Kwa hakika kwa Mcha Mungu ni haramu kwake kuiadhimisha sherehe hiyo kutokana na ukweli ni siku ya KIPAGANI na inayokinzana na MAFUNDISHO YA MUNGU MWENYEEZI iwe kwa Ukristo ama kwa Uislam.
Hata hivyo ni vema tuongelee kidogo nini maana ya Valentine kwa asili yake kisha kila mtu kwa IMANI yake na mapana yake akatambua na kujiamulia kwa nafsi yake ama kukufuru au kumshukuru aliyemuumba.
Maneno hayo aliyoyasema Mtume Muhammad (SAW) hakika yamethibiti kwa sababu imedhihirika Waislamu kuigizia mila,
desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii
inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).
Na
baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa
katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe
(e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.
Na Mwenyezi Mungu anasema kuwa "Hawatakuwa Radhi Mayahudi na Manaswara kuwaona mpaka mfuate mila zao"
Baadhi ya Waislam na wasio waislam wapo kwenye harakati za kujiandaa na siku hiyo wajifuata mkumbo bila kujua kile wanachokisherehekea ebu tujifunze;
Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya ValentineSherehe hii ya wapendanao ni sherehe ya wapagani wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita.
Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya 'mapenzi ya kiroho'
Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo.
Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikma.
Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa.
Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi.
Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa.
Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawili wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani.
Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.
Kufungamana kwa Mt. Valentine na Sherehe Hii
Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo.
Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu.
Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius.
Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.
Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya 'mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni 'mapenzi ya mashujaa' yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani.
Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.
Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza.
Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.
Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana.
Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri.
Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa.
Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.
Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake.
Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 CE.
Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).
Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 CE kuwa ni sikukuu ya mapenzi.
Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la 'universal church', ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.
Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo.
Hii itukumbushe kauli ya Allaah
"Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu"At-Tawbah: 31
Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Katika Sikukuu Hii
1- Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.
2-Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, 'mapenzi ya kiroho' ya wapagani au 'mapenzi' ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni 'Sikukuu Ya Wapendanao'.
3-Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za 'mungu wa mapenzi wa kirumi' ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?
4-Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi.
Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema 'Kuwa Valentine wangu'.
Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.
5-Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.
Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea?
Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu 'Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah na kama tunavyojua kuwa Allaah Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo:
"Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa" (An-Nisaa: 48).
Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.
"Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru"-Al-Maaidah: 72.
Tunamuomba Allaah Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuonyeshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn
Special Al Hidaya
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Friday, 13 February
2015
VALENTINE NI NINI?
Leo nimeona niongelee kidogo nini maana ya Valentine kwa asili yake
kisha kila mtu kwa Imani yake na mapana yake akatambua kuwa anapokuwa
sehemu ya Valentine Day anakuwa ana adhimisha nini na kwa sababu gani
wengi tunasheherekea kama sio kuadhimisha Valetine Pasipo kujua asili
yake.
Valentine’s Day kama Sikukuu Ya Kipagani:
Valentine’s Day si siku ya Sikuu ya Kikristo, hata kama jina lake asili
yake inatokana na Ukristo haiwezi kuhalalisha sasa Valentine kuwa Siku
Ya Kikristo. Tukiangalia suala sikukuu hii kwa jicho la tatu, hatuoni
uhusiano mkubwa kati ya watu wa Mungu na Malove dove yaani mapenzi.
Kuna mambo mengi yanaweza ibua mjadala na kutokuelewana miongoni mwa
jamii ya wakristo na wasomi juu ya chimbuko ya Siku ya wapendanao al
maarufu Valentine’s Day. Hatutaweza kamwe kuwa na uwezo wa kuwa na jibu
muafaka kuhusu uhalali wa kusheherekea valentine kwa namna moja ama
nyingine kutokana na tofauti za kitamaduni na kidini ili mwisho wa siku
tujenga upya hadithi kamili na madhubuti, lakini uhusiano kipagani hadi
sasa na nguvu zaidi kuliko wale wa Kikristo kwa namna yoyote ile.
