STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 13, 2013

Azam yaiengua Yanga, Mbeya City moto chini, Mtibwa yaua, Abdalla Juma apiga Hat Trick, Maguri naye kama kawa

Mbeya City

Azam Fc
MABINGWA watetezi Yanga imeenguliwa kwenye  nafasi ya pili na kuporomoka hadi nafasi ya nne kufuatia jioni hii timu za Azam na Mbeya City kupata ushindi katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Azam iliisasambua JKT Ruvu kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Chamazi, huku Mbeya City wakipata pointi tatu katika uwanja wa Mkwakwani kwa kuizabua Mgambo JKT kwa bao 1-0.
Ushindi wa timu hizo umezifanya Azam kurejea kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 17 sawa na za Mbeya City inayokamata nafasi ya tatu ila inawazidi uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam ilipata ushindi wake kwa mabao ya Humphrey Mieno katika dakika 12 kabla ya Erasto Nyoni kufunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 32 mabao yhaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kilipoisha.
Bao la tatu lililowanyong'onyesha JKT lilifungwa na kiungo Salum Abubakar Sure Boy dakika ya 90.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Elias Maguri aliendeleza kasi yake ya kufumania nyavu baada ya kuifungia Ruvu Shooting bao pekee katika pambano lao dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Maguri alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati baada ya Aypoub Kitala kurangushwa kwenye lango la Rhino na mfungaji huyo kufunga penati. Hata hivyo Ruvu ilipata pigo baada ya kiungo wake Juma Seif 'Kijiko' kulimwa kadi nyekundu.
Nayo Mtibwa Sugar ikiwa kwenye uwanja wa Manungu iliisambaratisha Oljoro JKT kwa kuifunga mabao 5-2, huku Abdsalla Juma akitupia kimiani mabaop matatu (hat Trick) na kuweka rekodi.
Maao mengi ya Mtibwa yalifungwa na Juma Luizio na kumfanya afikishe jumla ya mabao matano mpaka sasa.
Mabao ya kufutia machozi ya Oljoro yalifungwa na Saidi Nayoka na Amir Omar.

No comments:

Post a Comment