STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 12, 2014

Rais TAFF amwagiwa sifa kwa kujitolea


RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba amemwagiwa sifa kwa kuwa mwepesi wa kujitolea kuwasaidia wasanii wenye matatizo, huku wasanii wengine wakiombwa kuiga mfano wake bila kujali uwezo wa mtu wa kifedha.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye msiba wa Mzee Small kutokana na namna Rais huyo wa TAFF alivyokuwa akihaha kuweka mambo sawa huku wasanii wa Bongo Movie wakiwa hawapo kwenye eneo hilo mpaka walipokuja baadaye majira ya mchana.
"Kwa kweli Rais wa TAFF, ni mtu wa watu anajitolea na amekuwa mwepesi kila wasanii wanapopatwa na shida ni mfano wa kuigwa na kufahamu wajibu wake kama kiongozi, wasanii wote wangekuwa hivi mambo yangekuwa mazuri sana," alisema mmoja wa wasanii wakiongwe aliyeomba kuhifadhiwa jina lake aliyekuwa msibani hapo mapema.
Mdau mwingine wa sanaa, alisema tofauti na wasanii wa Bongo Movie ambao huchagua aina ya misiba au wasanii wa kuwasaidia hali ni tofauti kwa uongozi wa TAFF na hasa Rais wake na baadhi ya waigizaji
wakongwe wakitajwa kwa majina, Dk Cheni, Chiki Mchoma, Monalisa na mama yake.

Baby Madaha ala 'shavu' Kenya

NYOTA wa filamu na muziki wa Tanzania anayefanya kazi zake nchini Kenya, Baby Madaha amelamba 'shavu' nono kupitia kampuni ya simu ya Safaricom.
Akizungumza na MICHARAZO toka nchini humo, Baby Madaha aliyeachia wimbo mpya uitwao 'Nawaponda' alisema karibu mwezi mmoja sasa anafanya 'tour' chini ya Safaricom, jambo alilofichua limempa ulaji mkubwa na kujitambulisha zaidi nchini humo.
"Nipo kwenye 'tour' ya Safaricom, ambapo napiga shoo sambamba na kuitangaza kampuni kwa kweli nashukuru sana kufanya kazi chini ya Candy n Candy', " alisema Baby.
Msanii huyo hata hivyo hakuweka bayana mkataba alioingia na kampuni hiyo maarufu ya simu za mkononi nchini humo, ila alidai ni mnono na kwamba umemfanya kujivunia kuwa msanii anayefanya kazi nchini Kenya.

Kipute cha Kombe la Dunia kuanza leo Brazil

Wenyeji Brazil watakaoanza mtihani wao leo dhidi ya Croatia
FAINALI za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza kutimka rasmi kuanzia usiku wa leo kwa wenyeji wa michuano hiyo Brazil itakapou
mana na Croatia. 
Brazil chini ya kocha Luis Fillipe Scolari na itakayokuwa ikimtegemea Neymar kulibakisha kombe hilo itakuwa na mtihani mbele ya Croatia.
Michuano hiyo itakayodumu kwa muda wa mwezi mmoja, itashuhudia mataifa 32 yakichuana katika kugombea nafasi ya kucheza fainali itakayofanyika Julai 13 jijini Rio de Janeiro. 
Mchezo huo wa ufunguzi utakaochezwa katika Uwanja wa Corinthians uliopo jijini Sao Paulo utatanguliwa na sherehe fupi ambazo zitakuwa na maonesho mbalimbali kuelezea uhalisia wa watu wa nchi hiyo na soka. 
Akihojiwa jana kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari aliwaambia wapenzi wote wa soka kwamba muda umefika, wanatakiwa kwenda pamoja kwasababu hilo ni Kombe lao la Dunia. 
Pamoja na shamrashamra za kuanza michuano hiyo, mwaka jana zaidi ya watu milioni moja waliingia mtaani katika miji mikubwa kwa ajili ya kuandamana kupinga kile walichokiita gharama kubwa za maandalizi ya michuano hiyo. 
Hata hivyo safari hii, rais wa Brazil Dilma Rousseff amesema hataruhusu maandamano kwa ajili ya kufuruga michuano hiyo ambapo maelfu ya polisi na wanajeshi wamepangwa ili kuhakikisha michuano hiyo inakwenda vyema.