Februari 14 & Juno Fructifier au Juno Februata (February 14th &
Juno Fructifier or Juno Februata)
Enzi hizo Warumi walikuwa wakisheherekea kwa kupumzika kabisa kama
sikukuu ya muungano ama sikukuu zozote za hapa bongo kila Februari 14
kama siku ya kutoa heshima kwa Juno Fructifier. Huyu Juno Fructifier
alikuwa nani?huyu alikuwa Malkia wa miungu ya Kirumi ambaye alikuwa
Mungu mke kama mmoja wapo wa miungu ya ndoa kama ndo zilikuwa zinasua
sua basi tarehe 14 February ndo ilikuwa kama siku ya kufanya matambiko.
Enzi hizoilikuwa Katika sherehe moja, wanawake walikuwa wakiwasilisha
majina yao na kuweka kwenye kisanduku na baadae wanaume wangepita mbele
ya kisanduku hicho na kila mmoja kujitwalia jina moja. Kilichokuwa
kinatokea katika sherehe kila aliyejiokotea jina hulitaja na kujitwalia
huyo mwanamke kuwa mwanandoa kwa muda wote wa sikukuu wakati mwingine
ilikuwa ni mwanandoa wako kwa mwaka mzima mpaka Valentine nyingine
akaweke jina pale kwenye kibox. Mila hii ilitumika kukuza Jamii ya
Kirumi kwa maana ya uzazi na maisha mengine kwa ujumla, kasheshe kama
ulibeba ile ya mwaka mzima then Valentine imefika kisha unataka
kubadilisha halafu uliyembeba mwaka jana mjamzito tehe tehe imekula
kwako.
St Valentine, Padri Wa Kikristo (St. Valentine, Christian Priest)
Kulingana na hadithi za zamani, Mfalme wa Kirumi mwenye jina Claudius II
ilipiga marufuku juu ya ndoa kwa sababu enzi hizo vijana wengi walikuwa
wakiojitwalia wake mapema ili kukimbia jeshi maana amri ilikuwa mtu
ambaye hana mke hana familia ndo alikuwa anapaswa kuingia jeshini maana
hana cha kupoteza yuko mwenyewe tuy tehe tehe. Sasa kuna Padri mmoja wa
Kikristo aitwaye Valentinus yeye ndo alikuwa kazi yake kufungisha hizo
harusi kisirisiri maana inaonekana walikiuwa wakimpoza na mwisho wa siku
huyu padri akahukumiwa kunyongwa. Wakati akisubiri kunyongwa, Wapenzi
Vijana (Couples) walimtembelea na kumwandikia kitu kama barua kama sio
waraka kuwa ni namna gani ndo ni tamu kuliko Vita ya kwanza vya dunia na
vya pili.
Valentine Mwingine.
Valentinus mwingine alikuwa Padri nae alifungwa jela kwa ajili ya
kusaidia Wakristo. Wakati akiwa bado yuko jela huyu kuhani aka fall in
love na binti mlinzi wa gereza na wakati karibu anakwenda kunyongwa
akaandika ujumbe “From Your Valentine” . Habari zake zikahifadhiwa na
kuripotiwa Papa Julius I na baadae alijenga nakshi nakshi juu ya kaburi
lake.
