Mabaki ya basi la Al Jabir (Picha zote na Global Publishers) |
Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
Basi hilo likiwa limepinduka.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
MIILI ya watu watatu kati ya 12
waliofariki katika ajali mbaya ya gari dhidi ya treni huko Ifaraka mchana wa leo imetambuliwa.
Watu hao walifariki dunia papo hapo na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi
walililokuwa wakisafiria la Kampuni ya Al Jabir kugonga treni eneo la
Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.
Kamanda
wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema basi hilo lilokuwa likitokea
Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya –
jijini Dar es Salaam.
Kamanda
huyo aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni
Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde
Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Paulo alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo lenye namba
za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na reli bila
ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.
Alisema
kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mtakatifu
Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Paulo alisema miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu Francis Ifakara.
Alisema
dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi
wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment