POLISI wawili wameuawa wakati watatu wakijeruhiwa mapema leo baada ya kuvamiwa na kundi linalodaiwa kuwa la Al-Shabab.
Tukio hili limetokea wakati Wakenya wakiwa katika maombolezo ya siku tatu kuwakumbuka watu zaidi ya 60 waliopoteza maisha na 175 kujeruhiwa katika shambulio la Jumamosi iliyopita kwenye jengo la biashara la Westgate.
Shambulio hilo limetokea mapema leo katika kituo cha ulinzi kilichopo karibu na mpaka wa Somalia, mjini Mandera.
Kamanda wa Polisi, Charlton Mureithi ameeleza kuwa mbali na polisi wawili kuuawa na watatu kujeruhiwa kundi hilo limechoma magari 11.
Tukio hili limetokea saa chache baada ya kundi la Al-Shabab kutoa taarifa kuwa mashambulio yataendelea mpaka Kenya watakapoondoa wanajeshi wake nchini Somalia.
Kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Godane Shaykh Mukhtar Abu Zubayr, alitoa onyo kwa Wakenya kuwa hakuna njia yoyote wangeweza "kuhimili vita ya kulipa kisasi ndani ya nchi yao wenyewe" katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao jana Jumatano.
"Chagua kuondoa majeshi yenu yote,.." Godane alisema. "Vinginevyo jiandae kwa wingi wa damu itakayomwagika nchini kwenu, anguko la kiuchumi na makazi."
STRIKA
USILIKOSE
Thursday, September 26, 2013
TANZIA! Mwanahabari Venance George afariki dunia
TASNIA ya Habari imepata pigo baada ya Mwandishi wa Habari wa magazaeti ya kampuni ya Mwananchi Communication Limited mkoa wa Morogoro, Venance George (Pichani anayeangalia kamera) kufariki dunia leo mchana katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa toka Morogoro marehemu aliyewahi kuyaandikia pia magazeti ya Uhuru na Mzalendo alifariki na mipango ya mazishi inaendelewa kufanywa na familia yake ikishirikiana na MCL.
MICHARAZO inatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa pamoja na wanahabari wote hususani kampuni ya MCL kwa msiba huo na inawatakia subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuwakumbusha 'mwenzetu katangulia nasi tu nyuma yake'
'BWANA AMETOA NAYE NDITYE ALIYETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE'
Credit:Juma Mtanda
Kamati TFF yawakomalia Shafii Dauda na wenzake
Shafii Dauda mmoja ya waliotoswa jumla ya TFF |
KAMATI
ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza
hukumu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake kwa kumsafisha
mlalamikiwa mmoja, kutowaadhibu zaidi washtakiwa sita na kuahirisha
kusikiliza shauri moja baada ya mlalamikiwa kutokuwepo.
Riziki
Juma Majala, ambaye ni Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani
(COREFA) ndiye pekee aliyesafishwa na Kamati ya Maadili dhidi ya
mashtaka ya kutoa kauli zilizosababisha kufunguliwa kwa kesi dhidi ya
TFF.
Vilevile
Kamati imesita kuwachukulia hatua Shafii Dauda, Nazarius Kilungeja,
Wilfred Kidao, Omar Isaak Abdulkadir na Kamwanga Tambwe kutokana na
kuridhika kuwa wameshaadhibiwa kwa kuenguliwa kwenye uchaguzi, hivyo
hawawezi kuadhibiwa mara mbili.
Pia
imesema haiwezi kumuadhibu Richard Julius Rukambura, aliyeshtakiwa kwa
kukiuka Katiba ya TFF kwa kosa la kufungua kesi mahakamani, baada ya
kubaini kuwa si mwanafamilia wa TFF kutokana na kuenguliwa kwenye
uchaguzi.
Hoja
hiyo pia ilitumika kutomchukulia hatua Dauda na mwamuzi wa zamani Omar
Abdulkadir kwa hoja kuwa walipoteza sifa za kuwa wanafamilia wa TFF
baada ya kuenguliwa kwenye uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi.
Shauri
la Omary Mussa Mkwaruro la tuhuma za kutumia cheti cha elimu
kisichotambuliwa na mamlaka husika, limeahirishwa kutokana na
Mlalamikiwa kutowasilisha utetezi wake, hivyo Kamati imeagiza
Sekretarieti kuwasiliana naye ili awasilishe maelezo yake.
Watu
hao walifikishwa mbele ya Kamati ya Maadili baada ya kujitokeza kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi wa TFF na baada ya usaili walibainika kuwa
na matatizo ya kimaadili, hivyo ili iamue juu ya hadhi yao katika
familia ya mpira wa miguu kwa kuwachukulia hatua au kuwaweka huru.
Katika
hukumu iliyotolewa leo (Septemba 26 mwaka huu), Kamati ya Maadili
imeeleza kuwa Majala hakiuka Kanuni za Maadili kwa kuwa vielelezo
vilivyowasilishwa na TFF vinaonyesha kuwa klabu ya Kiluvya United
imesajiliwa na Serikali na vyama wanachama wa TFF.
Kuhusu
Rukambura, ambaye alilalamikiwa kwa kuipeleka TFF kwenye mahakama ya
kiraia, hivyo kukiuka Kanuni ya 73 (3) (b) ya Kanuni za Maadili, Kamati
imesema ushahidi uliowasilishwa na TFF hauonyeshi kama mgombea ni
mwanafamilia wa TFF; alishaondolewa katika uchaguzi na hivyo si kati ya
wagombea na hivyo mikono ya Kamati kufungwa kwa mujibu wa kanuni ya pili
ya Kanuni za Maadili.
Kamati
pia imeeleza kuwa Kanuni ya 73 (3) ambayo ingepaswa kutumika
kumchukulia hatua, chimbuko lake ni Ibara ya 75 ya Katiba ya TFF ambayo
inawalenga wanachama tu na hivyo kuamua kuwa malalamiko hayo hayana
mashiko na kwani Rukambura alishapoteza sifa za kuwa mwanafamilia na
hivyo kushindwa kumchukulia hatua.
Kidao
alishtakiwa kwa kosa la kumiliki nyaraka za Kamati ya Utendaji kinyume
na taratibu na pia kuwasilisha malalamiko yake Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) bila ya kufuata taratibu, lakini Kamati imesema
kwa vile mlalamikiwa ameenguliwa kwenye uchaguzi, anatumikia adhabu ya
kinidhamu na hivyo haiwezi kumuadhibu mara mbili.
Kuhusu
Shafii Dauda, Kamati imesema malalamiko dhidi yake hayana mashiko kwa
kuwa si mwanafamilia wa TFF na kwamba lalamiko dhidi yake linatupiliwa
mbali kwa kuwa tayari ameshaondolewa kwenye uchaguzi kutokana na kosa la
kinidhamu.
Kamati
iliona hakukuwa na haja ya kushughulikia mashauri dhidi ya Nazarius
Kilungeja, ambaye alishtakiwa kwa kukaidi maagizo ya vyombo halali vya
TFF, na Kamwanga Tambwe kwa kuwa tayari wawili hao wanatumikia adhabu ya
kufungiwa na Kamati ya Nidhamu.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Simba yamruka Okwi yatoa ufafanuzi ujio wake Dar
Emmanuel Okwi enzi akiichezea Simba |
KLABU ya
Simba inapenda kutoa taarifa zifuatazo kwa umma kuhusu masuala yanayoihusu kwa
sasa.
Kuhusu Emmanuel Okwi
KATIKA
siku za karibuni, vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimeripoti kuhusu
uwepo nchini wa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu, Emmanuel Arnold Okwi
kutoka nchini Uganda.
Taarifa
hizo zimeeleza mambo mbalimbali ikiwamo taarifa kuwa Simba Sports Club ina
mawasiliano na mchezaji huyo na alikuja kwa mwaliko wa viongozi wa klabu.
Baadhi ya vyombo vimekwenda mbali zaidi na kudai kuwa uongozi wa Simba
unamshawishi mchezaji huyo avunje mkataba wake na klabu anayoichezea sasa ya Etoile
du Sahel (ESS) ya Tunisia.
Klabu
inapenda kuuarifu umma kwamba Simba au kiongozi wake yeyote (Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Sekretarieti haijahusika kwa namna
yoyote ile na ujio wa mchezaji huyo hapa nchini. Hakukuwepo na mwaliko rasmi au
usio rasmi kwa viongozi wa Simba.
Taarifa
zozote za kuhusisha ujio wa Okwi na uongozi wa Simba ni za upotoshaji na zina
lengo la kuharibu heshima na hadhi ambayo uongozi huu umeijenga kitaifa na
kimataifa kwenye tasnia ya soka.
Hata
hivyo, kisheria, Simba haiwezi kumzuia mchezaji huyo kusafiri kwenda nchi
yoyote anayotaka kama amefuata sheria zote za uhamiaji. Mchezaji huyo ana
mkataba na timu nyingine na Simba haihusiki na safari zake, matembezi yake au
mipango yake ya kimaisha.
Uongozi
wa Simba unafahamu kwamba Okwi ni mchezaji halali wa ESS maana wenyewe ndiyo
uliomuuza kwa klabu hiyo. Kwa mujibu wa sheria za FIFA, klabu yeyote, ikiwamo
Simba SC, haziruhusiwi kufanya mawasiliano na mchezaji huyo au yeyote yule
halali wa klabu nyingine bila ruhusa ya klabu yake kama mkataba wa mchezaji
husika umebakiza kipindi kinachozidi miezi sita. Hii maana yake ni kwamba
uongozi hauwezi kumshawishi mchezaji huyo kujiunga na klabu.
Ikumbukwe
kwamba hadi sasa, klabu ya Simba, inaidai klabu ya Etoile du Sahel kiasi cha
dola za Marekani 300,000 (laki tatu) ambazo zinapaswa kuwa zimelipwa kabla ya
tarehe 30 mwezi huu wa tisa mwaka 2013. Kinyume cha hapo matokeo mengine
yataamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya FIFA ambapo
makubaliano husika yalisajiliwa.
Uongozi
wa Simba ungeomba vyombo vya habari na watu binafsi waache kutoa taarifa zozote
za kuhusisha ujio wa Okwi na klabu au kwamba kuna mipango ya kumshawishi avunje
mkataba wake kwani taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Imetolewa
na
Ezekiel Kamwaga,
Ofisa Habari,
Simba Sports Club
'Ulimbukeni unawasumbua wana hip hop'
Ile Ile |
Ile Ile alisema siyo kweli kama mtu kuwa msanii wa hip hop ni lazima awe mtemi, mfanya fujo na anayejihusisha na matumizi ya pombe au dawa za kulevya isipokuwa wanaofanya hivyo wanasumbuliwa na kasumba ya kuiga mambo tu.
"Binafsi sikubaliani na mambo yanayofanywa na baadhi ya wasanii wa miondoko ya Hip Hop ya kufanya fujo, kujitia wababe na matukio mengine ya ovyo, naamini wanaofanya hivyo wanasumbuliwa na ulimbukeni wa kuiga kila jambo bila kujali kama ni zuri au la ama linaloendana na utamaduni wa Kitanzania," alisema.
Ile Ile anayetamba na nyimbo kama 'Ile Ile', 'Bora Liende' na 'Wazazi' aliouachia hivi karibuni, alisema mila na tamaduni za hip hop ni amani na upendo na kukomboa wengine sna kuhoji ni vipi sasa wanahip hop kupenda kuwanyanyasa wengine.
Alisema ni lazima wasanii wa miondoko hiyo wajaribu kuepuka mambo hayo ambayo alidai yanachangia kuufanya muziki huo kuchukuliwa kama wa wahuni ilihali karibu dunia nzima inakombolewa na harakati za wanahip hop.
Msanii huyo alisema pia japo kila mtu ana uhuru wake wa kutumia kitu chochote, bado wasanii wanapaswa kuepuka matumizi ya ulevi na dawa za kulevya kwani ndizo zinazochangia wengi wao kuwa wakorofi na kuharibu sifa za hip hop.
Ajali tena! moja afa kwa kugandamizwa na gari wanne hoi
Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashidi Seleman mkazi wa
Isevya manispaa ya Tabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori
walilokuwa wamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda
Kigwa.
Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva
ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya
ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti
ya mtu huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali
ya kampuni ya mkandarasi JOSSAM
Awali jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki
wakiiangalia maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea
majira ya saa kumi jioni hapo jana.
Askari wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi cha
usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye
wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya
mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX
Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX
MDODOSAJI
Mtibwa Sugar wapo tayari kwa vita sasa
Mecky Mexime |
Aidha kocha huyo alisema pamoja na Ashanti United kuonekana kama timu dhaifu katika ligi hiyo watashuka dimbani katika mechi baina yao siku ya Jumapili kwa tahadhari kubwa na bila kuidharau ilimradi kuhakikisha wanapata ushindi.