Wakristo Wajibinafsishia Valentine’s Day:
Katika mwaka wa 469 wa kutawala kwake Gelasius alitangaza Februari 14
siku takatifu kwa heshima ya Valentinus tajwa hapo juu badala ya kuwa
siku ya kipagani ya mungu Lupercus wa Kirumi. Hapa ndo Wakristo wa enzi
hizo wakachakachua sikukuu hiyo na kuruhusu kuchukua baadhi ya
maadhimisho ya siku ya mapendo na ngono ambapo awali mambo hayo yalikuwa
katika mazingira ya upagani. Si ajabu kwenye Valentine hii ukaona Guest
House zimejaa, madukani watu wananunua condom hawajui kuwa kuadhimisha
huko hawajaanza wao ila ni zile imani za kipagani. Maadhimisho ya
kipagani yalikuwa lazima yaitimishwe kwa tendo la ngono ili kuonesha
kilele cha upendo. Na njia rahisi iliyokuwa ikitumika katika
kusheherekea siku hii ni ile ya kuweka majina kwenye kibox kisha kilaini
unajibebea huku “mungu” Shahidi akisimamia zoezi zima. Kwa maana ya
kwamba hakuna mtu atakaye okota jina bahati mbaya kuna roho
inayomuongoza mtu kuchagua jina fulani.
Valentine Day Yageuka kuwa Siku Ya Wapendanao.
Kama ambavyo tumeitazama siku ya Valentine wala haikuwa siku ya
wapendanao ilikuwa sikukuu ya Kipagani, ila baadae ikachakachuliwa hapo
ikawa ya Kikristo lakini ni kama upagani ndani yake. Ilipokuwa Wakati wa
Uamsho kwente Karne ya 14 ambapo tamaduni zikaanza kupewa tena
shamrashamra za Kitaifa, ndipo Valentine ikapewa shavu la kuwa siku ya
wapendanao. Ndipo katika kipindi hiki watu wakaachana na makatazo ya
kidini wakati huo na yale mafundisho ya msingi katika dini yakapewa
kisogo na watu wakageukia matamanio yao.Nyaraka na nyimbo mbali mbali za
kuhusu mapenzi, ngono na kujamiiana vikaenea katika kizazi hicho kama
ilivyo sasa kila nyimbo ni mapenzi hata picha za mabango ya barabarani
ni mapenzi kwenda mbele.
Valentine na Kibiashara Zaidi.
We utaona tu valentine hii ubepari unavyoshika hatamu yake katika
kutumia ili tu “Wapenzi” Wakolezee eti Valentine Day. Kuna watu
watanunua nguo mpya nyekundu ili mradi tu watupie kitu chekundu,
mijihela mingine itapelekwa kununulia zawadi za wapenzi, hapo sijahesabu
maua yatakayonunuliwa siku ya valentine, hapo sijaongelea chakula cha
usiku cha wapenzi, hapo sijaongelea wale watakao amua kwenda kulala.
Kama kuna siku nzuri ya biashara basi Valentine inakaribiana na
Christimas.
Mtazamo Wangu na Valentine Za Kibongo.
Nakubaliana na wale ambao siku hiyo watatumia kuwapongeza ndugu zao
wazazi wao na wapenzi wao. Swali la kujiuliza hapa “tuna adhimisha” ama
“tunasheherekea” Valentine?kama tuna adhimisha siku hii, lazima ujue
unachoadhimisha, kipi kati yapo juu unachoadhimisha?kama unasheherekea
unashehereka nini?otherwise tunakuwa busy na sikukuu tusiyoijua.
Ukitaka lawama valentine we usinunue zawadi, usimtoe mtu dinner,
jikaushe kama jumanne zingine tu za kawaida. Kwa Mtazamo wangu mdogo
nimebaini “Valentine Day” Wanawake ndo wako excited nayo kuliko Wanaume.
Kwanini?Kwa wale wanaume wasio waaminifu siku hiyo wengi hu opt
kupumzika nyumbani ili kuondoa lawama. How?Unajua wanaume wengi ndio
wanao cheat sasa anapotaka kwenda outing anajua msala unaweza kutokea.
Ila kwa wale wanao tazamia kusheherekea ama kuadhimisha siku hii kwa
namna yoyote ile basi nina wasiwasi wa baadhi ya watu kukimbiwa
kidizaini siku hii, na wengi pasipo kujua kuwa kuna roho nyuma yake
watajikuta wakiadhimisha kwa ngono kama ishara ya upendo kumbe ni ile
ibada ya kipagani tuliyoisoma hapo juu. Abiria chunga mzigo wako kwenye
Valentine.
