STRIKA
USILIKOSE
Sunday, September 15, 2013
Balotelli aiokoa Milan na kipigo cha ugenini
Mario Balotelli akishangilia bao |
STRAIKA Mario Balotelli jana aliiokoa timu yake ya AC Milan isiaibike ugenini baada ya kufunga bao dakika za nyongeza na kuipa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Torino katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Italia Seria A.
Balotelli aliyetoka kuipeleka nchi yake kwenye michuano ya Fainali za Kombe la Dunia za mwakani, alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 90+6 na kuiepushia aibu Milan walioonekana kulala 2-1.
Kabla ya hapo Milan ilijipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Sulley Muntari baada ya wenyeji kutangulia kupata mabao mawili yaliyofungwa na D'Ambrosio na Cerci.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo mabingwa watetezi, Juventus wakiwa ugenini mjini Milan dhidi yasa Inter Milan waliambulia sare ya bao 1-1, huku Napoli ikipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Atalanta, huku Fiorentina nayo ikilazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Cagliari.
Gareth Bale aanza na bao Real Madrid ikipata sare ugenini la liga
NYOTA mpya wa Real Madrid na mchezaji ghali kuliko wote duniani, winga Gareth Bale usiku wa kuamkia leo alianza makeke yake katika klabu yake kwa kuifungia moja ya mabao yaliyoisaidia vinara hao wa Hispania wasiumbuke ugenini walipotoka sare ya 2-2 na Villareal.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na alionyesha uwezo mkubwa, akifunga bao hilo la kusawazisha baada ya wenyeji kuwatangulia Madrid kwa bao la Cani na kufanya hadi mapumziko timu hizo ziwe nguvu sawa ya bao 1-1.
Kipindi cha pili Cristiano Ronaldo aliiongezea Madrid bao ambalo hata hivuo lilikuja kurejeshwa na wenyeji kupitia kwa Giovani Dos Santos.
Katika mechi iliyochezwa mapema leo, Espanol ikiwa ugenini imeizabua Granada kwa bao 1-0 lilitupiwa kambani na Lanzarote.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa jana katika ligi hiyo maarufu kama La Liga, mabingwa watetezi Barcelona ikiwa nyumbani ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Sevilla, shukrani ya mabao ya Dani Alves ,
Lionel Messi na Alexis Sanchez.
Wageni mabao yao yalitupiwa kimiani na Coke na Ivan Rakitic. Nao Atletico Madrid walipata ushindi wao wa nne mfululizo kwa kuwalaza Almeria mabao 4-2 na kuwaweka kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakati Levante walilazimishwa suluhu na Real Sociaded.
Warembo wa Miss Tanzania waitembelea DTL
NA MWANDISHI WETU
WAREMBO wanaowania taji la Miss Tanzania wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa
Kiwanda cha Tanzania Distilleries (KONYAGI) Bw. David Mgwassa wakati
akiongea na Warembo 30 wanaowani taji la Miss Tanzania walipotembelea
kiwanda hicho jijini Dar es salaam.
"Nyinyi
ni mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa za humu ndani hivyo nawaomba
sana mzipende na kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda
vya ndani" alisema Bw. Mgwassa.
Amesema
kuwa TDL kupitia kinywaji cha Zanzi imeamua kudhamini shindano la Miss
Tanzania kwa kiasi cha Milioni 40 ikiwa na lengo la kutangaza kinywaji
hicho na pia kuboresha shindano hilo.
Kwa
mujibu wa Bw. Mgwassa shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa
taifa hili na kuwataka warembo hao kutangaza milima kilimanjaro na pia
kuitangaza Zanzi kuwa ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua
uchumi wa nchi.
"Nyinyi
warembo naombeni sana Zanzi iwe kwenye mawazo yenu kila siku na
muitangaze Zanzi baada ya mlima kilimanjaro kwa kufanya hivyo basi
uchumi wa nchiu pia utakua mzuri zaidi." alisema
Kwa
upande wake meneja masoko wa TDL, Bw. Vimal Vaghmaria aliwataka warembo
hao kuwa na nidhamu kubwa wanapokuwa kambini kwa lengo la kupata mrembo
mwenye viwango vya juu na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
kimataifa.
"Sisi
kama TDL kupitia kinywaji cha Zanzi tumemua kudhamini shindano hili la
Miss Tanzania tukiamini kuwa nyinyi ni mabalozi wazuri wa kuitangaza
kinywaji hichi na kuiletea sifa Tanzania" alisema Bw. Vaghmaria.
Katika
ziara hiyo warembo walipata nafasi ya kujione shughuli mbalimbali za
kiwanda hicho kuanzia mwanzo wa vinywaji vinapozalishwa hadi kwenye
sehemu ya mwisho ya upakiaji.
JKT Ruvu hawakamatiki, Kavumbangu, Maguri, Kipanga wawanasa akina Tegete, Mkude katika magoli
Didier Kavumbagu |
Ruvu inayonolewa na kipa wa zamani wa Tukuyu Stars na Yanga, Mbwana Makatta, iliitafuta Ashanti United jana kwa bao la Amos Mgisa na kuifanya ifikishe pointi 9 na magoli sita ya kufungwa huku yenyewe ikiwa na ukuta wa chuma kwa kutoruhusu kufungwa bao lolote.
Kikosi cha JKT Ruvu |
Bao pekee lililofungwa na Elius Maguri lilitosha kuifanya maafande hao kufikisha pointi sita, huku mfungaji huyo akiingia kwenye orodha ya wafungaji watano wanaoongoza kwa sasa katika ligi hiyo kila mmoja akiwa na mabao mawili.
