|
Mtibwa Sugar iliyoipokea kichapo cha nne mfululizo leo kwa Mgambo JKT |
|
Kagera Sugar waliongára Kambarage kwa kuilaza Polisi Moro |
|
Polisi Moro wliopoteza mchezo wa pili leo mbele ya Kagera Sugar baada ya wiki iliyopita kulala kwa Simba 2-0 |
|
Ndanda iliyotakata nyumbani Mtwara kwa kuilaza Coastal Union 1-0 |
JAHAZI la Mtibwa Sugar linazidi kuzama baada ya kufungwa 1-0 na Mgambo JKT ikiwa ni mechi ya nne mfululizo kupoteza katika Ligi kuu Tanzania Bara.
Kipigo hicho cha Mtibwa kimeifanya timu hiyo kuzidi kuporomoka kwenye msimamo wa ligi hiyo wakisaliwa na pointi zao 19 baad ya mechi 15.
Bao lililoizamisha Mtibwa katika pambano hilo lililochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, liliwekwa kimiani na Malimi Busungu katika dakika ya 36 na kuifanya timu yao kufikisha pointi 17.
Katika mchezo mwingine ul;iochezwa Nangwanda Sijaona, wenyeji Ndanda waliinyuka Coastal Union kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Jacob Massawe katika dakika ya 79.
Aidha Kagera Sugar wakwia uwanja wa Kambarage Shinyanga wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani, iliendelea kutakata baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro.
Bao hilo pekee lililowapa ushindi Kagera na kuzidi kujikita nafasi ya tatu ikifikisha pointi 24 liliwekwa kimiani na Rashid Mandawa ambaye anafikisha bao lake la saba katika ligi hiyo, bao moja nyuma dhidi ya kinara wa mabao kwa sasa wa ligi hiyo Didier Kavumbagu wa Azam.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu, Yanga wakiwa uwanja wa Sokoine Mbeya kupapetana na Mbeya City, Simba watakuwa wageni wa Stand Utd mjini Shinyanga na Azam watauamana na Prisons Mbeya uwanja wa Chamazi.
Mechi hiyo ya Azam na maafande itachezwa saa 2 usiku na kila timu imetamba kujiandikishia ushindi katika pambano hilo.