Akizungumza na MICHARAZO, Mexime, nahodha wa zamani wa timu hiyo ya Mtibwa na Taifa Stars, alisema benchi lao la ufundi tayari limeshagundua wapio walipokuwa wamekosea katika mechi zao zilizopita na kujipanga upya kuianza ligi.
Mexime, alisema kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Simba na sare mbili dhidi ya timu za Mbeya City na Prisons za Mbeya vimewafanya wajipange upya kwa kurekebisha makosa yao na sasa wapo tayari kwa vita katika ligi hiyo.
"Tumejipanga upya kwa kuangalia wapi tulipokuwa tunakosea na kurekebisha na sasa tupo tayari kwa vita, hatutakubali kuona tukipoteza tena pointi japo hatuwezi kuidharau Ashanti United tutakaovaana nao Jumapili hii jijini Dar," alisema.
Kocha huyo alisema wataenda uwanja wa Chamazi kwa tahadhari kubwa dhidi ya Ashanti Utd bila kuidharau kwani wanaamini ni timu ngumu na inayoweza kufanya lolote iwapo watawapuuza katika pambano hilo.
Kuhusu kikosi chake, Mexime alisema kinaendelea vyema na hakuna mchezaji yeyote majeruhi kitu kinachompa faraja kwamba watapata pointi tatu muhimu kwa ajili ya kuwatoa nafasi ya tisa waliopo na kurejea nafasi za juu walizokuwa awali.
Mtibwa Sugar katika mechi zake tano ilizocheza mpaka sasa imeshinda mechi moja tu na kupoteza moja huku tatu ikipata sare na kukusanya pointi 6 sawa na Yanga walioopo juu yao wanaotofautiana nao kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba 'kamili gado' kuiua JKT Ruvu
KLABU ya soka ya Simba imetamba kuwa wapo kamili gado kwa ajili ya 'kuiua' JKT Ruvu watakaokutana nao kwenye pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili, licha ya kukiri wanatarajia kupata upinzani mkali kwa wapinzani wao hao.
Simba wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 11 na JKT Ruvu waliopo nafasi ya pili wakiwa na poini zao 9 watavaana kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa ligi hiyo iliyopo raundi ya sita.
Benchi la ufundi la Simba limekiri kutambua ugumu wa pambano hilo dhidi ya JKT Ruvu, lakini limetamba kuwa hawana hofu yoyote kwa vile kikosi chao kipo fiti ikiwamo kuendelea vyema kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio', aliiambia MICHARAZO kwa njia ya simu jana akiwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach, Kigamboni kuwa, kikosi chao kipo tayari kwa vita ya Jumapili ili kuimarisha uongozi wao.
Julio alisema wanajua wanakutana na timu ngumu, lakini wanajipanga ili kuweza kuvuna pointi zote tatu na kuendelea kujikita kileleni baada ya mechi yao iliyopita kupata sare ya mabao 2-2 mbele ya 'wageni' Mbeya City ya Mbeya.
Kocha huyo mwenye maneno mengi alisema kwa kuwa lengo la Simba msimu huu ni kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kuupoteza msimu uliopita kwa watani zao Yanga, hawatafanya makosa kwa JKT au klabu yoyote watakayokutana nao.
"Kambi yetu inaendelea vyema ikiwamo wachezaji waliokuwa majeruhi wakiendelea vyema na imani yetu tutapata ushindi kwa JKT Ruvu ili kuendelea kukaa kileleni, japo tunajua litakuwa pambano gumu mno," alisema Julio.
Julio aliongeza pamoja na kukiamini kikosi chao, hawaidharau timu yoyote katika ligi hiyo na badala yake watakuwa wakishuka dimbani kama wanacheza fainali muhimu kuvuna pointi zitakazowasaidia mbele ya safari.
KARAMA NYILAWILA KUZIPIGA OCTOBA 20
Karama Nyilawila |
Nyilawila aliyempiga Kreshnik Qato wa Czech wakati akitwaa taji lake la WBF ambalo alilitema baada ya kushindwa kwenda kulitetea ili apate nafasi ya kuzipiga kirafiki na Francis Cheka mjini Morogoro na kudundwa, atazipiga na Philemon kwenye ukumbi wa CCM Mwinjuma siku ya Oktoba 20, pambano lililoandaliwa na kampuni ya Bigright
Promotion.
Mratibu wa pambano hilo, Ibrahim kamwe alisema kuwa
maandalizi mpaka sasa yanaenda vizuri.
