MABAO mawili yaliyofungwa na Tumba Sued moja likiwa la penati liliisaidia Ashanti United kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kujinasua mkiani wakiiachia Mgambo JKT ya Tanga.
Ashanti iliipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi kwa kuicharaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-1, bao la ushindi likifungwa dakika za jioni na kulalamikiwa na Wagosi wa Kaya.
Tumba Sued beki wa kati mmoja wa wachezaji chipukizi wanaotoka ukoo wa wanasoka kaka zake wakiwa ni Said Swued 'Panucci' na Salum Sued 'Kussi' alifunga bao la kwanza kabla ya Coastal Union kusawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia nahodha, Jerry Santo.
Mchezaji huyo mrefu aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini China, aliiongezea Ashanti bao la pili dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati na kuifanya Ashanti ifikishe pointi 5 sawa na Mgambo JKT, ambayo leo inashuka dimbani kuvaana na Mbeya City mjini Tanga.
Hata hivyo Ashanti wapo juu ikishika nafasi ya 13 kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa na kuiacha Mgambo ikiburuza mkia kwa sasa.
Matokeo ya mechi za jana pia zilibadilisha msimamo wa ligi kuu ambapo Yanga ilikwea hadi nafasi ya pili ikiwapumulia watani zao watakaovaana nao Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, huku Coastal ikijikuta ikiporomoka kwa nafasi moja hadi nafasi ya nane ikiiachia nafasi Ruvu Shooting ambaye hata hivyo jana haikushuka dimbani kwa leo leo itapepetana na Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Mabatini.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014 P W D L F A GD PTS
1. Simba 8 5 3 0 17 5 12 18
2. Yanga 8 4 3 1 15 8 7 15
3. Azam 8 3 5 0 11 6 5 14
4. Mbeya City 8 3 5 0 11 7 4 14
5. JKT Ruvu 8 4 0 4 9 7 2 12
6. Kagera Sugar 8 3 2 3 9 7 2 11
7. Ruvu Shooting 8 3 2 3 9 7 2 11
8. Coastal Union 8 2 5 1 7 5 2 11
9. Mtibwa Sugar 8 2 4 2 7 9 -2 10
10.Rhino Rangers 8 1 4 3 8 11 -3 7
11.Prisons 8 1 4 3 4 10 -6 7
12. Oljoro 8 1 3 4 6 10 -4 6
13.Ashanti 8 1 2 5 6 16 -10 5
14.Mgambo 8 1 2 5 2 13 -11 5
Wafungaji:
8- Tambwe Amisi (Simba
4- Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons), Kipre Tchetche (Azam), Elias Maguri (Ruvu Shooting)
3- Jerry Tegete, Hamis Kiiza (Yanga), Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Jerry Santo (Coastal Union), Tumba Sued (Ashanti Utd)
2- Haruna Moshi (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya (Mbeya City), Mrisho Ngassa (Yanga), Godfrey Wambura (Kagera Sugar)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla,(Coastal Union), Henry Joseph, Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris, John Bocco, Joseph Kimwaga, Faridi Maliki (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Peter Mapunda (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader, Said Dilunga (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Nditti, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG) (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary, Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)
Ratiba za Ligi Kuu
Leo
Ruvu Shooting vs Rhino Rangers (-)
Mgambo JKT vs Mbeya City (-)
Azam vs JKT Ruvu (-)
Mtibwa Sugar vs Oljoro JKT (-)
Okt 16, 2013
Ashanti Utd vs Prisons (-)
Okt 19, 2013
Kagera Sugar vs Coastal Union (-)
Oljoro JKT vs Azam (-)
Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT (-)
Mbeya City vs JKT Ruvu (-)
Ashanti Utd vs Ruvu Shooting
Okt 20, 2013
Simba vs Yanga