 04 iliyolala ugenini kwa mabao 4-2 mbele ya Sporting yenye pointi tano.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, Manchester City walijikuta wakijiweka pabaya kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya CSKA Moscow, huku ikiwapoteza nyota wake wawili, akiwamo Yaya Toure aliyefunga bao pekee la timu hiyo.
Yaya alilimwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na nyekundu na kuwa kadi yake ya kwanza tangu aanze kuichezea timu hiyo na tayari amewaomba radhi mashabiki wa klabu hioyo ya Etihad.
CSKA Moscow waliwashtukiza wenyeji kwa bao la mapema la dakika ya pili kupitia Seydou Doumbia akimalizia kati ya Natcho kabla ya Yaya Toure kusawazisha dakika sita baadaye ma Doumbia akamaliza udhia dakika ya 34 kwa kufunga bao la pili na katika kipindi cha pili wenyeji kuwapoteza Yaya na Fernandinho.
Kipigo hicho kimeiacha City wakiwa wanaburuza mkia wakiwa na pointi mbili wakitakiwa kupata ushindi mfululizo dhidi ya  Bayern Munich waliofuzu baada ya kuilaza Roma kwa mabao 2-0 na ile dhidi ya Roma wenyewe ambao wanashika nafasi ya pili wakilingana pointi na CSKA.
Katika mechi nyingine Porto ya Ureno ikiwa ugenini nchini Hispania ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Athletico Bilbao, huku Shakhtar Donetsk ya Uturuki wakiichakaza BATE kwa mabao 5-0 katika mechi za kundi H.

Messi achana naye, aitungua Ajax 2-0 na kumfikia Raul


Lionel Messi celebrates scoring his first goal against Ajax on Wednesday night
Messi akishangilia moja ya mabao yake yaliyomfanya amfikie raul
Messi heads into the Ajax goal for his 70th Champions League goal... he later scored his 71st
Messi akifunga  bao dhidi ya Ajax
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi usiku wa jana ameweka relodi ya kumfikia kinara wa mabao wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa, Rau baada ya kufunga mabao mawili wakati barcelona wakiilipua Ajax kwa mabao 2-0.
Messi amefikisha jumla ya mabao 71 na kulingana na Raul aliyewahi kutamba Real Madrid.
Mwanasoka Bora huyo wa mara nne wa zamani wa dunia alifunga mabo la kwanza kwa kichwa kabla ya kuongeza jingine na kufikia rekodi hiyo iliyowekwa miaka 10 iliyopita na Raul.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kukamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 9, moja ya vinara wa kundi F PSG ambayo ilishinda nyumbani 1-0 dhidi ya APOEL Nicosia na kulifanya kundi hilo kuzidi kuwa gumu bila kujua itakayofuzu hatua ya 16 Bora hadi michezo ijayo.

Ronaldo atamba yeye ni mkali bwanaa!

http://www.footballlive.ng/football/wp-content/uploads/2014/10/cr7goldenshoe.jpg
Ronaldo
CRISTIANO Ronaldo, Mwanasoka Bora Duniani, anaamini atajumuishwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mchezo huo wakati utakapofikia wakati wake wa kustaafu.
Nyota huyo wa Real Madrid na raia wa Ureno, 29 alipokea tuzo yake ya Kiatu cha Dhahabu cha Mfungaji Bora Barani Ulaya ikiwa ni mara ya tatu kwake jana huku pia akipewa nafasi ya kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tatu Januari mwaka huu.
Wakati akisisitiza kuwa bado ana miaka mingi ya kucheza soka katika kiwango cha juu, nyota alisema ana uhakika nafasi yake kama mmoja wa manguli wa soka katika historia tayari ameshajihakikishia.
Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake hiyo Ronaldo amesema siku zote anataka kuwa bora ndio maana anafanya jitihada kila kukicha.
Msimu huu Ronaldo bado ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga akiwa tayari ameshafunga mabao 22 katika mechi 16 za mashindano yote na kuiwezesha Madrid kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga sambamba na kutinga hatua ya timu 16 bora.
Ronaldo alifungana mabao na Luis Suarez ambaye tyayari alishakabidhiwa tuzo yake hivi karibuni. kila mmoja alifunga mabao 31 katika ligi maarufu Suarez akiwa Liverpool japo kwa sasa amehamia Barcelona.
Make money by copying the best: http://bit.ly/cop
MCHEZAJI bora wa mwaka wa dunia, Cristiano Ronaldo anaamini atajumuishwa kama mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mchezo huo wakati utakapofikia wakati wake wa kustaafu. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alipokea tuzo yake ya kiatu cha dhahabu ikiwa ni mara ya tatu kwa kuwa mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya jana huku pia akipewa nafasi ya kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tatu Januari mwaka huu. Wakati akisisitiza kuwa bado ana miaka mingi ya kucheza soka katika kiwango cha juu, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ana uhakika nafasi yake kama mmoja wa manguli wa soka katika historia tayari ameshajihakikishia. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake hiyo Ronaldo amesema siku zote anataka kuwa bora ndio maana anafanya jitihada kila kukicha. Msimu huu Ronaldo bado ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga akiwa tayari ameshafunga mabao 22 katika mechi 16 za mashindano yote na kuiwezesha Madrid kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga sambamba na kutinga hatua ya timu 16 bora.

Make money by copying the best: http://bit.ly/copy_win

Wape Salam kuzinduliwa J2, Jahazi, King Majuto kunogesha

Kava la filamu ya Wape Salam
Bango la onyesho hilo la Jumapili
Ujio mpya wa Ulimwengu wa Filamu ndanio ya TBC1, Kibirigi a.k.a Kisate ndani

KUNDI la muziki wa taarab la Jahazi Modern linatarajiwa kupamba uzinduzi wa filamu mpya iitwayo 'Wape Salamu Zao' utakaoenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya kipindi cha Ulimwengu wa Filamu cha kituo cha TBC1.
Kwa mujibu wa mmoja wa waratibu na mshiriki wa filamu hiyo, Jackson Kibirigi 'Kisate' uzinduzi huo utafanyika kwenye ukumbi wa Travertine Magomeni na Jahazi wataangusha burudani kusindikiza tukio hilo.
Kisate alisema amepanga kufanya uzinduzi wa aina yake ambao haujawahi kufanywa katika uzinduzi wowote wa filamu nchini.
“Nimepanga kuacha historia katika uzinduzi wa filamu ya 'Wape Salamu Zao'. Kuna vitu vingi ambavyo sijawahi kuwaonyesha watazamaji kupiotia kazi zangu za nyuma hivyo mashabiki watarajie makubwa Jumapili," alisema Kisate.
Kisate alisema uzinduzi huo utasindikizwa na Jahazi chini ya Mzee Yusuf ambaye ameahidi pia kutoa burudani ya aina yake pamoja na King Majuto na wasanii mbalimbali wa Bongo Movie na watu wengine maarufu watapata fursa ya kupiga picha kwenye zulia jekundu.
Muigizaji huyo alisema kwa ndani ya filamu hiyo wamecheza Fatuma Makongoro, Jackson Kibirigi, Dennis David, Khadija Jarufu na wengine ambao waliitendea haki.