Hata hivyo Kamwe alisema mabondia wanaendelea kujifua kimkandamkanda kutokana na kukosekana kwa wadhamini na hasa mabondia watakaosindikiza pambano hilo.
Kamwe alisema Nyilawila na mwenzake wameshasaini makubaliano ya kupanda ulingoni siku hiyo ambapo watasindikizwa na michezo kadhaa itakayohusisha mabondia chipukizi.
AIRTEL YAPIGA JEKI MBIO ZA ROCK CITY MARATHON
Meneja
Matukio wa Capital Plus, Mathew Kasonta (kulia) akifafanua jambo wakati
wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Katikati
ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando na Ofisa Uhusiano CP, Geofrey Nangai.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando akionesha fomu za
kujisajili kushiriki mbio hizo. Kulia ni Meneja Matukio wa Capital
Plus, Mathew Kasonta na Ofisa Uhusiano CP, Geofrey Nangai.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Airtel ya Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa mara ya tano mfululizo imetangaza kudhamini mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zilizopangwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27, Oktoba 2013 ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya mchezo wa riadha nchini.
Airtel
imekuwa mdhamini mkuu kwa upande wa mawasiliano katika mbiyo hizo,
wakishirikiana na wadhaminiwa wengine kama NSSF, Africa Barrick Gold
(ABG), Precision Air, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza
Hotel, Sahara Communications pamoja na Umoja Switch, ili kutoa fursa ya
kuinua mchezo wa riadha inchini.
Akizungumza
wakati wa tukio fupi lililofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini
Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson
Mmbando alisema kampuni yake imejidhatiti kusaidia shughuli mbali mbali
za maendeleo ya jamii na mbio za Rock City Marathon pia ni fursa pekee
ya kukuza vipaji katika michezo huo kwa ujumla.
“Kampuni
ya Airtel Tanzania kwa mwaka wa tano mfululizo, leo hii tunatangaza
udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
jitihada zetu za kusaidia maendeleo ya michezo nchi nzima.
“Tunaamini
kuwa mchango wetu utasaidia katika kuvumbua vipaji vipya
vitakavyoshiriki si tu kwa mashindano ya kitaifa lakini pia na ya
kimataifa,” alisema.
Mmbando
aliongeza kuwa washiriki kwa mwaka huu wataweza kusajili moja kwa moja
kupitia huduma ya kampuni yake ya Airtel Money kwa kutuma malipo yao kwa
neno MARATHON na kuhifadhi ujumbe kwa ajili ya kuuonyesha wakati wa
kuchukua fomu katika vituo mbali mbali.
Kwa
upande wake mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew
Kasonta wakati wa tukio alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa na
bora zaidi kwa kuleta pamoja washiriki kutoka ndani ya nje ya nchi.
“Kwa
mwaka huu tumeungana na kampuni ya Airtel lakini kupitia Airtel Money
ili kutanua wigo wa ushiriki zaidi. Katika miaka iliyopita, watu wengi
wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki au wakilazimika kusafiri umbali
mkubwa kwenda kwenye vituo vichache tulivyoviandaa ili waweze kununua
fomu za usajili, kwa kupitia Airtel Money zoezi hili litakuwa
limerahisishwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Kasonta.
Kasonta
aliongeza, “ukishamaliza zoezi hilo, utapokea ujumbe utakaouonyesha
pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu
ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na
Mwanza.”
Alisema
kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata fomu
zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika ofisi
za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu,
upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.
Kasonta
alibainisha kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei
vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi
3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi).
Alisema
kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu
wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa
miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.
