STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 26, 2013

Kichanga cha siku nne chaokotwa shimoni alikokaa kwa siku 6



UKISHANGAA ya Mussa basi utayaona ya Firauni, usemi huu umethibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe aliyekuwa amewekwa kwenye mfuko wa mbolea kisha kutupwa kwenye shimo kuokolea akiwa hai licha ya kuishi shimoni humo kwa sita sita.
 
Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamaria wema...
Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama  Salimini .
Yeyote Mwenye nafasi ya kumsaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba zifuatayo,  mchango  utafuatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima

Taifa Stars kwenda Ethiopia leo njiani kuifuata Morocco

 
Kikosi cha Stars
Na Boniface Wambura
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26 mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake kipa Juma Kaseja.

Timu hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.

Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.

Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Ommy Lax aachia mpya akisaka meneja

Ommy Lax katika pozi
MKALI wa wimbo wa 'Kioo Changu' alioimba na Matonya, Imani Omary 'Ommy Lax' ameachia wimbo mwingine mpya uitwao 'Wapotezee' huku akisaka meneja wa kuzisimamia kazi zake.
Akizungumza na MICHARAZO, Ommy Lax, alisema angependa kufanya kazi chini ya meneja ili kumuongoza katika majukumu yake baada ya mtu aliyekuwa akimtegemea ambaye ni mjomba wake, MP kuwa na majukumu mengine mazito binafsi.
"Natamani na ninasaka meneja wa kunisimamia kazi zangu, hivyo yeyote atakayekuwa tayari anaweza kuwasiliana nami tukae chini na kukubaliana, " alisema Ommy Lax.
Juu ya wimbo wake mpya, Ommy lax alisema ameimba na  mkali kutoka Watanashati, PNC na tayari umeanza kurushwa hewani.
Ommy Lax, alisema kazi hiyo mpya aliyorekodia kwa maprodyuza R Pino na The Timing, ni moja ya nyimbo kali kwa mwaka 2013.
Msanii huyo aliyejishughulisha na sanaa tangu akiwa shuleni na kutoa kazi ya kwanza mwaka 2006, alisema kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kutoa  video ya wimbo huo.
"Kaka nimepakua wimbo mpya uitwao 'Wapotezee' nilioimba na PNC, ni moja ya kazi bomba siyo mchezo mashabiki wasubiri kuisikia hewani na sasa nafanya mipango ya video yake, lakini muhimu naomba mtu ajitokeze anipige tafu kama meneja," alisema.

Madabida mgeni tamasha la vipaji



MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 litafanyika leo Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.

 

Peter Mwenda

                             

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.
Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .
Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,
 Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.
Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677

Kampuni ya Issere yatoa msaada wa jezi


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja mwakilishi, Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitengo cha kihalifu.


 

Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.

Abajalo kuonyeshana kazi na Kariakoo Lindi leo RCL







Na Boniface Wambura
Raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea tena leo (Mei 26 mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.

Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Nayo Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Twiga Stars waingia kambini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9qCbvL7ACfY-W273M78SjNwShyphenhyphento0pGY0jocv4YwPbT2si8HWRgx-R_CH50plR4aAhjyvtlT_RlMM3p55WStyP9sBPLbjbDHdB-_SW_dqsAbqS6oRTd0nBZTJOMDGRyTRgcDxKE7WB-Zm/s1600/Pix-1.jpg
Kikosi cha Twiga Stars

 
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.

Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao.

Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.

Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).

Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).

Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

Miss Tabata 2013 waenda Mikumi



WASHIRIKI wa wa Dodoma Wine, Redd’s Miss Tabata 2013 leo wanatarajiwa kwenda kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi.
Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga alisema warembo hao wataondoka na gari ya aina ya Toyota Double Coaster ikiwa na warembo 20 pamoja na walimu na viongozi wao.
Kalinga alisema ziara hiyo ina lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga ushirikiano miongoni mwao.
Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.
“Tutarudi Dar es Salaam Jumatatu kujiandaa na shindano letu litakalofanyika Ijumaa ijayo,” alisema Kalinga.
Kadhalika, Kalinga  alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na kampuni ya CXC Africa.
Shindano la kumsaka Miss Tabata  litafanyika Ijumaa ya Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Warembo hao ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

MSHAMBULIAJI NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO FC BARCELONA


 

Neymar akichuana na Messi wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu baina ya Barca na Santos mwaka juzi
Neymar akichuana na Glen Johnson wakati wa mechi baina ya timu ya taifa ya Brazil na England

Neymar (katikati) akikimbizwa na Gary Cahill (kulia) na Smalling (kushoto)

Neymar akionyeshana shughuli na Tom Cleverly
Karibu Barca mwana.... Neymar akipongezana na Lionel Messi baada ya mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka juzi. 

