Emmanuel Okwi enzi akiichezea Simba |
KLABU ya
Simba inapenda kutoa taarifa zifuatazo kwa umma kuhusu masuala yanayoihusu kwa
sasa.
Kuhusu Emmanuel Okwi
KATIKA
siku za karibuni, vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimeripoti kuhusu
uwepo nchini wa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu, Emmanuel Arnold Okwi
kutoka nchini Uganda.
Taarifa
hizo zimeeleza mambo mbalimbali ikiwamo taarifa kuwa Simba Sports Club ina
mawasiliano na mchezaji huyo na alikuja kwa mwaliko wa viongozi wa klabu.
Baadhi ya vyombo vimekwenda mbali zaidi na kudai kuwa uongozi wa Simba
unamshawishi mchezaji huyo avunje mkataba wake na klabu anayoichezea sasa ya Etoile
du Sahel (ESS) ya Tunisia.
Klabu
inapenda kuuarifu umma kwamba Simba au kiongozi wake yeyote (Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Sekretarieti haijahusika kwa namna
yoyote ile na ujio wa mchezaji huyo hapa nchini. Hakukuwepo na mwaliko rasmi au
usio rasmi kwa viongozi wa Simba.
Taarifa
zozote za kuhusisha ujio wa Okwi na uongozi wa Simba ni za upotoshaji na zina
lengo la kuharibu heshima na hadhi ambayo uongozi huu umeijenga kitaifa na
kimataifa kwenye tasnia ya soka.
Hata
hivyo, kisheria, Simba haiwezi kumzuia mchezaji huyo kusafiri kwenda nchi
yoyote anayotaka kama amefuata sheria zote za uhamiaji. Mchezaji huyo ana
mkataba na timu nyingine na Simba haihusiki na safari zake, matembezi yake au
mipango yake ya kimaisha.
Uongozi
wa Simba unafahamu kwamba Okwi ni mchezaji halali wa ESS maana wenyewe ndiyo
uliomuuza kwa klabu hiyo. Kwa mujibu wa sheria za FIFA, klabu yeyote, ikiwamo
Simba SC, haziruhusiwi kufanya mawasiliano na mchezaji huyo au yeyote yule
halali wa klabu nyingine bila ruhusa ya klabu yake kama mkataba wa mchezaji
husika umebakiza kipindi kinachozidi miezi sita. Hii maana yake ni kwamba
uongozi hauwezi kumshawishi mchezaji huyo kujiunga na klabu.
Ikumbukwe
kwamba hadi sasa, klabu ya Simba, inaidai klabu ya Etoile du Sahel kiasi cha
dola za Marekani 300,000 (laki tatu) ambazo zinapaswa kuwa zimelipwa kabla ya
tarehe 30 mwezi huu wa tisa mwaka 2013. Kinyume cha hapo matokeo mengine
yataamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya FIFA ambapo
makubaliano husika yalisajiliwa.
Uongozi
wa Simba ungeomba vyombo vya habari na watu binafsi waache kutoa taarifa zozote
za kuhusisha ujio wa Okwi na klabu au kwamba kuna mipango ya kumshawishi avunje
mkataba wake kwani taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Imetolewa
na
Ezekiel Kamwaga,
Ofisa Habari,
Simba Sports Club
No comments:
Post a Comment