Cheka mdogo, Shauri kumaliza ubishi Oktoba 27
Mabondia Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka wakitunishiana misuri wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa UBO Dar es salaam utakaofanyika tarehe 27 mwezi wa kumi
Pamoja
na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na
vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa zawadi kwa mabondia
na Kocha Super D ambaye ameahidi kutoa vikinga meno, bandeji, bukta, na dvd za mafunzo kwa mabondia na vifaa mbalimbali kwa mabondia
watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi
Promota
wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono
juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana
tarehe 27 Mwezi wa kumi jijini Dar es Salaam
|
MPAMBANO mwingine wa masumbwi unatarajia kufanyika Oktoba 27 katika ukumbi
wa Friends Coner Manzese Dar es salaam litakalo wakutanisha mabondia
Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka mpambano huo ulidhaminiwa na Hotel ya
Tanamera ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani
Akizungumza
mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju amesema amepata sapoti katika
hotel hiyo ili aweze kuendeleza vipaji vya vijana unakumbuka mimi ndie
ninae andaaga mapambano makubwa nchini kama utakumbuka ila nilisimama
kidogo kwa ajili ya kutafakali na kulekebisha mambo yangu binafsi lakini
kwa sasa nimekuja kuinua mchezo huu kwa vijana chipkizi kwanza ndio
msingi wa ngumi duniani kote
Aliongeza
kwa kutaja mapambano ya utangulizi kuwa ni Mohamed Matumla anamenyana
na Sadiki Momba huku Amosi Mwamakula akizichapa na Hamisi Ajali na Juma
Fundi atazipiga na Shabani Kilumbelumbe
Siku
hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia
wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama. Manny Pacquaio, Saul
'canelo' alverez, Floyd Mayweather, Mike Tyson, Muhammed Ali, Ferex
Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
TPBF yalia ngumi kudhalilishwa
Na Suleiman Msuya
SHIRIKISHO la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBF) limesema linasikitishwa na watu ambao wanadhalilisha mchezo wa ngumi hapa nchini kwa maslahi yao binafsi.
Kauli hiyo ya masikitiko imetolewa na Rais wa TPBF Chatta Michael wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Rais huyo alisema baada ya pambano la bondia Francis Cheka kupigana mwezi mmoja uliopita yameibuka makundi ya watu ambao wanaonekana kuwa na mikakati yao binafsi jambo ambalo halipaswi kunyamaziwa kwani linaweza kuleta picha mbaya kwa nchi.
Alisema kitendo cha Cheka kuibuka bingwa katika mpambano huo wa dunia ingetakiwa iwe ni sehemu ya nchi kuungana ili kuhakikisha kuwa fursa hiyo haiondoki kirahisi na iwe ni moja kufungua njia ya ujio wa mabondi wengine.
Michael alisema baada ya mpambano huo hadi sasa wamejitokeza mabondia kutoka nchi za Mexico na Australia kuhitaji kupambana na Cheka kutokana na kuridhishwa na kiwango chake.
“Napenda kutumia fursa hii kuzungumza na jamii ya kitanzania ambayo inafuatilia mchezo huu wa ngumi kuwa ni vema kuachana na maneno ya baadhi ya watu ambao wapo kwa nia ya kupotosha hali ambayo inaweza kuathiri dhima nzima za wadau wenye nia ya kukuza mchezo huo,” alisema.
Rais huyo alisema mikakati ambayo ipo ni kuhakikisha kupitia shirikisho la Ngumi la Dunia (WBF) Tanzania inapata mapambano mengi makubwa ya kimataifa ili kuweza kukuza vipaji vya vijana ambao wapo tayari.
Alisema TPBF imejipanga vilivyo ili kuweza kushirikiana na WBF ili kuhakikisha kuwa mchezo wa ngumi Tanzania unapiga hatua kwani ni moja ya mchezo ambao unatoa fursa za mafanikio kwa haraka.
Azam Tv yamkosha Julio
KOCHA Msaidizi wa timu ya Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' ameipongeza kampuni ya Azam TV kwa kitendo chao cha kuongeza udhamini katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kitu alichodai kimesaidia kuongeza ushindani katika ligi tofauti na zamani.
Julio alisema udhamini huo wa Azam TV ambao umezihusisha timu zote umesaidia kuondoa ligi ya timu chache na ndiyo maana mpaka sasa kumekuwa na matokeo ya kushangaza hata kwa timu ambazo zilikuwa zikionekana kama nyonge.
Akizungumza na MICHARAZO, Julio alisema udhamini mpya wa Azam umezifanya kila timu kuwa na maandalizi mazuri na ari ya kutaka kufanya vyema katika ligi kitu ambacho kimesababisha baadhii ya timu zilizozoea 'kupeta' kuwa na wakati mgumu.
"Kama mdau wa soka naipongeza kampuni ya Azam Media kwa uamuzi wake wa kuongeza udhamini katika ligi, imeifanya ligi kuwa tamu na yenye ushindani wa kweli kitu ambacho kitasaidia kupanda kwa soka la Tanzania," alisema.
