WASHIRIKI wa wa Dodoma
Wine, Redd’s Miss Tabata 2013 leo wanatarajiwa kwenda kutembelea
hifadhi ya taifa ya Mikumi.
Mratibu wa
shindano hilo Godfrey Kalinga alisema warembo hao wataondoka na gari
ya aina ya Toyota Double Coaster ikiwa na warembo 20 pamoja na walimu na
viongozi wao.
Kalinga alisema
ziara hiyo ina lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga ushirikiano miongoni
mwao.
Alisema kuwa
warembo hao pia watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo
kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.
“Tutarudi Dar es
Salaam Jumatatu kujiandaa na shindano letu litakalofanyika Ijumaa ijayo,”
alisema Kalinga.
Kadhalika, Kalinga
alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na kampuni
ya CXC Africa.
Shindano la
kumsaka Miss Tabata litafanyika Ijumaa ya Mei 31 katika ukumbi wa Da’
West Park, Tabata.
Wadhamini wa
shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs,
Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC
Africa, Brake Point na Saluti5.
Warembo hao ni Madgalena
Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),
Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema
Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga
(21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Anayeshikilia taji
la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Miss Tabata
inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
No comments:
Post a Comment