BARCELONA imefanikisha kumsajili mshambuliaji wa Santos, Neymar kwa dau linalokadiriwa kuwa euro milioni 28 leo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil atajiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kukataa ushawishi wa Real Madrid, ambao wanaamini kwamba walitoa ofa nono ya euro milioni 35.

Mshambuliaji huyo ataingiza malipo binafsi ya euro milioni 7 kwa mwaka, ambayo licha ya kwamba ni pungufu ya ambayo angepata Real Madrid, yatamshuhudia akipata malipo ya ziada kutokana na maafikiano ya mkataba na kampuni ya kimataifa ya vifaa vya michezo ya Nike.

Neymar amekuwa katika rada za klabu nyingi kubwa za Ulaya kwa miaka kadhaa baada ya kung'aa Amerika Kusini na aliingia kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2013.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa kama Chelsea, Bayern Munich na PSG, lakini Barcelona imeziacha mbali sana klabu hiyo kwa kupewa nafasi kubwa zaidi ya kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.

Mabingwa hao wapya wa La Liga, hata hivyo, wamewapiku mahasimu wao Real katika kumsajili Neymar ambaye atajiunga nao katika kipindi hiki cha usajili kujiandaa na msimu ujao wa 2013-14.

Kama sehemu ya dili hilo, Barcelona imeafiki kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Santos zenye thamani ya euro milioni 2 kila moja, hivi karibuni, moja kila bara - Amerika Kusini na Ulaya.

Klabuni Nou Camp, Mbrazil huyo atajiunga na nyota wenzake wanaotokea katika bara ya Amerika Kusini kama Lionel Messi, Alexis Sanchez, Javier Mascherano na nyota wenzake wa timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves na Adriano.

Neymar alipata kusema siku za nyuma kwamba anataka kusubiri kuhamia Ulaya hadi baada ya fainali za Kombe la Dunia 2014, lakini kutokana na mkataba wake kumalizika mwakani, Santos wamelazimika kumuuza ili mchezaji huyo waliyemlea tangu mdogo asije kuondoka bure.  

Bayern Munich waizima Dortmund na kutwaa Ubingwa Ulaya

Top of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia Dortmund
Wachezaji wa Bayern wakishangilia na taji lao la Ulaya jana

Dutch delight: Arjen Robben settled the Champions League final with a late, late strike
Aerjen Robben akishangilia bao lake
HUU ni msimu ni Bayern Munich! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mabingwa hao wa Ujerumani kunyakua taji la Ligi ya Ulaya usiku wa kuamkia leo kwa kuwanyuka mahasimu wao Borussia Dortmund kwa mabao 2-1.
Winga wa Kiholanzi, Arjen Robben ndiye aliyewahakikishia wakali hao wa Ujerumani ambao wamekuwa na msimu mzuri mwaka huu kwa kufunga bao dakika za lala salama la pambano hilo.
Robben alifunga bao katika pambano hilo la fainali lililochezwa kwenye uwanja wa Wembley, London nchini England na kuipa Bayern taji hilo lililokuwa halina mtu baada ya waliokuwa mabingwa watetezi, Chelsea kulitema mapema.
Mholanzi huyo alifunga bao hilo tamu dakika ya 89, na pia ndiye aliyetoa pasi ya bao la kwanza la mabingwa hao wapya wa Ulaya lilitumbukizwa kimiani na Mario Mandzukic katika dakika ya 60.
Dortmund iilijipatia bao lake dakika saba baada ya kutanguliwa kufungwa na wapinzani wao kupitia mkwaju wa penati wa Ilkay Gundogan baada ya Mario Reus kuangushwa langoni mwa Bayern na Dante.