Maguri aliyesajiliwa na Ruvu Shooting toka Prisons ameungana na akina Jerry Tegete na Didier Kavumbagu wa Yanga, Jonas Mkude wa Simba, Saad Kipanga aliyeanza kuonyesha makeke licha ya ugeni wake katika ligi hiyo naye akiwa na mabao mawili baada ya jana kuisaidia timu yake ya Rhino kupata sare dhidi ya Olojoro JKT jijini Arusha.
Mchezaji mwingine aliye katika orodha hiyo ya wafungaji bora kwa sasa wakati ligi ikiwa ndiyo kwanza ipo raundi ya tatu ni Bakar Kombo wa JKT Ruvu.
Wakati Prisons ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafanikiwa kufunga bao lolote mpaka sasa angalau wenyewe wameambulia pointi jana jijini Tanga mbele ya Coastal, kuliko Ashanti United ambayo licha ya kuwa na goli moja, lakini haijaonja furaha ya kumiliki pointi baada ya kupoteza mechi zake zote tatu.
Ilianza kwa kufungwa na Yanga mabao 5-1 kabla ya kunyolewa bao 1-0 katika mechi zilizofuata dhidi ya Mgambo na jana JKT Ruvu na kuwa ndiyo inayoburuza mkia ikizibeba timu zote za ligi hiyo yenye klabu 14.
Ashanti ni kati ya timu tatu zilizopanda daraja msimu huu sambamba na Rhino Rangers iliyokusanya pointi mbili mpaka sasa katika mechi zake tatu na Mbeya City iliyokaribia kuiadhiri mabingwa watetezi Yanga jana kwenye mechi yao ilioisha kwa sare ya 1-1 yenyewe ikiwa na pointi tano sambamba na klabu nyingine wakiwamo Yanga, Coastal Union na Azam.
Msimamo kamili wa ligi hiyo baada ya mechi ya jana ni kama ifuatavyo na wafungaji na ratiba ya mechi zijazo utachungulia hapo chini:
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
1. JKT Ruvu 3 3 0 0 6 0 6 9
2. Simba 3 2 1 0 5 2 3 7
3. Ruvu Shooting 3 2 0 1 5 2 3 6
4. Yanga 3 1 2 0 7 3 4 5
5. Azam 3 1 2 0 4 2 2 5
6. Coastal Union 3 1 2 0 3 1 2 5
7. Mbeya City 3 1 2 0 3 2 1 5
8. Mtibwa Sugar 3 1 1 1 2 3 -1 4
9. Mgambo 3 1 0 2 1 3 -2 3
10. Rhino Rangers 3 0 2 1 3 5 -2 2
11. Kagera Sugar 3 0 2 1 1 2 -1 2
12. Oljoro 3 0 1 2 1 4 -3 1
13. Prisons 3 0 1 2 0 6 -6 1
14. Ashanti 3 0 0 3 1 7 -6 0
Wafungaji:
2- Jerry Tegete, Didier Kavumbangu (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla, Jerry Santo (Coastal Union), Haruna Chanongo, Henry Joseph, Betram Mombeki (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva (Yanga), Iman Joel (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris (Azam), Mwagani Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Ayoub Kitala, Jerome Lembeli (Ruvu Shooting), Juma Luzio, Masoud Ally (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Salum Machaku, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga (Mgambo JKT), Themi Felix (Kagera Sugar), Amir Omary (Oljoro JKT)
Mechi zinazofuata siku ya Jumatano
Sept 18, 2013Prisons vs Yanga
Simba vs Mgambo JKT
Kagera Sugar vs JKT Oljoro
Azam vs Ashanti United
Coastal Union vs Rhino Rangers
Mtibwa Sugar vs Mbeya City
Ruvu Shooting vs JKT Ruvu
Mjini Magharib mabingwa wa Copa Coca Cola
MJINI
Magharibi imetwaa ubingwa wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 15 upande wa wavulana baada ya jana (Septemba
14 mwaka huu) kuifunga Ilala bao 1-0.
Mechi
hiyo ya fainali ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es
Salaam. Ilala iliwavua ubingwa Morogoro baada ya kuwafunga kwenye mechi
ya nusu fainali kwa kuivua ubingwa Morogoro katika mechi iliyoamriwa kwa
mikwaju ya penalti.
Kwa
upande wa wasichana, Mwanza ndiyo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwa
njia ya penalti dhidi ya Ilala. Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo
uliochezwa jana (Septemba 14 mwaka huu) jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, jijini Dar es Salaam timu hizo zilikuwa suluhu.
Simba, Mtibwa waingiza Mil 102
Na Boniface Wambura
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa
jana (Septemba 14 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 95,080,000.
Watazamaji
16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa
2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao
2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18,
tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi
sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,730,958.34.
Mbunge Mtemvu awaga magodoro Temeke Hospitali
Mbunge wa temeke Abbas Mtemvu akikabidhi kwa Lucy Sozigwa ambae ni
katibu wa hospitali ya temeke moja ya magodoro 30 yaliotolewa na
kikundi cha akina mama wa Neema Woman's Power (NWP).
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akisalimiana na Mgeni Otto katibu wa
kikundi cha Neema Woman's Power(NWP) mara alipowasili katika hospitali
ya Temeke.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na Moshi Ndungu ,mjumbe halmashauri tawi la Azimio.
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akikabidhiwa magodoro 30 na Maryam Dedes ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha Neema Woman's Power (NWP)
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akikabidhiwa magodoro 30 na Maryam Dedes ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha Neema Woman's Power (NWP)
Mayweather Jr noumaa amtwanga Mmexico
Subscribe to:
Posts (Atom)