Na Boniface Wambura
TIMU
ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)
itacheza na Afrika Kusini katika mechi za mchujo kutafuta tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika kwa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini
Niger.
Serengeti
Boys ambayo pamoja na nchi nyingine 17 zimeingia moja kwa moja katika
raundi ya pili itaanzia mechi hiyo nyumbani kati ya Julai 18-20 mwaka
huu wakati ile ya marudiano itafanyika nchini Afrika Kusini kati ya
Agosti 1-3 mwaka huu.
Ikifanikiwa
kuitoa Afrika Kusini, Serengeti Boys itacheza mechi ya raundi ya tatu
na ya mwisho na mshindi wa mechi kati ya Misri/Sudan vs Congo
Brazzaville.
Nchi
nyingine ambazo zimeingia moja kwa moja raundi ya pili ni Afrika
Kusini, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville,
Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda,
Senegal, Tunisia na Zambia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kutangaza benchi la ufundi litakaloiongoza Serengeti Boys hivi karibuni.