"Ule utamaduni wa timu ndogo kuwa wanyonge mbele ya timu kubwa ni kama sasa unaondoka na hiki ni kitu kizuri kwa mustakabali wa soka letu, hivyo nawapongeza na kutaka wengine wajitokeze kusaidia kuinua soka la Tanzania," aliongeza Julio.
Alisema anaamini ushindani uliopo katika ligi msimu huu utasaidia kutoa mabingwa na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa wanaostahili na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika anga hizo badalaya kuwa wasindikizaji tu,
"Ligi inapokuwa ngumu na yenye ushindani inasaidia kutoa mabingwa wa kweli na wanaostahili ambao wataiwakilisha vyema kimataifa, hivyo narejea kuipongeza Azam Media walichokifanya na kuomba wasapotiwe na kila mtu," alisema Julio.
Kampuni hiyo ya Azam Media imeingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh. Bilioni 6 ambapo kila klabu ya ligi itakuwa ikivuna Sh Milioni 100, hiyo ni mbali na udhamini wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom
Julio alisema udhamini huo wa Azam TV ambao umezihusisha timu zote umesaidia kuondoa ligi ya timu chache na ndiyo maana mpaka sasa kumekuwa na matokeo ya kushangaza hata kwa timu ambazo zilikuwa zikionekana kama nyonge.
Akizungumza na MICHARAZO, Julio alisema udhamini mpya wa Azam umezifanya kila timu kuwa na maandalizi mazuri na ari ya kutaka kufanya vyema katika ligi kitu ambacho kimesababisha baadhii ya timu zilizozoea 'kupeta' kuwa na wakati mgumu.
"Kama mdau wa soka naipongeza kampuni ya Azam Media kwa uamuzi wake wa kuongeza udhamini katika ligi, imeifanya ligi kuwa tamu na yenye ushindani wa kweli kitu ambacho kitasaidia kupanda kwa soka la Tanzania," alisema.
"Ule utamaduni wa timu ndogo kuwa wanyonge mbele ya timu kubwa ni kama sasa unaondoka na hiki ni kitu kizuri kwa mustakabali wa soka letu, hivyo nawapongeza na kutaka wengine wajitokeze kusaidia kuinua soka la Tanzania," aliongeza Julio.
Alisema anaamini ushindani uliopo katika ligi msimu huu utasaidia kutoa mabingwa na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa wanaostahili na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika anga hizo badalaya kuwa wasindikizaji tu,
"Ligi inapokuwa ngumu na yenye ushindani inasaidia kutoa mabingwa wa kweli na wanaostahili ambao wataiwakilisha vyema kimataifa, hivyo narejea kuipongeza Azam Media walichokifanya na kuomba wasapotiwe na kila mtu," alisema Julio.
Kampuni hiyo ya Azam Media imeingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh. Bilioni 6 ambapo kila klabu ya ligi itakuwa ikivuna Sh Milioni 100, hiyo ni mbali na udhamini wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom
Vodacom yazipiga tafu Shule 12 vifaa vya michezo
KAMPUNI ya VODACOM Tanzania imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 11kwa shule 12 za Sekondari katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa na lengo la kukuza mchezo wa soka kuanzia ngazi za chini.
Msaada huo umekabidhiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa VODACOM Tanzania Kelvin Twissa kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mkandara leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waanahabari Twissa alisema msaada huo ni mwendelezo wa kampuni yao katika kuhakikisha kuwa michezo inakuwa nchini kuanzia ngazi ya chini ambapo wanatarajia kuendelea na mikoa mingine.
Twissa alisema VODACOM pamoja na ukweli kuwa imekuwa ikisaidia sekta mbalimbali ila michezo ni sehemu kubwa ya ufadhili wao wakiamini kuwa ni sehemu ambayo inahusisha jamii kubwa.
“Mh. Waziri napenda kukuambia baada ya majadiliano yetu ya muda tumeweza kutoa msaada huu kwa kuanza ambapo zipo jezi pea 12 na mipira 40 jambo ambalo litaweza kuleta tija kwa sasa,” alisema.
Kwa upande Waziri Mkandara alisema wizara yake imefarijika sana kwa kupata msaada huo kwani ni moja ya malengo yao ya kukuza michezo kwa kushirikiana na wadau wengine.
Alisema lengo lao ni kuhakikisha kuwa michezo inachezwa kila wakati katika maeneo yote ya nchi hasa kwa kuanzia ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kuwa na mwelekeo mzuri wa kimichezo.
