Kampuni ya Issere yatoa msaada wa jezi
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere
(kulia) akimkabidhi jezi seti moja mwakilishi, Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu
ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo
vijijini.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Isere Sports imetoa
vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza
vijana katika wilaya ya Kondoa.
Akikabidhi vifaa hivyo jana,
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa
hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na
kujikinga na vitengo cha kihalifu.
Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa
ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na
soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa
wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya
vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi
waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa
vya michezo.
Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa
niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini
lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo
vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.
No comments:
Post a Comment