Swali la Kujiuliza Kuna madhara yoyote ya Mkristo kusheherekea Sikukuu
Ya Valentine?
SPECIAL THANKS TO SAM SASALI.
Posted by Sophia Mbeyu at 00:36
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
No comments:
Post a Comment
Links to this post
Create a Link
Older Post Home
Translate
Powered by Translate
PLACE YOUR ADS HERE
PLACE YOUR ADS HERE
TANGAZO: UNAHITAJI VIATU WASILIANA NASI HAPA
TANGAZO: UNAHITAJI VIATU WASILIANA NASI HAPA
UNAHITAJI BOFYA PICHA HII KUONA PICHA ZAIDI
About Me
My Photo
Sophia Mbeyu
View my complete profile
Blog Archive
Popular Posts
MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2014 YAMETOKA, INGIA HUMU KUONA
DK. CHARLES E. MSOND E AKITANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA MAPEMA
HII LEO OFISINI KWAKE,MSONDA AMESEMA MATOKEO YA MWAKA HUU UFAURU WAKE
...
MITINDO YA VITENGE KWA WANAWAKE NA WANAUME...
KAMA INAVYYONYESHA PICHA! VAZI LAKITENGE LAWEZA KUTUMIWA KAMA VAZI
LA OFISI AMA CASUAL SIO LAZIMA KITENGE KIWE N...
MITINDO YA VITENGE KWA WOTE,.... WADAU WA VITENGE KILA WIKI KUNA
POST YA VITENGE FUATILIA POST ZA NYUMA KUPATA MITINDO MBALIMBALI
ZAIDI...
MITINDO YA VITENGE KWA AKINA DADA NA WATOTO..
MITINDO YA VITENGE
Mitindo ya Vitenge inaweza kushonwa katika dizain mbalimbali, hii
inaonyesha mitindo kwa vijana ni katika kuonyesha kuwa kitenge si lazima
...
MITINDO BOMBA YA VITENGE!
Huhitaji nguo za majina kupendeza, kitu cha kitenge tosha kabisa
kukutoa bomba!
MITINDO MBALIMBALI YA VITENGE, VIATU NA HANDBAG ZA KITENGE....
MITINDO YA VITENGE KWA AKINA DADA NA WATOTO!
MITINDO YA VITENGE KATIKA MATUKIO TOFAUTI...
MITINDO YA VITENGE
Labels
African day 2008 may
AMUUA BABA YAKE KUMUOKOA SHANGAZI YAKE ALIYEKUWA ANABAKWA-
NACHINGWEA
ARIEL SHARON AFARIKI
ASEMA YADHOOFISHA UCHUMI AFRIKA
aswira Kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar:Rais wa
Comoro Awasili Zanzibar Kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya
Mapinduzi
BAADA YA BASI KUGONGA NA KUUA WATATU
BABA NA MWANA JAY-Z NA MWANAE BLUE IVY..
Biza mupulu artist
Biza mupulu Botswana
BREAKING NEWS: FIFA YAHAMISHA MUDA WA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022 HUKO
QATAR
HABARI ZA KIMATAIFA/ WAUMINI WAUAWA MSIKITINI NCHINI NIGERIA
HABARI ZA UMBEYA/. WAKATI WEMA AKITUMA VIDEO YA DIAMOND AKIWA
KITANDANI
HAKUNA KAMA MWANAMKE
HAPO NAPO SASA
IGP ATANGAZA MABADILIKO MAKUBWA JESHI LA POLISI.
IJUMAA NJEMA WADAU WA SOPHIEMBEYU BLOG....