Kajala aibuka na laana kivyake

Lamata aliyeiongoza filamu ya Kajala iitwayo Laana
BAADA ya kuzitumikia filamu za wenzake, hatimaye msanii Kajala Masanja amevunja ukimya akijiandaa kutoa kazi yake mwenyewe iitwayo 'Laana' kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment.
Muongozaji wa filamu hiyo, Leah Richard 'Lamata' alisema filamu hiyo ipo ambayo Kajala ameiigiza akishirikiana na wasanii wengine nyota ipo hatua ya mwisho kabla ya kuachiwa mtaani, ikiwa ni kazi yake ya kwanza binafsi.
Lamata alisema mkasa wa filamu hiyo ni simulizi linaloelekea kweli juu ya mambo yanayowapata baadhi ya wanajamii kiasi cha kushindwa kuamini.
Baadhi ya wasanii walioshirikishwa katika filamu hiyo ni Salim Ahmed 'Gabo', Farida Sabu 'Mama Sonia' na wengine.
"Tupo katika maandalizi ya mwisho kutoa filamu mpya na ya kwanza binafsi ya Kajala iitwayo 'Laana' imeshirikisha wakali kadhaa na ni bonge la filamu," alisema Lamata mmoja wa waongozaji bora nchini wa filamu kwa sasa.
Kabla ya kutoa kazi binafsi, Kajala alitamba na filamu za watu wengine alizoshirikishwa zikiwamo, Jeraha la Moyo, House Boy, Vita Baridi, House Girl & Boy, Dhuluma, Shortcut, Basilisa, You Me and Him na Devil's Kingdom ya marehemu Steve Kanumba iliyomshirikisha nyota wa kimataifa, Ramsey Nouah.

Soko la Karume lateketea



Pichani ni namna moto ulivyokuwa ukiteketeza soko la mitumba la Mchikichikini

Duh! Waganga wanaotibu wagionjwa kwa ngono wanaswa na Ch**i za kike



POLISI Mkoa wa Temeke, imewakamata vijana wawili wanaodaiwa kujifanya waganga wanaotoa tiba kwa wanawake, ambao masharti yake ni kushiriki nao ngono bila kinga na kuacha nguo za ndani, ili zifanyiwe dawa zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alidai vijana hao Juma Hemedi (32) na Abrahman Mulsin, wote wakazi wa Tandika, baada ya kushiriki ngono na wagonjwa wao huwaambia waache nguo za ndani.
Kamanda Kiondo alidai baada ya kupata malalamiko, Jeshi la Polisi ilianzisha msako na kuwapekua waganga hao, ambapo walikutwa na nguo za ndani za kike 22, ambazo alisema zitakuwa ushahidi wa kuingiliwa kimwili kwa wanawake hao. Vitu vingine wanavyodaiwa kukutwa navyo ni pembe, tunguli, makopo ya dawa na vibuyu.
 “Sheria iko wazi, inasema mganga anapofanya ngono kama uganga anakuwa amebaka, na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu 130 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,”alisema Kamanda Kiondo.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kiondo, vijana hao wamekuwa wakijifanya waganga wa tiba asili, husambaza vipeperushi sehemu mbalimbali za jiji kutafuta wateja.
Mbali na tiba hiyo ya kupata watoto, inayotolewa kwa kushiriki ngono na mganga, Kamanda Kiondo alidai watuhumiwa hao wamekuwa wakidai kutibu magonjwa mengine kama kisukari, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume, kukuza maumbile, kupata kazi, kufaulu mtihani, mvuto wa biashara, kumilikishwa jini na kupewa pete ya bahati.

Katika tukio lingine, Polisi inamshikilia kijana mwingine mkazi wa Tandika Devis Corner, Maalim Kimti  Rita au kwa jina lingine, Joseph Rita  anayedaiwa kutapeli Sh milioni 11 akijidai kumfanyia dua mfanyabiashara aweze kukuza biashara yake.

Alidai kuna mfanyabiashara mwanamke ambaye alitoa Sh milioni 11 kwa Maalim Rita, akidanganywa kuwa atafanyiwa uganga ili afanikiwe katika biashara yake, lakini alipoona hakuna alichopata, akaamua kutoa taarifa Polisi.

Kamanda Kiondo alisema jamii inapaswa kuelimishwa kuachana na mambo hayo, kwa sababu  tiba yake haipo kwa waganga wa jadi na kwamba hakuna uhusiano kati ya kufaulu na kwenda kwa waganga isipokuwa bidii ya kazi.

“Watu wengi wamelalamikia matukio ya namna hiyo, sasa tumeamua kuweka wazi kwa umma kwa kuwa watu wanateketea kwa kukosa elimu… watu wanauza nyumba magari na mali zao, kwa ajili ya kupata fedha za kupeleka kwa waganga wakiamini kuna tiba, huu ni utapeli vijana kama hawa hawawezi kukupa utajiri wala mtoto,” alisema Kamanda Kiondo.

Alisema waganga hao wamepata vyeti vya kufanyia kazi hiyo ya uganga wa jadi, lakini wanachofanya ni kinyume na kazi hiyo ambapo aliahidi vyeti vyao kuchunguzwa, kuona  wamevipataje na kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii, ili watambue pembe wanazotumia ni za mnyama gani. 



via Habari leo.