Na Boniface Wambura
MECHI
ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya
Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana
(Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.
Fedha
hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128
waliokata tiketi.
Viingilio
vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho
kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000
ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.
Mgawo
ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya
uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh.
28,990,500.
Mechi
iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano hayo kati ya Azam na El
Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16
mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku
ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.