Dk. Mkandara alisema mashindano hayo ya majaribio yatahusisha Wilaya tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa kila Wilaya kutoa shule nne za sekondari ambao michezo miwili ya mpira wa pete na mpira wa miguu.
Waziri alisema michezo ni ajira, afya na pia inajenga akili hivyo ni vyema kwa kuanzia ngazi ya chini ili iweze kuwaathiri vijana wakiwa wadogo.
Aidha waziri alitoa rai kwa wadau mbalimbali na taasisi kujitokeza kusaidia michezo mbalimbali kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kufikia malengo ya kukuza michezo hapa nchini.
Cash Money watoa msaada TMK Hosp, Gurumo naye...
Wana kikundi cha Cash Money wakiwa tayali kwa kutoa msaada katika hospitali ya Temeke |
Mlezi wa Kikundi cha Cash Money ,Ratifa Masasi kulia akimkabibi muhuguzi wa wodi ya watoto bi, Nuswe Ambokile zawai mbalimbali walizoleta kwa ajili ya watoto waliolaza katika hospital ya Temeke |
Baadhi ya wana kikundi cha Cash Money wakiwa katika picha ya pamoja na wahuguzi wa word ya watoto Hospitali ya temeke baada ya kukabidhi msaada |
Na Mwandishi Wetu
MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda
jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za
heshima.
Gurumo atatoa burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki,
ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money,
la Tandika mjini Dar es Salaam.
"Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo
katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na
nyimbo zake.
Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga
hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi
mlezi wa kundi hilo.
Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz
Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu
zikiwemo Coast na G Five.
Kundi la Cash Money ambalo lilianzishwa mwaka 2011, pia limetoa vitu
mbalimbali kwa wodi ya watoto, na vituo vya watoto yatima jana, ikiwa
ni sehemu ya uzinduzi huo
Mlezi wa kikundi cha Cash Money akimfaliji mama Samir Nassoro, Naomi Ramadhani walipokutana wakati kundi hilo likitoa msaada kwa wagojwa katika hod ya watoto |
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Cash Money wakimfariji Bi Naomi Ramadhani |
Msanii wa bendi ya Msondo ngoma Saddy Ally katikati akisalimiana na wanakikundi cha cash money walipokutana katika hospitali ya Temeke wakitokea kutoa msaada |
Wana kikundi wa chass money kushoto Amina Uredi 'Mmanyema ' na Zulfa Kasongo |
Uwanja wa Taifa sasa hata kwa Kitchen Party, serikali yafunguka
Na Suleiman Msuya
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo imetoa wito kwa Wananchi ambao wanapendelea kuingia uwanja wa Taifa
kushughudia michezo na shughuli zingine za kijamii wawe watunzaji wa rasilimali
zilizopo katika uwanja huo.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara hiyo Godblease
Malisa wakati akizungumza na mwandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema ni vema kila mpenda michezo kuwa sehemu ya
kulinda na kutunza uwanja huo kutokana na ukweli kuwa gharama kubwa zilitumika hadi
kupatikana kwake.
Malisa alisema serikali inajitahidi kutunza na
kuboresha huduma uwanja hapo ili kuhakikisha kuwa unakuwa wa salama na bora kwa
muda wote ili vizazi vijavyo viweze kufaidika.
“Napenda kuwaomba wanamichezo na wasio wanamichezo
kuutunza uwanja wetu wa Taifa ili uweze kudumu kwa muda mrefu pia ni vema
tutambue kuwa uwanja huo ni wa gharama kubwa,” alisema.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa
viwanja vya michezo vinakuwa bora na vinatumika wakati ote hali ambayo itakuwa
ni sehemu ya kukuza michezo hapa nchini.
Msemaji huyo alisema uwanja mkubwa wa Taifa
unahitahiji gharama kubwa za kuutunza hivyo ni vema kwa wadau ambao wanauomba
kuutumia katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Aidha Malisa aliwataka wananchi kutumia uwanja huo
kwa shughuli mbalimbali kama za mikutano na sherehe za harusi kwani una kumbi
za kutosha na nzuri kwani ni vigumu kwa uwanja huo kujiendasha kwa mapato ya
mechi zinazochezwa.
Malisa alisema pamoja na uwanja wa Taifa pia
Serikali inaendelea na maboresho ya uwanja wa Uhuru, ujenzi wa uwanja wa ndani,
mabwawa ya kuogolea yenye viwango vya olimpiki na hosteli.
Subscribe to:
Posts (Atom)