IMETANGAZWA RASMI KESHO NI SIKU YA MAPUMZIKO KUSHEHEREKEA MAPINDUZI:
Kundi la FM Academia
KUTWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA NJE YA AFRIKA
Machael Jackson kuaga dunia
MADAWA YA KULEVYA YAINGIZWA SUPERMARKET KATIKA MAKASHA YA NDIZI
MAGAZETI YA LEO IJUMAA 10 JANUARY 2014
Magonjwa ya mlipuko yanukia jijini Dar
MAN UNITED YAZINDUKA
Mariam bongo
MAWAZIRI WAPYA WATANO WATAJWA TANZANIA
MITINDO YA NYWELE
MITINDO YA VITENGE
MKAPA AIPONDA MISAADA KUTOKA NJE
MSIKIE JOKATE AKIONGELEA MUZIKI NA FILAMU.......
Mwekezaji abomoa nyumba za wananchi wa Mkuyuni-Morogoro ili kupisha
ujenzi wa Majosho.11 jan mgogoro
Nondoz wa Bongo waliokamilisha kisomo chao Data India.
Pablo Machine Familia dar
Pablo Machine na watoto
Pablo Machine na wakenya kwenye festival
Pablo Machine Sabiti
PENNY NAE ANENA "HAITATOKEA KAMWE NIKAMDHARAU DIAMOND
PICHA ZA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKISAFIRISHA SILAHA ZA KIVITA
KATAVI
PICTURE OF THE DAY..KWA RAHA ZAO
Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Aendelea Kutunuku Nishani
Rihanna out in Barbados
RWANDA YAKANUSHA UVUMI KUHUSU KIFO CHA KAGAME
SABABU YA KIFO CHA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA
TASWIRA MBALI MBALI KATIKA SHEREHE YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR
LEO 12/01/2014
UNAKANDAMIZA ...
VAZI LA LEO
Wa Bongo
WAFANYABIASHARA WA DAR WAGOMEA MASHINE ZA KODI ZA TRA
WAFUNGA MADUKA LEO
Wakali bongo hawo
WANANCHI WALITEKETEZA BASI KWA MOTO
WAZIRI KIGODA : MFUMO MASHINE EFDs NI MBOVU
WEEKEND NJEMA WADAU WA SOPHIEMBEYU BLOG....NAWAPENDAAA MINGIIII.
WEMA NI MAMA KIJACHO? SOMA ALICHOANDIKA HAPO
Wizara ya maliasili na utalii imewasimamisha kazi watumishi wake 22
wa idara ya wanyama pori
YAICHAPA 2-0 SWANSEA CITY
Yatima Dar walilia madarasa yakujisomea
PLACE YOUR ADS HERE
PLACE YOUR ADS HERE
powered by
Slideshow
Sikiliza clouds radio
SIKILIZA KWANZA JAMII RADIO
Followers
Google+ Followers
Total visitors
Total Pageviews
Sparkline 1515131
CLOCK & CALENDAR
buy research paper custom essay writing answering service care
February 2015
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
Free Counter
Counter Free
PLACE YOUR ADS HERE
PLACE YOUR ADS HERE
WEBSITES & BLOGS
MICHUZI
JIACHIE
BONGOBLOGS
TanzMED
Wavuti
Allyshams
Myummah76
Francis Godwin
Globalpublishers
Full Shangwe
Ladyjaydee
Swahili TV
TMF
Haki Ngowi
Mimi na Tanzania
Mo Blog
Chadema Blog
CCM Blog
January Makamba
Zitto kabwe
Habari Leo
Daily News
Mwananchi
Mtanzania
Tanzania Daima
Raia Mwema
Majira
Mwanaspoti
The Citizen
Daraja Letu
IPP Media
Bashir Nkoromo
BBC Swahili
Sauti ya Amerika
Jamii Forums
BLOG DEVELOPMENT
BLOG DEVELOPMENT
AUDIO BAR
SIKILIZA BRAND NEW TRACK HAPA!!
VIDEO BAR
UNATAKA KUPUNGUA UZITO!!
CLICK THIS IMAGE
Contact Form
Name